Mwakinyo ni miongoni mwa wanamuchezo wenye majibu ya majivuno

Maboxer ndivyo walivyo Mohammed Ali kua ni greatest boxer of all time. Ila mlishawahi msikia akiwa anajikubali na maneno ya shombo anayoongea kuhusu wapinzani wake? Yaani Mwakinyo akasome Ali alikua anashombo zaidi la pale Ferry.
Tupe baadhi ya shombo zake alizowahi kusema, msiwe mnamtetea kwa kigezo eti hata mabondia wakubwa walikuwa wanafanya hivyo
 
Zile ngumi za kichwani hua zinawafanya madishi yayumbe.
Inaenda ikawa au wanakula vikali..? Maana hawajambo kwa majigambo mara sipiganii gari nina gari tatu moja nawapeleka mbwa wangu baharini kuwaosha kila wiki. How come..?
 
Nishawahi kumsikia EFM mwaka jana alikuwa anajibu kwa dharau sana na kama majivuno hivi. Akiulizwa swali rahisi tu anajibu kwa mkato sana. Sidhani kama watakuja kumualika tena.
Na uzuri wa watanzania mimi nawajua na wanasubiri apigwe hata pambano moja ndo watakuja kumsagia kunguni

Mimi nasema anachokitafuta Mwakinyo atakipata tu
 
Dogo anapewa plomo sana lakini hamna kitu alafu anajiskia sana
Kuna kitambo alisema anamtaka mayweather apigane naye maana mayweather eti anapigana kibishoo hivyo kwake co kitu. [emoji1787][emoji1787][emoji1787] nikajisemea anataka kuvunjwa fuvu sasa
 
Sasa hapo dharau inatoka wapi......... ni maneno ya mabondia tu
 
Ni kawaida kwa mabondia wote duniani,ata kabla ya pambania unajua siku hiyo lazima upigwe na bado unatamba lazima umnyonyoe mtu ,fanani lazima kuongeza nyodo kwa hadhira
 
Inahitajika akili sana kutofautisha ukweli na dharau...!
 
Akili za watanzania wengi ziko kiushabiki zaidi, mnataka kuuchukulia mchezo wa boxing kama ugomvi wa mitaani.

Mwakinyo yuko sahihi 100%, huwezi kuanza kupigana kisa unatafuta uonekane mbabe mitaani badala ya kujenga maisha yako.

Akiwaelewesha mnasema anadharau, kapiganeni nyie sasa.
 
USD m2 per fight? Umeitolea wapi hii habari?
Aliyopigana na terrence mbona jamaa anaishi USA kabisa ingawa ni mnamibia? huamini kwamba hizo hela zipo? m cuba aliyempiga PAQUIAO juzi hakuzoea kupata hela nyingi ila juzi kachukua usd millions 3 baada ya kumpiga Manny ingawa yeye manny alichukua 10 usd millions
 
Haya hapa maneno yake ndugu.... Nawasilisha



View attachment 1919102
Umwagaji wa shombo ndo sisi wapenzi wa boxing tunaopendezwa nao mwaga shombo then mtu akijichanganya mnyooshe kweli kweli kama Mwakinyo anavyoninyooasheaga watu na huyo Twaha akue kwanza asiote kupigana na Kilerrkinyo ajue atapigwa kipigo Cha jibwa jizi yaan watanga watamroga hadi arogeke haswa akifika kwenye ring kipigo tu halafu akimaliza kupokea kipigo Killerrkinyo anatamba haters sijui mtaeka api sura zenu
 
Kumbukeni kumtakia mtu mabaya haitoshi kufanya mtu huyo aharibikiwe mungu ndo anaamua Mwakinyo watambie Washamba wasiojua thaman ya ngumi wanazozivumilia kwenye ring mabondia kama kina Twaha ndo wanaofanya bongo boxing ichelewe kulipa na mabondia wetu kulalamika njaa na kufa maskin Mwakinyo is a true definition of modern boxer in Tanzania revolution anayoifanya itakuja kukumbukwa siku moja
 
Maboxer ndivyo walivyo Mohammed Ali kua ni greatest boxer of all time. Ila mlishawahi msikia akiwa anajikubali na maneno ya shombo anayoongea kuhusu wapinzani wake? Yaani Mwakinyo akasome Ali alikua anashombo zaidi la pale Ferry.
Hii ni entertain business boxer halafu ukiwa mpole kama askofu hufiki mbali haya majigambo ndio sehemu ya mchezo utakuta matusi na majigambo lakini baada ya pambano wanakumbatiana tu na mfano wa Mohd Ali mtu mzuri lakini kwenye majigambo unaweza kumchukia bure.
 
Yuko sahihi, boxing ni kama drafti vile, vitambo muhimu, acha atambe kama wanataka wajitahidi wafike alipo, bondia wa 4 star akapigane na 2 [emoji93], anajaribu kuilinda hadhi yake, kiduku kama kweli anataka apigane na kidunda kwanza.
 
Jamaa atakua anatumia hela zake vibaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…