Elections 2010 Mwakipesile atangaza rasmi kutokugombea ubunge wa Kyela 2010

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2006
Posts
4,816
Reaction score
684
Hili wengine tuliandika tokea mwaka jana kwamba Mwakipesile hana mpango tena wa kugombea ubunge wa Kyela.
 
Kaona hataiweza tsunami ya mwana wa watu -- Dr HM. Sababu nyingine ni blah blah tu.
 
hivi hao maaskofu na viongozi wa kisiasa na serikali vipi?Yaani Askofu mzima anauliza swali la kijinga hivyo..Badala ya kuuliza ni lini serkilai itaaacha kukumbatia mafisadi au ni lini serikali italeta maendeleo?

Na mie nikirudi nitawaita
 
Enyi wenzetu wa mwaka 1930 kweusi na 1940 kweupe, ndoto za kudhani mnaweza kuhimili mikimiki ya kwenye majukwaa mwazitoa wapi?

Mwakipesile is history as far as Kyela politics is concerned. Ashukuru na aendelea kuimba wimbo wa 'ameniona, ameniona ...." kwa kupewa ukuu wa Mkoa.
 
2010 around ze corner

Wanaoona na kusoma alama za nyakati mapema ni bora wafanye hivyo la sivyo...............watahaibika.

Aibu yetu....................... Aibu yao ...........Aibu yao mwenyewe........

Na Bado tutasikia wengi
 
Hah ha ha ha,

Mwakipesile amegonga jackpot hapa kwenye PR. Kwa sasa hata isemwe nini, yeye kishatangulia na kusema kuwa hagombei.

Si-hasa mchezo mchafu
 
Hah ha ha ha,

Mwakipesile amegonga jackpot hapa kwenye PR. Kwa sasa hata isemwe nini, yeye kishatangulia na kusema kuwa hagombei.

Si-hasa mchezo mchafu

Mwakipesile aliwaambia Wapambe wake mwishoni mwa 2006 kwamba hatagombea ubunge tena Kyela. Wengi hawakuamini, hata mimi nilifikiri ni kama kawaida ya wanasiasa na kwamba baadaye angebadilika tu maana hata tunaowajua hapa JF nao wamebadilika na kuanza kusema wananchi wamewabembeleza.

Sababu alizotoa ni hizo hizo kwamba kupewa kuwa mkuu wa mkoa kwake ni faraja kubwa. Nafikiri alionja joto ya jiwe kwenye ubunge na sasa anaona anafaidi pesa za kwenye siasa bila bugudha za wananchi.
 
Bado siamini....Mh Kagasheki alisema haya baadaye akakanusha...Hata Mzee Kaunda alikuja kujikana mwenyewe akagombea uraisi Zambia na kupata aibu. Mwakipesile 2010 atakuja na visingizio wazee wameniomba and all those bla bla....!
 
Masanilo,

Sitashangaa akibadilika, ila pia anajua kura zake hazitatimia 2010 kwasababu Kyela wakikutema mara moja sahau hiyo ya kurudi tena.

Mwaka kwenye politics ni muda mrefu sana, anaweza kuja na visingizio kibao vya kugombea, ndio siasa hizo, wanafikiri sisi wananchi ni wajinga na hatufikiri.
 
hivi hao maaskofu na viongozi wa kisiasa na serikali vipi?Yaani Askofu mzima anauliza swali la kijinga hivyo..Badala ya kuuliza ni lini serkilai itaaacha kukumbatia mafisadi au ni lini serikali italeta maendeleo?

Na mie nikirudi nitawaita

Rudi tu mapema ndugu, inaelekea wewe huna habari jinsi ufisadi/mafisadi walivyotumia vyombo vya dola katika vinyanganyiro tofauti mkoani Mbeya.
Hawa Maaskofu wako katibu sana na wananchi(kwa taarifa yako wanakutana kila jumapili).
Si jambo la kushangaza kwamba katika michakato ya kisiasa Mkuu wa Wilaya Kyela tayari ametemwa.Mkuu Mwakipesile amefanya jambo la busara kutamka na mapema azma yake ya kutogombea.
 
Kainzi kalikoazimwa toka kwa Mwanakijiji kamefanikiwa kuliona file la DC aliyeondolewa Kyela. Madai makubwa ni umalaya na kwamba eti alikuwa anatumia gari la serikali kufuata watoto wa shule mpaka kule Malawi. Hiyo taarifa iliandaliwa kule ofisi ya PM.

Kama kuthibitisha madai yao wakaweka na case yake ya kufumaniwa na mkewe. Hapo ngoma ikawa imeisha, jamaa akapigwa nje.

Siasa bwana kazi kweli kweli! CCM wakianza kufukuza malaya, mbona serikali na bunge litabaki tupu!
 
Hili wengine tuliandika tokea mwaka jana kwamba Mwakipesile hana mpango tena wa kugombea ubunge wa Kyela.

Du nimekubali kuwa una data mzee. hebu tupe wengine basi ambao hawangombei ili tupime basi kama form zinachukulika
 
Du nimekubali kuwa una data mzee. hebu tupe wengine basi ambao hawangombei ili tupime basi kama form zinachukulika

Umeanza tena matatizo yako? Angalia sana, ukifuata fuata watu utaishia kuumbuka maana data zote tunazo!
 
Msishangae atachaguliwa kuwa balozi wa Tanzania USA anytime from now.
 
Msishangae atachaguliwa kuwa balozi wa Tanzania USA anytime from now.

Not a chance! Naweza kwenda mbali zaidi na kusema jamaa atatemwa kuwa mkuu wa mkoa kwenye mabadiliko yatakayofanywa na JK baada ya uchaguzi mwakani.
 
Amesahau kusema pia ataachana na kundi baya sana la mtandao....maana hilo ndilo analoliabudu kwa sasa angetubu na kuachana nao kama kweli alikuwa anatubu na kusema na Mungu mbele ya maaskofu.......aache unafiki wake.....
 
Not a chance! Naweza kwenda mbali zaidi na kusema jamaa atatemwa kuwa mkuu wa mkoa kwenye mabadiliko yatakayofanywa na JK baada ya uchaguzi mwakani.

Tanzania ina wapiga ramli wengi kweli kweli!
 
Wanasiasa hawaaminiki! Hawakawii kusema niliombwana wazee nigombee tena!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…