Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi amesema Taifa linahitaji Bunge lenye wabunge makini, mahiri na wenye uelewa wa kina wa masuala ya kikatiba, ili kuhakikisha uwajibikaji na ufanisi katika mfumo wa utawala wa nchi unarejea kwenye misingi iliyowekwa na Katiba. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam baada ya kupokea ugeni wa Wakili Msomi Sweetbert Nkuba ofisini kwake, Mwabukusi amesema taifa linahitaji viongozi wa kizazi kipya waliobobea katika taaluma na wenye uthubutu wa kweli.
“Bunge linahitaji vijana makini, wenye nguvu na uelewa wa hali ya juu ili kulisaidia katika utekelezaji wa majukumu ya kikatiba. Ni muhimu kwa nchi kuwa na viongozi wanaojua misingi ya Katiba na wanaoweza kuisimamia,” amesema Mwabukusi Wakili Nkuba alimtembelea Rais huyo wa TLS kumjulisha rasmi kuhusu nia yake ya kuomba ridhaa ya wananchi wa Jimbo la Kahama Mjini kumchagua kuwa Mbunge wao katika Uchaguzi Mkuu ujao. Akizungumzia uamuzi huo, Mwabukusi amesema: “Nkuba alikuwa mpinzani wangu katika kinyang’anyiro cha urais wa TLS mwaka 2024.
Kama ningetakiwa kutoa maoni, ningewaambia wananchi wa Kahama kuwa hawana sababu yoyote ya kumkataa mtu huyu. Ana sifa zote za kuwa mwakilishi bora.” Aidha, ameongeza kuwa anaamini katika uwezo, uthubutu na ubunifu wa Wakili Nkuba, ambaye wamefahamiana kwa zaidi ya miaka 15