Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Wote wamesimama kwenye mvua, moja atishia kumlowesha mwenziye !
Wote wanaogelea kwenye tope, moja adai aliyechafuka labda mwenziye !
Wote wamtumikia bwana moja, hakuna wa kumsaliti mwenziye !
Kwani
Wote huunganisha nguvu, anapotokea mpinzani.
Hili la Mwakyembe hakika ni changa la macho, jamani angalieni
Hakuweza kuyasema bungeni ama NEC, sasa ataka kuyaanika uchochoroni !
Lakini
Si wadanganyika wapo na watachangamkia tenda ?
Wanachosahau ni kuwa toka lini mafahali wawili wakakaa zizi moja ?
Linapotokea hivyo ama moja kishashikishwa adabu, vipi awike tena ?
Hata hivyo
Kila kivumacho kina mwisho, historia haina tabia ya uwongo.
Kama limetokea limetokea, kudai vinginevyo ni kujaribu kupindisha ukweli
Waliapa kuwa watalindana, sasa huu usanii ni wa nini ?
Ni uwongo
Wananchi wengine tumeamka zamani na hivi sasa tuko macho.
Ili ziweze kupigwa kavu kavu ni bidi watokee kona tofauti ulingoni.
Moja akivaa mkanda mwekundu na mwenziye akivaa mkanda wa bluu.
Huo ndio utaitwa mpambano.