Mwakyembe aitumia TAKUKURU kumng'oa Jamal Malinzi TFF?

Malinzi jeuri sana apelekwe mahakamani haraka sana
 
Kwa Tanzania ya viwanda,tunahitaji kutengeneza ajira kwenye soccer pia. Hivyo watu wenye kusimamia haki ndio wanaopaswa kuwepo TFF. Hatutaki viongozi wala rushwa hivyo TAKUKURU bana kabisa mpaka uchaguzi uishe.
 
tuhuma za kina malinzi ziko wazi muda mrefu kama ungesoma nipashe waliripoti ripoti ya ukaguzi wa fedha sasa hapo Mwakyembe anaingiaje
 
Mi mwanachadema lakini simpendi huyo Malinzi kama hao kina Mwakalebela au Ali Mayayi watakuwa na mabadiliko wachaguliwe tu.

Acheni kumficha Malinzi kichaka cha ukawa wakati kaboronga kuendesha soka letu,Kaingia uongozi kaikuta Tz nafasi za 90s kiwango cha soka fifa sasa tupo 150s hukooo. Malinzi kwenda mwana kwenda
 
Acheni vyombo husika vifanye kazi yake! Hivi kwa akili ya kawaida tu ni ajabu sana hawa watu kuhojiwa? TFF ni maficho mazuri ya "wapigaji"! Halafu wakiguswa kidogo tu utawasikia wakidai; "FIFA haitaki serikali kuingilia Mpira!" Utadhani "upigaji" Nao ndo mpira!
 
kwahiyo mwakyembe siku hizi yupo Takukuru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…