Mwakyembe aitumia TAKUKURU kumng'oa Jamal Malinzi TFF?

Mwakyembe aitumia TAKUKURU kumng'oa Jamal Malinzi TFF?

JAMALI AMEFANYA HAYA
UFISADI WA KUTISHA TFF
Ripoti ya ukaguzi wa fedha za udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania kwa Taifa Stars iliyotolewa Oktoba 2, 2014, inaelezwa kuwa, mbali na mambo mengine, TBL iliamua kufanya ukaguzi huo ili kujiridhisha kama shirikisho linazingatia makubaliano yaliyomo kwenye mkataba.

Inaelezwa katika ripoti hiyo ambayo uongozi wa juu wa TBL uliithibitishia Nipashe jana kwamba ilifanywa na Mkaguzi Mkuu wake wa ndani, Richard Magongo, kuwa kati ya Novemba 13, 2013 (siku 11 tangu uongozi wa sasa wa TFF uingie madarakani) na Februari 15, 2014, Dola za Marekani 315,577 (Sh. milioni 688.368) zilitumika bila ya nyaraka za kuthibitisha matumizi yake kinyume cha makubaliano ya mkataba wa pande hizo mbili.

Kati ya Novemba 11, 2013 na Machi 11, 2014, Dola za Marekani 381,248 (Sh. milioni 831.616) pia zilichotwa kwenye akaunti hiyo na kutumika kwa shughuli ambazo hazijaanishwa katika mkataba wa TBL na TFF, ripoti inabainisha.

Mchanganuo wa ripoti hiyo unaonesha kuwa, miongoni mwa waliotajwa kwenye ripoti hiyo kutumia fedha hiyo ni pamoja na rais wa TFF, Jamal Malinzi, ambaye Desemba 24, 2013 alilipwa Dola za Marekani 159 kupitia vocha yenye namba 1075 zikiwa ni gharama za malazi hotelini (Hotel accommodation).

Ripoti inaonesha kuwa, siku hiyo hiyo (Desemba 24, 2013), Malinzi alilipwa na TFF Dola 10,000 kupitia vocha namba 1077 (Repayment to Jamal Malinzi/Marejesho ya fedha za Jamal Malinzi), kisha Februari 6, 2014 akalipwa Dola 15,934 (Loan Repayment to Jamal Malinzi/Marejesho ya mkopo kutoka kwa Jamal Malinzi) na baadaye kulipwa Dola 69,471 kupitia vocha namba 1098 na Dola 63,735 kupitia vocha namba 1401.

Wengine waliopewa fedha hiyo ya udhamini wa TBL kwa Taifa Stars ni aliyekuwa msaidizi wa Malinzi, Juma Matandika, Ali Ruvu na mwingine aliyetajwa kwa jina la S. Madadi ambao kwa pamoja walilipwa Dola 1,084 kupitia vocha namba 828 Februari 6, 2014.

Ripoti pia inabainisha malipo ya Dola 3,500 Januari 16, 2014 kwa ajili ya ziara ya Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF jijini Nairobi.

Pia zimo Dola 4,630 zilizochotwa Desemba 24, 2013 kugharamia mtihani wa utimamu wa mwili kwa waamuzi (Cooper test for referees), Dola 4,120 zilizotolewa siku hiyo hiyo kwa ajili ya Ally Mayay na Ayubu Nyenzi kufanya ziara Uganda na Dola 1,638 ambazo zilitolewa siku hiyo hiyo zikiwa fidia ya malipo ya deni la TFF kulipia ziara ya uongozi wa shirikisho mkoani Mwanza.

Dola 4,023 zilitolewa Desemba 24, 2013 kwa ajili ya posho ya sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya kwa wafanyakazi wa TFF na Dola 30,000 zilitumika kwa semina elekezi kwa makocha iliyofanyika Lushoto (coach retreat at Lushoto), ripoti inasema.

Inaongeza: "Dola 2,829 zilitumika kutoa rambirambi na misaada, Dola 3,298 zikakopeshwa kwa Chama cha Soka Mbeya huku Dola 989 zikitolewa kwa Chama cha Soka Mkoa wa Mtwara zikiwa ni msaada."

Katika ripoti hiyo, inaelezwa kuwa, Dola 90,000 zilitumika kulipia fidia ya kuvunjwa kwa mkataba wa aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen na Dola 34,177 zikatumika kununua magari mawili aina ya Toyota Hiace.

Ripoti inaeleza kuwa, kulikuwa na mawasiliano rasmi kati ya maofisa wa TFF na TBL kabla ya kufanya malipo kwa Poulsen na ununuzi wa magari hayo.

UKABILA ULIOKIDHIRI
Baada ya tu ya ndugu yetu huyu kuingia madarakani, vipaumbele vikabadilika ghafla na ku-format management ya TFF na ikajaza wahaya kibao. Katibu mpya akawa Mhaya, Mkurugenzi wa sheria na utawala ni Mhaya, Mshauri wa masuala ya kiufundi ni Mhaya, Mwenyekiti mpya wa kamati ya maadili ni Mhaya, Mwenyekiti mpya wa kamati ya Uchaguzi ni Mhaya

FITNA KWA WANAMICHEZO
Kuna taarifa zilisema Mtangazaji nguli wa michezo hapa nchini na aliyepata kuwa msemaji wa Club ya Simba Clifford Mario Ndimbo alifukuzwa Radio Times Fm ambapo ndio alikuwa akiendesha kipindi chake cha michezo kiitwacho "Wizara ya Michezo"

Taarifa za ndani zinasema kuwa Mkurugenzi wa radio hiyo alifikia hatua hiyo kwa kile kinachosemekana kuwa ni kulinda maslahi ya viongozi wa michezo hasa mpira wa miguu waliokuwa wakianikwa hadharani "uozo" wao kupitia segment ya "Dokodoko" ambayo ilijikita katika kueleza ukweli wa masuala mbalimbali ya mpira wa Tanzania.

Wafuatiliaji wa kipindi cha Wizara ya michezo walisema wana muda mrefu sana hawajasikia segment ya "Dokodoko" ambayo ndio iliibua skendo kubwa ya Rushwa TFF na mambo mengine, na kupelekea kesi kwenda mahakamani na TFF wakashinda

Wanamichezo wengine waliokumbwa na fitna za Malinzi ni Haji Manara msemaji wa Simba, wakala Dr.Ndumbaro

SOKA LA VIJANA/WATOTO
Wakati anaingia madarakani alikuja na mipango kibao kwenye soka la watoto. mpango wa kuunda kikosi cha Taifa cha watoto umri chini ya miaka 13 kitakachokua pamoja kuelekea fainali za Afrika umri chini ya miaka 17 mwaka 2019. Mpango wa kuunda kikosi cha taifa umri chini ya miaka 14 mwaka huu,kikosi kitakachokaa pamoja LordBaden school kujiandaa na Africa qualifiers under 17 mwaka 2016. Mpango wa Taifa wa kuhakikisha kila mkoa unakuwa na youth football centre kwa ajili ya age group 8-17

Aje hapa aseme haya yote yaliishia wapi?

SOKA LA WANAWAKE
Soka la kinamama ilikuwa kipaumbele chake wakati wa kampeni. Alikuja na mpango wa uanzishwaji wa kombe la Taifa la wanawake Desemba mwaka 2014. Mpaka leo hii hakuna kitu kama hicho.

KUDHALILISHWA KWA SERENGETI BOYS
Kutokana na Malinzi kutafuta mapato ya TFF ilifikia kipindi TRA wakawa wanaidai TFF kiasi kikubwa cha kodi. Mamlaka ya Mapato Tanzania ilifikia hatua ya kuwashusha Njiani Timu ya vijana chini ya miaka 17 TRA wakilitaka Basi lililokua limewabeba vijana hao ili kulipiga mnada waweze kulipa deni la kodi.

Jamali Malinzi ni mwanachama wa JF. Baada ya kuona anafanya madudu katika soka aliikimbia JF na kuibukia magazetini huku akikashifu kwamba JF tunamuonea na kumzushia. Baada ya kubanwa sana na wanaJF akaomba uzi wake uliokuwa unawekwa gundi pale juu, uondolewe kuficha aibu. Tunamuomba aje humu kujibu hoja za wadau, ikiwa ni pamoja na sisi kumpa facts kwa nini tutampiga chini uchaguzi ujao.

Fedha za FIFA ambazo ziko kwenye dola sasa zimebatizwa kuwa za TBL ambayo imeshindwa hata kuwalipa magawiwo ya kila mwaka wanahisa wake.

Pili, tangia lini TBL wakalipa kwa dola, tafakari chukua hatua
 
Mwakyembe naomba unyooshe na Magazeti ya michezo ambayo pia yanaharibu Mpira wa TZ kwa kuandika udaku. Mfano utakuta gazeti linamsifia mchezaji Fulani atakae sajiliwa na timu, Fulani utazani mchezaji Huyo anakiwango cha Madrid kumbe Hovyo kabisa.
 
"...huu ndio mwisho wa kupata pesa kiujanja ujanja na kupiga dili..... "
Mkuu wa nchi
 
Fedha za FIFA ambazo ziko kwenye dola sasa zimebatizwa kuwa za TBL ambayo imeshindwa hata kuwalipa magawiwo ya kila mwaka wanahisa wake.

Pili, tangia lini TBL wakalipa kwa dola, tafakari chukua hatua
Yeye kajing'oa tff, sio mwingine. Tatizo ujanja mwingi matokeo haba.
 
Tukigingiwa ndio safivtutakuwa tunajenga timu. Kwani si hata wadau wengi wa michezo walipropose tusishiriki michuano ya kimatsifa kwa muda ili tujenge timu.
 
Back
Top Bottom