- Bila mupangilio au mtiririko maalum.
- Nikifuatilia mlolongo wa Matukio, kutoka vyombo vya habari siku tatu kabla ya Ujio wa Mgeni wa Marekani nimeweza kugandua haya na hii ndio nadharia yangu kuhusu ukweli fulani fulani wa alichosema Fortilo kwamba 'mambo ni magumu' ambayo mie naona sio kawaida.
- Mh. Tax aongea na Waandishi wa Habari kuhusu ujio wa Kamara Harris
- Makyembe alizungumzia mashoga na kutaja Shirika la ki-Marekani kama muhusika fulani
- Raisi aliunda kamati kutathmini utendaji kazi Wizara ya Mambo ya Nje
- Mgeni Kutoka Marekani Alihutubia kwa dakika takriba 7 nane bila kuulizwa maswali.
Kutokana na itafaki za kidiplomasia ambazo huwa ni nguzo za msingi zinazotumiwa Wakati wa Ziara za wakuu wa nchi kuzingatiwa na kukubalika baina ya nchi husika basi kunakuwa na 'go ahead' ya aina na wanawasiliana na kupiga saini... go ahead hiyo... na ..hapa ndipo Mh. Tax anaingia.
Tax na Balozi wa Marekani kwa pamoja wanatoa taarifa n.k Yaani walishakubaliana mambo kibao...mfano Nani atakaa wapi kwenye iftar, yaani mpangilio wa viti na waheshimiwa, au kwenye msululu wa magari kutoka airport yatapita wapi, Je, nani ataulizwa maswali au lah na waandiahi wa habari wakati wa hotuba zao ikulu, au mbowe atapiga picha na nani n.k .n.k na mifano mingi tu, hata aina ya nguo watazo vaa!
Sasa narukia kwenda kwa SSH kutangaza kamati, Je hakufurahishwa na mpangilio mzima wa jinsi watavyokuwa wamekaa au kusimama wakati Wakuu hao wakipiga sahihi kwenye ile MOU? Baina ya Nchi zetu?
hiyo peke yake(kusimama wakati mgeni amekaa) na kinyume chake ni tete na tumeona mpaka uzi umebandikwa humu kwa jinsi gani taswira ile ilivyoonekana, yaani SSh amesimama wakati Kamara akipiga mkono kabrasha la makubaliano yao? Sio kawaida na imeonyesha mambo ni magumu..
Sasa turudi kidogo mpaka pale Mh. Tax akitangaza/ akitoa taarifa kwa umma na waandishi wa habari hiyo peke yake sio kawaida.... haijalishi hapa hayo, ila ina maana wakati akifanya hivyo, idara za itifaki walishakubaliana itakavokuwa na inawezekana SSH aliipata hiyo ratiba/ itenary late tena baada ya kukubalika pande zote bila ya yeye kuwa na ka input kake, kama vile, alitaka avae bangili nyingi apake hina au avae suti au baibui, yani kile angependa kuonekana nacho kama tamaduni zinavyomtaka, sasa wanafanyaje na kitu ndio kishatoka.. yaani wawakilishi wa itifaki wameshakubaliana. Kitokee au Kisitokee.
Watafanyeje kubadilisha kitu mule? manake kusimama kule inawezekana kabisa hakikumfurahisha SSH au wasaidizi waliobobea na mambo ya Itifaki na kumshauri hiyo inaweweza kuonekana kana kwamba unasujuda? na vilevile labda pia, kukawa na Upande wa mgeni nao ulikuwa na kaspeech kenye kamstari useme...."tungependa kuona haki zote zinazingatiwa ikiwemo zile za LGBTQ"
Anaambiwa 'Aisee hiyo, inaleta 'Taswira hasi' na inaweza kuleta aibu na ukaonekana Mh. SSh uko weak, yani kwanza anasimama halafu anakuwa lectured.....sasa hapo ndio tunapojua hatujui.... Wanajadiliana(itifaki ikulu/wizarani) na kuanza kutafuta jinsi ya kuporomoa hata moja za ' muonekano wa Taswira hasi ' na aibu yaani kule kusimama na lecture juu kuhusu LGTBQ (kale kamstari kale juu)'
'ahhhh' naona alisema, 'mkalitizame hilo' mie naona kulikuwa hakuna muda wa kufanya diplomatic manuevering bila ya kuwepo na jambo la msingi, yaani kama emergency fulani yaani criteria waliokubaliana kifanyike pale kutakapo tokea dharura fulani fulani ivi ili na wao wageni wakiona hivyo nao wakubali- kukubali na kuweza badili gia angani(literaly at this point) manake Kamara alikuwa kule Ghana... Sasa ndio Makyembe anakuja sasa, anapata maagizo kutoka juu, anatifua tifua, na sasa linakuwa suala fulani yaani sasa ni issue la dharura na bibie Lilian anashangashangaa....
....Mambo ya dharura ambayo yanaweza kubalika na pande zote na inaweza badilisha mambo mengine pamoja na kale ka mstari-wageni wanaambiwa 'Jamani ehhh huku kimenuka', mnamjua yulee? 'eeeh' yule waziri wetu wazamani ?, 'ehhh' 'aha kaharibu mambo Wananchi wameanza tafrani, tunaomba angalau muondoe kale ka mstari ili mambo yaende vizuri'....nafikiri wakakubali na katika majadiliano wakaona waondoe hayo ya LGBTQ
...hapo sasa kazi kwao wageni watacheza gemu gani ili nao waandishi wao wasione gemu hapa manake huwa wanapata hata kafununu, ma dondoo za hotuba n.k mapema wakiwa angani....
....mie naona yule wa itifaki wa wageni akaona njia na mbinu rahisi zaidi ya kufanya hivyo ni kusitisha maswali pale Ikulu, Dar, manake yale majamaaa ya habari kule yangeweza kutaka kujua Msimamo wa Raisi kuhusu Makyembe kuweka giza kwenye masuala waliokubaliana awali kuwa Kamara atazungumzia hayo Jukwaani ikulu....sasa mbona huyu Waziri anafanya hivi? Aisee sio kawaida ukizingatia ni mambo magumu....
.... kwani wanajua Kamara atazungumzia mambo ya Demokrasia sambamba na Haki, kwenye hotuba yake/jumbe zake na ....
......hapo ndipo hatujui tunajua ni nini nani wanaofanya mavituz na kuonekana jinsi yanavyoonekana na ndipo tunafikia zile dakika chache sana za Kamara kuzungumza pale, manake kale kamstari kanawezekana kutumia hata dakika 10 hivi kuelewesha, aanze na historia sijui nini wapi nani, kwa lugha nyingine ni ile Lecture ambayo ilipigwa chini kwa mbinu waliyotumia wabobezi wa Diplomasia na washauri manake ile tifutifua ya Makyembe ilikuwa sio kawaida, taarifa kwa vyombo vya habari, sio kawaida kwa Waziri wa mambo ya nje kufanya....kutoa tarifa sio kawaida, kwani kawaida ni...idara za itifaki, aidha Ikulu au Wizarani ndizo hufanya hivyo, sio kawaida kwa Raisi kutangaza tathmini ya Wizara kama ya Mambo ya nje, tena siku au masaa machache kabla ya Ujio wa mgeni Mkubwa kama Kamara. Mambo mengi hayakuwa ya kawaida na ni hivyo basi, hata yale anayotaka Bibie lilian kuonekana sio kawaida na mwishoe, labda kuzimwa kidizaini kama fortilo anavyodai?
Nisiwachoshe