BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Imeandikwa na Basil Msongo;
Tarehe: 27th July 2009
Tarehe: 27th July 2009
Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe ameitaka Serikali iufunge mara moja mgodi wa dhahabu wa North Mara ili sumu inayodaiwa kutoka hapo isiendelee kuwadhuru wananchi.
Mbunge huyo pia ametaka mgodi wa dhahabu wa Geita ufungwe kwa sababu, kwa muda mrefu umekuwa ukitoa kemikali za sumu zinazowadhuru wananchi wa kijiji cha Nyakabale.
Kwa nini tuogope wawekezaji kama wakwe? amehoji Mwakyembe na pia kuuuliza kwa nini vifungu vya mikataba havitumiki kuwabana wawekezaji.
Kwa muda mrefu kumekuwa na madai kuwa mgodi wa North Mara uliopo wilayani Tarime mkoani Mara umekuwa ikimwaga maji yenye sumu katika mto Tigithe.
Kwa mujibu wa madai hayo, wananchi 21 kati ya waliyoyatumia maji hayo wamefariki dunia, wengine wamekumbwa na matatizo ya kiafya, na pia mifugo 200 imepoteza maisha.
Kampuni inayoendesha mgodi huo, Barrick Tanzania, imekanusha taarifa hizo kwa madai kuwa polisi kwa kushirikiana na mamlaka za Wilaya ya Tarime zimefanya uchunguzi na kubaini kuwa hakuna uthibitisho wa kuwapo kwa madhara hayo.
Dk Mwakyembe amesema, anafahamu kwamba, kampuni inayomiliki mgodi wa North Mara, Barrick, ni kubwa zaidi kwa uzalishaji wa dhahabu duniani na ina nguvu kubwa lakini hawezi kukaa kimya wakati wananchi wanaathirika na lazima hatua zichukuliwe.
Hii nchi ni yetu, tutaongea kwa ujasiri tu Dk Mwakyembe ameyasema hayo bungeni mjini Dodoma wakati anachangia bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2009/2010.
Kwa mujibu wa Mbunge kampuni ya Barrick ina rekodi mbaya ya kuharibu mazingira.
Kampuni ya Barrick Tanzania inaendesha migodi minne nchini, Bulyanhulu, North Mara, Tulawaka, na Buzwagi.
Pamoja na mapenzi yetu makubwa kwa wawekezaji lazima hatua zichukuliwe amesema Dk Mwakyembe na kupendekeza kuwa wananchi waishitaki kampuni ya Barrick.
Mbunge huyo amesema, wabunge wa maeneo ulipo mgodi huo washirikiane na wananchi, wanaharakati na wanasheria kufungua kesi mahakamani kuishitaki kampuni ya Barrick kwa kuwa maneno ya majukwaani hayawezi kuwasaidia waathirika.
Kwa mujibu wa Mwakyembe, kuna taarifa kwamba, mgodi wa Tulawaka unafungwa kwa kuwa dhahabu imekwisha, hivyo amehoji kama Serikali imepewa fedha za kuhuisha mazingira, zipo wapi na kiasi gani.
Dk Mwakyembe amesema, watanzania wamechoka kuachiwa mashimo yeye sumu ya zebaki.
Mbunge wa Ukerewe, Balozi Getrude Mongella amesema, kama hatua zisipochukuliwa sumu zinazotoka kwenye mchakato wa kupata madini zitawamaliza watanzania.
Balozi Mongella ametaka migodi inayotoa sumu ifungwe mara moja kwa kuwa zebaki inabaki mwilini na kukiharibu kizazi cha sasa na vijavyo.
Kwa kweli ni jambo baya, baya, kama hatuchukui hatua mambo ya sumu it is blood money hili la sumu it is immediate, tunafunga tujue moja amesema Balozi Mongella.
Dk Mwakyembe amesema, kama ubinafsishaji usipofanywa kwa makini utaligharimu taifa na ametoa mfano kuwa, madini yanawanufaisha wageni kuliko watanzania.
Mbunge huyo amesema, ni bora madini yaachwe ardhini hadi Tanzania itakapokuwa tayari kuyachimba badala ya hali ilivyo sasa.
Mheshimiwa, kama uadilifu wetu una mgogoro yaachwe chini ya ardhi watachimba wengine amesema Mbunge huyo na kusema kuna uroho katika kuzitumia rasilimali nchini.
Uroho umetutawala, tumeanza kutoana macho hata kabla utafiti haujafanyika amesema na kubanisha kwamba, Baba wa Taifa, Julius Nyerere na Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Aman Karume hawakutaka kuchimba hata mafuta.
Wakati huo huo, Dk Mwakyembe amesema, kama Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA) imeshindwa kazi iwaachie wengine.
Amesema, kuna mafisadi katika sekta ya mafuta, Ewura inawafahamu kwa majina wakiwamo wanaochanganya mafuta ya taa na dizeli lakini mamlaka hiyo haichukui hatua.
Dk Mwakyembe ametoa miezi mitatu Ewura ijirekebishe, isipofanya hivyo atawasilisha hoja binafsi bungeni. Kama ni mshiko unaofanya wafumbie macho wahakikishe hili tatizo linakwisha Tanzania amesema