Mwakyembe alitumika kumuumiza Lowassa kwenye kashfa ya Richmond

Huihui2

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
7,021
Reaction score
11,475
Wakati wa mjadala mkali wa kashfa ya Richmond bungeni, huku tume iliyochunguza kashfa hiyo ikibanwa kuwa haikutoa nafasi kwa watuhumiwa hasa Lowassa kujitetea, aliibuka mwenyekiti wa tume ile Mwakyembe na kusema kuwa kama watu hawaridhiki waombe kanuni zitenguliwe ili aweze kuwasilisha upya ripoti yake ili aweze kusema hata siri waliyoificha ili kuikoa serikali isiporomoke yote.

Kwa maneno hayo mimi nilliewa kuwa kumbe tume ile iliwasilisha ukweli nusu na hivyo kumtoa kafara Lowassa na mawaziri wawili ili kumwokoa rais ambaye kwa maneno ya Mwakyembe kama wangeyasema yote, ingesababisha serikali yote kuporomoka.

Kwa ufupi nilivyoelewa ni kuwa taarifa ile ilikuwa inamgusa Rais moja kwa moja na kwa maana hiyo alipaswa kuondolewa madarakani lakini akaokolewa na tume kwa kuficha siri.

Hivyo kilichofanyika ilikuwa ni kukivunja kichwa (Lowassa) kwa kosa lililofanywa na ulimi (rais). Na ndio maana katika kikao kimojawapo cha chama Lowassa alimuhoji mwenyekiti kuwa ni jambo gani ambalo yeye aililifanya ambalo yeye hakujua au kumtuma?

Ni wazi Harrison Mwakyembe alitumika na Spika Sitta kumuumiza Lowassa kwa vile Sitta na Lowassa wote walikuwa wanautaka u PM kama build up ya U-Rais wa 2015


Soma
 
Naamini pia alitumika hasa nikikumbuka;

- Alivyotoa ile ripoti yake bila kumhoji Lowassa. Mwanasheria gani unaye hukumu bila ya kutoa haki ya kusikilizwa yule unayemhukumu.

- Alivyosema wakati wa kusoma ile ripoti kuna mambo mengine anayaacha, kwani kama angeyaweka wazi nchi ingeyumba.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Mwakyembe mi moja wa wasomi wa hovyo kabisa kuwahi kutokea katika taifa hili.

Naomba Mungu roho ya Lowasa iranderande pale msoga pamoja na mizimu ya kimasai mpaka yule mzee apakimbie kwake.
 
Acheni kupotosha Mwakyembe alifanya Kazi yake vzr mambo Mengine tuchukulie ni mambo ya kibidanamu Lowassa hakuwa malaika mapungufu yake hatuwezi kuyaondoa saizi yy anajua na Mungu wake
Alifanyaje kazi nzuri wakati hakukamilisha ripoti yote? Isitoshe aliweza kutembea dunia nzima kutafuta ushahidi lakini akapuuza kwenda kumhoji Lowassa aliyekuwa hapahapa Dodoma?

Mwakyembe ni RUBBISH πŸ—‘ πŸ—‘
 
Alivunja principle ya hear the other side also kwa kilatini inaitwa "Audi alteram partem".

Halafu anadai ana degree 4 na PhD ya sheria. Upumbavu mtupu
 
Lowassa alikuwa "mbuzi wa kafara tu". Kila kitu kilikuwa kimesukwa na Mkwere na Sitta kumtoasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…