MBUNGE wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM),
1. alisema pia kwamba, kuyumba kwa serikali iliyopo madarakani kunatokana na viongozi kutokubali kuwajibika, ikiwa ni pamoja na kushindwa kuchukua maamuzi magumu hali inayotokana an mmomonyoko wa maadili.
2. "Mheshimiwa Mwenyekiti, viongozi wetu hawana ‘political responsibility', wamejiuzulu lakini hadi leo wanalia wamekosa ‘dili'.
3. Wameanzisha magazeti kwa ajili ya kumtukana Spika wa Bunge na wajumbe wa kamati teule. Hawa watu wanazo hela hawa, sasa mimi nawashauri watumie fedha zao kununua airtime tujadili hoja," alisema.
4. Aidha, mbunge huyo, alimtaka Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na timu yake kujiuzulu ili kuonyesha uwajibikaji kutokana na kulidanganya taifa kuhusu mkataba wa Richmond.
5. Alisema, taasisi hiyo imelitia aibu taifa kwa kufunika uoza uliokuwepo kwenye mkataba wa kampuni hewa ya kufua umeme ya Richmond.
- Warioba:-
6. Awali, akizungumza katika kongamano hilo jana, Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, alisema wakati wa viongozi kuchukua maamuzi magumu katika kashfa mbalimbali zikiwamo zile za Richmond, Kagoda na Deep Green umefika.
- Dr. Salim:-
Kwa upande wake, Dk. Salim ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere iliyoandaa kongamano hilo, alisema rushwa katika nchi hii haitamalizika kwa msimamo wa chama ama serikali pekee, bali ni kwa Watanzania wote kuikataa kwa vitendo.
Hata hivyo, alisema suala hilo ni gumu iwapo wananchi wataendelea kubaki kwenye umaskini walionao na akaitaka TAKUKURU kuitikia wito uliotolewa kwao na Rais Jakaya Kikwete wa kuitaka ifanye kazi kwa haki.
Dk. Salim alibainisha kwamba hivi sasa taifa limeelemewa na matatizo mengi, yakiwamo chuki, mauaji ya kinyama, ubaguzi, siasa chafu, udini na vitendo vya watu fulani kujiona kuwa ni wazalendo kuliko wengine.
"Baada ya miaka 10 ya kuondokewa na Baba wa Taifa letu, kuna mambo mengi yametokea na yanayoendelea kutokea katika nchi yetu. Mambo ambayo yanatutaka sisi kama wadau wa taifa hili kuwa na uthubutu na ujasiri wa kuanzisha mchakato wa kujitazama, kujichunguza na kukubaliana jinsi gani tunaweza kujinasua katika matatizo ambayo kama yakipuuzwa yanaweza kugeuka majanga na kuliweka taifa letu mahali pabaya," alisema.
- Sumaye:-
Naye Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, alisema Watanzania wamekiuka ahadi yao kwa Mwalimu Nyerere ya kuenzi kwa vitendo mambo yote aliyoyasimamia hali inayosababisha taifa kufika lilipo sasa.
Alisema mfumo wa utawala na kuporomoka kwa maadili miongoni mwa viongozi, unakaribisha wakoloni wapya kuingia Tanzania, hasa kutokana na kushindwa kuzuia rushwa. "Kuna hatari ya Tanzania kuja kutawaliwa tena iwapo hatutaondokana na rushwa kwa matendo…"
Source: Tanzania Daima Dec 02, 2009.
- Haya ndiyo tunayoyasema hapa kila siku, yaani unafiki wa viongozi wetu tizama maneno kuanzia ya Mwakyembe, mpaka mwisho yaani Sumaye yako very clear nani mnafiki na nani yuko serious, sasa tukisema wengine hawafai kunatokea vilio vikubwa sana humu JF kwamba tuko bias,
- Mimi ni mwananchi wa kawaida nimehudhuria huu mdahalo, ninawasikiliza hawa viongozi wote mwanzo mpaka mwisho hivi kweli ninatakiwa kuwa genius kuamua nani wa kumchagua hapo juu kwa ajili ya kusimamia masilahi ya taifa langu?
- I mean hands down Mwakyembe is the man! Calling a spade exactly what it is a spade, that is it! Do not give me no nonsense za chama, oooh Mwalimu, oooh serikali, oooh wananchi all B/S! Bravo Dr. Mwakyembe tunatka viongozi wanaoweza kusimama na kuhesabiwa and let the chips fall where they may, Full Stop!
Respect.
FMEs!
haya ni mawazo finyu sana, test tube way of thinking, ina maana kwa kuwa walikuwa na mtu wao hawaruhusiwi kukemea pale nchi inapoyumba? nchi inaangamia na watu kama wewe wako kwenye lindi la usingizi mzito wa chagua la Mungu yaani kikwete
Mdahalo tena? Dr watakakutupeleka wapi?
Aidha, mbunge huyo, alimtaka Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na timu yake kujiuzulu ili kuonyesha uwajibikaji kutokana na kulidanganya taifa kuhusu mkataba wa Richmond.
Alisema, taasisi hiyo imelitia aibu taifa kwa kufunika uoza uliokuwepo kwenye mkataba wa kampuni hewa ya kufua umeme ya Richmond.
Source: Tanzania Daima Dec 02, 2009.
Mdahalo wa "Alibaba and 40 thieves",
CCM wote wevi tu.
- Hakuna cha kuppunguza wala kuongeza, hizi ndio tunaita facts!
Respect.
FMEs!
- I mean hands down Mwakyembe is the man! Calling a spade exactly what it is a spade, that is it! Do not give me no nonsense za chama, oooh Mwalimu, oooh serikali, oooh wananchi all B/S! Bravo Dr. Mwakyembe tunatka viongozi wanaoweza kusimama na kuhesabiwa and let the chips fall where they may, Full Stop!
Respect. FMEs!
.- Hakuna cha kuppunguza wala kuongeza, hizi ndio tunaita facts!
Respect.
FMEs!
Ni kweli hana jipya kwa vile ya zamani aliyosema hayajafanyiwa kazi. Kama huyo Rostam wako yuko sawa na anaamini anayowatendea Watz ni sawa basi akavinjari mitaa ya kariakoo aone atakavyo shangiliwa kwa wema wake..
Hakuna cha fact zaidi ya upuuzi.Waende kariakoo kufanya nini?Huyu ni Dr wa kienyeji?Huyu bwana harudi tena 2010.Hana jipya.
Ni kweli hana jipya kwa vile ya zamani aliyosema hayajafanyiwa kazi. Kama huyo Rostam wako yuko sawa na anaamini anayowatendea Watz ni sawa basi akavinjari mitaa ya kariakoo aone atakavyo shangiliwa kwa wema wake.
Mie nadhangaa kelele za siku nyingi za kina mwakyembe et all.
kama wana ushahidi kuhusiana na Rostam basi waende wakafungue mashtaka mahakamani.
We are tired of listening to this cheap politics while Tanzanians are still living very poor life..
Mwakyembe ni kioja tu