Mwakyembe Ataka Mdahalo na akina Rostam

Mwakyembe Ataka Mdahalo na akina Rostam

Kama lowassa aliona ameonewa kwanini alijiuzulu?
 
Mdahalo wa "Alibaba and 40 thieves",
CCM wote wevi tu.
 
- Mwakyembe:-

MBUNGE wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM),

1. alisema pia kwamba, kuyumba kwa serikali iliyopo madarakani kunatokana na viongozi kutokubali kuwajibika, ikiwa ni pamoja na kushindwa kuchukua maamuzi magumu hali inayotokana an mmomonyoko wa maadili.


2. "Mheshimiwa Mwenyekiti, viongozi wetu hawana ‘political responsibility', wamejiuzulu lakini hadi leo wanalia wamekosa ‘dili'.

3. Wameanzisha magazeti kwa ajili ya kumtukana Spika wa Bunge na wajumbe wa kamati teule. Hawa watu wanazo hela hawa, sasa mimi nawashauri watumie fedha zao kununua airtime tujadili hoja," alisema.


4. Aidha, mbunge huyo, alimtaka Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na timu yake kujiuzulu ili kuonyesha uwajibikaji kutokana na kulidanganya taifa kuhusu mkataba wa Richmond.


5. Alisema, taasisi hiyo imelitia aibu taifa kwa kufunika uoza uliokuwepo kwenye mkataba wa kampuni hewa ya kufua umeme ya Richmond.


- Warioba:-

6. Awali, akizungumza katika kongamano hilo jana, Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, alisema wakati wa viongozi kuchukua maamuzi magumu katika kashfa mbalimbali zikiwamo zile za Richmond, Kagoda na Deep Green umefika.


- Dr. Salim:-

Kwa upande wake, Dk. Salim ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere iliyoandaa kongamano hilo, alisema rushwa katika nchi hii haitamalizika kwa msimamo wa chama ama serikali pekee, bali ni kwa Watanzania wote kuikataa kwa vitendo.

Hata hivyo, alisema suala hilo ni gumu iwapo wananchi wataendelea kubaki kwenye umaskini walionao na akaitaka TAKUKURU kuitikia wito uliotolewa kwao na Rais Jakaya Kikwete wa kuitaka ifanye kazi kwa haki.


Dk. Salim alibainisha kwamba hivi sasa taifa limeelemewa na matatizo mengi, yakiwamo chuki, mauaji ya kinyama, ubaguzi, siasa chafu, udini na vitendo vya watu fulani kujiona kuwa ni wazalendo kuliko wengine.


"Baada ya miaka 10 ya kuondokewa na Baba wa Taifa letu, kuna mambo mengi yametokea na yanayoendelea kutokea katika nchi yetu. Mambo ambayo yanatutaka sisi kama wadau wa taifa hili kuwa na uthubutu na ujasiri wa kuanzisha mchakato wa kujitazama, kujichunguza na kukubaliana jinsi gani tunaweza kujinasua katika matatizo ambayo kama yakipuuzwa yanaweza kugeuka majanga na kuliweka taifa letu mahali pabaya," alisema.



- Sumaye:-


Naye Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, alisema Watanzania wamekiuka ahadi yao kwa Mwalimu Nyerere ya kuenzi kwa vitendo mambo yote aliyoyasimamia hali inayosababisha taifa kufika lilipo sasa.


Alisema mfumo wa utawala na kuporomoka kwa maadili miongoni mwa viongozi, unakaribisha wakoloni wapya kuingia Tanzania, hasa kutokana na kushindwa kuzuia rushwa. "Kuna hatari ya Tanzania kuja kutawaliwa tena iwapo hatutaondokana na rushwa kwa matendo…"



Source:
Tanzania Daima Dec 02, 2009.


- Haya ndiyo tunayoyasema hapa kila siku, yaani unafiki wa viongozi wetu tizama maneno kuanzia ya Mwakyembe, mpaka mwisho yaani Sumaye yako very clear nani mnafiki na nani yuko serious, sasa tukisema wengine hawafai kunatokea vilio vikubwa sana humu JF kwamba tuko bias,

- Mimi ni mwananchi wa kawaida nimehudhuria huu mdahalo, ninawasikiliza hawa viongozi wote mwanzo mpaka mwisho hivi kweli ninatakiwa kuwa genius kuamua nani wa kumchagua hapo juu kwa ajili ya kusimamia masilahi ya taifa langu?

- I mean hands down Mwakyembe is the man! Calling a spade exactly what it is a spade, that is it! Do not give me no nonsense za chama, oooh Mwalimu, oooh serikali, oooh wananchi all B/S! Bravo Dr. Mwakyembe tunatka viongozi wanaoweza kusimama na kuhesabiwa and let the chips fall where they may, Full Stop!

Respect.


FMEs!
 
haya ni mawazo finyu sana, test tube way of thinking, ina maana kwa kuwa walikuwa na mtu wao hawaruhusiwi kukemea pale nchi inapoyumba? nchi inaangamia na watu kama wewe wako kwenye lindi la usingizi mzito wa chagua la Mungu yaani kikwete

in simpler terms ni kuwa Mwakyembe anaelekea kufilisika kisiasa.hana hoja nyngine zaidi ya hiyo ya ufisadi wa Richmond...Mdahalo wa nini ,he makes himslef very low eti wafanye mdahalo halafu wapite kariakoo wananchi wawahukumu...Mawazo ya kipumbavu kabisa haya then anajiita Dr..juna tfauti gani kwa u Dr wako na wale wenye u Dr wa PAcicif University???

Mwakyembe unakoelekea ni kubaya na una kila dalili za kufulia...
 
RADIO KYELA FM imeanza kurushwa tunataka Mdahalo Mwakyembe VS Mwakalinga,topic ni maendeleo ya Kyela na sio richmond,wananchi wa kyela watakuwa na uwezo wa kusikiliza ,Maana KYELA FM inasikika Kyela nzima.
 
Mdahalo tena? Dr watakakutupeleka wapi?

mi nakuambia huyu kapotea njia na sijui kama atarudi 2010 bungeni..i doubt kwa kweli,yaani kashindwa kuongea bungeni na kwenye mikutano yao ya VICOBA na Mengi leo anataka mdahalo...hahaaaa
 

Aidha, mbunge huyo, alimtaka Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na timu yake kujiuzulu ili kuonyesha uwajibikaji kutokana na kulidanganya taifa kuhusu mkataba wa Richmond.


Alisema, taasisi hiyo imelitia aibu taifa kwa kufunika uoza uliokuwepo kwenye mkataba wa kampuni hewa ya kufua umeme ya Richmond.


Source: Tanzania Daima Dec 02, 2009.

- Hakuna cha kuppunguza wala kuongeza, hizi ndio tunaita facts!

Respect.


FMEs!
 
Mdahalo wa "Alibaba and 40 thieves",
CCM wote wevi tu.


Mjumbe wa kamati kuu na waziri wa CCM alisema authoritatively kuwa wao wote ni Mafisadi!! Sasa huyu Mwakimbi asitubabaishe hapa; anatafuta ulaji tu hana lolote!! Sijakosea Mwakyembe/Mwakimbi wote ndio hao hao !!
 
- Hakuna cha kuppunguza wala kuongeza, hizi ndio tunaita facts!

Respect.

FMEs!

FMES,

Karibu Kyela uje umsaidia Dr. Mwakyembe kwenye kampeni yake.

Ila jiandae maana kwa yale ninayoyaona hapa Kyela, mpambano utakuwa mkali sana kwake.

Pia mshauri jamaa yako atumie muda wake kuongelea maendeleo ya Kyela pia, Richmond, Richmond kila siku haitamsaidia.

Wenzake wanafanya mambo ya maana huku kimya kimya na yanaonekana. Itakuwa ngumu sana kwake kuwaambia wawaache hao wengine waendelee kumwamini yeye ambaye huku tunamwita mbunge wa taifa au msanii.
 

- I mean hands down Mwakyembe is the man! Calling a spade exactly what it is a spade, that is it! Do not give me no nonsense za chama, oooh Mwalimu, oooh serikali, oooh wananchi all B/S! Bravo Dr. Mwakyembe tunatka viongozi wanaoweza kusimama na kuhesabiwa and let the chips fall where they may, Full Stop!
Respect.
FMEs!

Thank you Mkuu, nitakucheck baadaye! Kwenye Ukweli tupo pamoja sana Kamanda
 
Mie nadhangaa kelele za siku nyingi za kina mwakyembe et all.

kama wana ushahidi kuhusiana na Rostam basi waende wakafungue mashtaka mahakamani.

We are tired of listening to this cheap politics while Tanzanians are still living very poor life..

Mwakyembe ni kioja tu
 
Midahalo ya nini? Facts si zimekwisha julikana. Nadhani way forward ni serikali kupitia DPP kuona kama kuna charges ambazo zinweza kusimama kisheria mbele ya mahakama.

Unajua, ni rasihi kuwazuga wananchi kwa kuleta longolongo nyingi lakini ukiziweka katika vipimo vya kisheria ukaambulia charges zote kutupwa nje. Mfano bora angalia kesi ya Zombe!!.

Kama mnavyofahamu, Dk. Mwakyembe si makini sana katika kujenga hoja. Jazba na majigambo huwa kwa wingi sana kwake mpaka wakati mwingine anakoroga mambo. Kwa nini sasa alete wazo la kuitishe mdahalo wakati wazo la kulipeleka suala hili mbele ya Majaji alilipinga. Mdahalo hauwezi kuleta action nyinge ya kufuata lakini jopo la Majaji likikuta kuna uhalifu linaweza kufuatiliwa na mashitaka ya DPP.

Tuachane na hizi PR gestures zenye lengo la kutaka kujijengea umaarufu na tutafutae ufumbuzi wa kimaendeleo..
 
Maana halisi ya Mwakyembe ni kuwa, inaonyesha vyombo vya dola vinavyopaswa kuchukua mkondo wa sheria pamoja na keuelewa nini kimetokea viko kimya, basi hakuna haja tena kuunda tume ya majaji au nini ila kwa vile mafisadi wana pesa wanunue Airtime ili katika mdahalo huo hata watu wakawaida wa Kariakoo wataona na kuelewa nini wametendewa na ukweli uko wapi kisha watatoa hukumu yao baada ya Mwakyembe na Rostam kupita pale Kariakoo.
Naungana na Mwakyembe kuwa kama Rostam atakuwa hai basi hatakuwa amebakiza hata nguo ya ndani. Ndio atajua hukumu ya wananchi wenye hasira kali. Hatatofautishwa na kibaka
 
lowasa anakwambia tatizo ni uwaziri mkuu lakini kampuni ni safi kabisa..........[/QUOTE]



😱
 
.
Hakuna cha fact zaidi ya upuuzi.Waende kariakoo kufanya nini?Huyu ni Dr wa kienyeji?Huyu bwana harudi tena 2010.Hana jipya.
Ni kweli hana jipya kwa vile ya zamani aliyosema hayajafanyiwa kazi. Kama huyo Rostam wako yuko sawa na anaamini anayowatendea Watz ni sawa basi akavinjari mitaa ya kariakoo aone atakavyo shangiliwa kwa wema wake.
 
Ni kweli hana jipya kwa vile ya zamani aliyosema hayajafanyiwa kazi. Kama huyo Rostam wako yuko sawa na anaamini anayowatendea Watz ni sawa basi akavinjari mitaa ya kariakoo aone atakavyo shangiliwa kwa wema wake.

Kama ameona hayajafanyiwa kazi basi ngoma ni 0-0.A seti mambo mengine kwenye mtandao(Achague ustarabu mwingine).watu tumechoka sasa na hizi ngongera.mpaka wapiga kura wake wanamwita amefulia.Sasa yeye atakaa hapo hapo na ngongera zake akisubiri mambo yafanyiwe kazi?.Ndiyo kufilisika kwenyewe.
 
Mie nadhangaa kelele za siku nyingi za kina mwakyembe et all.

kama wana ushahidi kuhusiana na Rostam basi waende wakafungue mashtaka mahakamani.

We are tired of listening to this cheap politics while Tanzanians are still living very poor life..

Mwakyembe ni kioja tu

If you are tired of listening, u can always use cotton balls
 
Back
Top Bottom