Mwakyembe na Makonda wanampa kiburi Diamond

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2015
Posts
1,527
Reaction score
3,811
Kama mlikuwa hamjui basi sisi wasanii wote tunajua kuwa Basata inatumiwa na Juliana kumsumbua Diamond kwakuwa aliwahi kuzungumza maneno ya kumkashifu hivyo bado ana kinyongo nae.


Mara kadhaa Diamond amekuwa akionana na Mwakyembe, na hata jana Mwakyembe ameulizwa swali la kufungiwa Diamond kasema hawezi kulizungumzia.

Makonda ni mlezi wa WCB. Hivyo Diamond anajivunia watu hao akiamini huyo Shonza hamtishi kwakuwa yeye ana back up ya wakubwa zaidi ya Shonza.

NB: Wasanii tukikaa studi au bar tujadili muziki, tusiwajadili wana muziki na mapungufu yao. Hayo ni majungu
 
Mbona unahangaika mkuu
 
Wewe ndie juliana shonza ?
 
Hivi wewe ni msanii wa miendeko ipi? Hip hop au wabana pua?
 
Hugo dogo hana nidhamu...
Siwapendi clouds lakini inatakiwa azichange karata zake vizuri.
 
Kalapina harakati yule hawezi poteza mda kwenye majungu
Basi ni muimbaji wa Taarabu huyu. Akisogea saaaana atakuwa ni Maua sama ( sijui nimepatia jina lake)

Ila Maua sama a.k.a BABA TUPAC una sauti nzuri sana. Inanikosha ki ukweli. Binafsi si mfuatiliaji wa miziki lakini sauti yako huwa naisikia na inanikosha ki ukweli.
 
Diamond kawashika clouds kila kona nyeti. Ila kwa maendeleo ya muziki na wanamuziki hilo jambo ni jema sana. Mleta mada kama ni msanii kweli basi ni mtumwa na nickname yako nyingine anza kujiita Mtumwa.
 
Siasa na Sanaa; Iwapo wasanii wanatumika kuwaingiza kingi wananchi wakati wa siasa, basi sanaa ni siasa na iwapo wananchi wanalalamikia siasa hakika pia sanaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…