dafity
JF-Expert Member
- Aug 16, 2008
- 1,858
- 2,059
Mwalimu wa Secondary ya BUNDIKANI iliyopo Kibaha Maili Moja Jana Alhamisi July 25, 2024 amempiga ngumi na kumtoa jino bila ganzi mwanafunzi wa kidato cha 3A.
Wanafunzi wote waliopata chini ya alama 30 za somo analofundisha la Hisabati alipanga kuwachapa, mwanafunzi hakikataa kuchapwa na alipokuwa anamchapa mkononi mwanafunzi alitulia bila kuugulia maumivu kitendo ambaco mwalimu aliona ni dharau na kutaka kumchapa makalioni. Mwanafunzi akasema huwa hachapwi makalioni na hata Mwalimu Mkuu na Mwalimu wa malezi wa darasa lao kidato cha 3A wote wanafahamu kibali hicho cha kutochapwa makalioni.
Mwalimu akaanza kumchapa kichwani kitendo kilichomfanya mwanafunzi akimbilie nje ya darasa kujiepusha na adhabu za kiholela. Mwalimu akawahi kufungua milango ndani ndipo alipomtandika ngumi kama mwizi na kumtoa jino Moja na lingine limelegea sana litatoka muda wowote.
Jambo hilo limeshuhudiwa na wanafunzi wote darasani hivyo ushahidi upo.
Je hii ni halali? Mwanafunzi amefuata ELIMU lakini anakutana na ulemavu wa kudumu. Wanahabari wa Mkoa wa Pwani liangazieni swala hilo tena ofisi zenu (Press Club) haizidi hata kilometers Moja kutoka shule ya BUNDIKANI.