Mwalimu afa kwa moto, funguo za nyumba zakutwa nje

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Mwalimu.jpg
Mwalimu wa shule ya sekondari ya Morogoro Daudi Senyagwa, amefariki dunia baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kutekea kwa moto akiwa amelala ndani usiku wa kuamkia leo Juni 15, 2022 katika mtaa wa Seminari, Kata ya Kingolwila Manispaa ya Morogoro.

Wakizungumza na EATV mashuda wa tukio hilo akiwemo Mjumbe wa serikali ya mtaa huo Gregory Tandu, amesema alipigiwa simu majira ya saa 6:00 usiku kuwa kuna nyumba inawaka moto na walienda kujaribu kutoa msaada ilishindikana kwa kuwa walikuwa wachache na moto ulishakuwa mkubwa licha ya kukuta funguo ya nyumba hiyo ikiwa nje ya mlango.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Morogoro, ACP Ralph Meela, amesema uchunguzi wa awali unaonesha kifo cha mwalimu huyo kimetokana na ajali ya moto baada ya kukuta viashilia vya mlipuko wa mtungi wa gesi lakini wataendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo ikiwemo mazingira ya funguo ya nyumba hiyo kuwa nje.

Source: East Africa TV
 
Atupe nje Kwan mlango haufunguki ndani?! Nje laimtupia Nani Hadi waseme watu wlichelewa
Itakuwa alikuja nyumbani akiwa vibaya psychologically, amelewa, au amechoka sana, kafungua mlango akasahau kuchomoa funguo, kaingia ndani na akabandika kitu kwenye jiko la gesi na akajiegesha kitandani huku akingojea kitu kiwe tiari, kitu kile kilikaukia na sufuria kushika moto huku yeye akiwa keshasinzia.
 
kwa hio gesi ikalipuka ufunguo ukatangulia nje ?🤔

hapo kuna waliofanya yao
 
Mwalimu wa shule ya sekondari ya Morogoro Daudi Senyagwa, amefariki dunia baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kutekea kwa moto akiwa amelala ndani usiku wa kuamkia leo Juni 15, 2022 katika mtaa wa Seminari, Kata ya Kingolwila Manispaa ya Morogoro.

Wakizungumza na EATV mashuda wa tukio hilo akiwemo Mjumbe wa serikali ya mtaa huo Gregory Tandu, amesema alipigiwa simu majira ya saa 6:00 usiku kuwa kuna nyumba inawaka moto na walienda kujaribu kutoa msaada ilishindikana kwa kuwa walikuwa wachache na moto ulishakuwa mkubwa licha ya kukuta funguo ya nyumba hiyo ikiwa nje ya mlango.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Morogoro, ACP Ralph Meela, amesema uchunguzi wa awali unaonesha kifo cha mwalimu huyo kimetokana na ajali ya moto baada ya kukuta viashilia vya mlipuko wa mtungi wa gesi lakini wataendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo ikiwemo mazingira ya funguo ya nyumba hiyo kuwa nje.

Source: East Africa TV
Apumzike salama Mwalimu
 
Funguo ilikuwa nje ya mlango ...

Uwe unasoma vizuri...
Pamoja na hayo. Kuna uwezeano kuwa moto ulipokolea aliamua kutupa funguo nje. Nadhani wengi hamjui ajali ya moto ilivyo complex. Milango inaweza kabisa kushindikana kufunguka au kuisogelea. Pia kuna suala la moshi linaloweza kufanya mtu aliyeko ndani kushindwa kuona au ku-focus vizuri. Sasa yeye kwa kiwewe akarusha ufunguo nje ili wafungue kwa nje. Hii siyo conlusion ila najaribu kusema aliyesema marehemu ndiyo alitupa nje asibezwe. Halafu nyumba inaweza kuwa na upenyo kwa chini kwenye mlango hivyo akazirusha akiwa mbali
 
Moto ukiwa unawaka hayo mavyuma huwa yanatanuka kwa sababu ya joto kwahiyo kufungua inakuwa kazi pia changanya na ule moshi mtu unazimia ndo kifo chako
 
Itakuwa alikuja nyumbani akiwa vibaya psychologically, amelewa, au amechoka sana, kafungua mlango akasahau kuchomoa funguo, kaingia ndani na akabandika kitu kwenye jiko la gesi na akajiegesha kitandani huku akingojea kitu kiwe tiari, kitu kile kilikaukia na sufuria kushika moto huku yeye akiwa keshasinzia.

Yawezekana.
 
Back
Top Bottom