Mwalimu afundisha shule nzima

Mwalimu afundisha shule nzima

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,575
SHULE ya Msingi Kiboriani, wilayani Mpwapwa, mkoa wa Dodoma, inakabiliwa na uhaba wa walimu na hivyo kusababisha mwalimu mmoja pekee aliyepo kufundisha darasa la kwanza hadi la saba.
Akizungumza na waandishi wa habari, mwalimu huyo ambaye vilevile ni mkuu wa shule hiyo, Abdalah Fundi, alisema kuwa ana wanafunzi 388 wa darasa la kwanza hadi la saba.
Alisema kutokana na kuwa peke yake shuleni hapo anashindwa kuwamudu wanafunzi hao hali inayosababisha ufanisi wa elimu kuwa mbaya.
Alisema kuwa anakabiliwa na tatizo la okosefu wa walimu na miundombinu ni mibovu kama vile matundu ya vyoo.
Fundi aliongeza kuwa shule hiyo haina matundu ya vyoo vya kudumu bali yanatumika matundu manne ambayo nayo ni ya muda na ni ya kienyeji jambo ambalo ni hatari kwa afya na usalama wa watoto hao.
“Ili upate huduma ya matibabu unalazimika kutembea mwendo wa umbali wa kilomita 21 kutoka hapa kijijini kwenda kutafuta huduma za afya mjini na tunatembea kwa miguu; hakuna usafiri wala barabara bali ni pori tu.
Ofisa Elimu Taaluma wa wilaya hiyo, Ester Kaaya, alikiri kuwepo kwa tatizo hilo shuleni hapo na kwamba shule hiyo ilikuwa na walimu wanne lakini sasa yuko mmoja kutokana na mwingine kuwa katika likizo ya uzazi.
Ester aliongeza kuwa mwalimu mwingine amesimamishwa kazi kutokana na kukabiliwa na makosa ya jinai huku mwingine akiwa katika likizo ya kustaafu Machi.


[TD="bgcolor: #ffffff"]



[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"]
amka2.gif
[/TD]
 
Waalimu wapo, ila serikali 'haina shida' na waalimu japokuwa wanahitajika sana kwa wanafunzi.
Pili, ikiwa mazingira ya kufanyia kazi ni hayo.......
 
mnaambiwa elimu yetu ni janga mnabisha - hapo unaandaa watoto wajifunze kitu gani kama siyo kuwaharibia future yao.
 
ila ikitokea ziara ya kwenda kupongeza kiongozi fulani kwa kupona gon* utaona ambavyo viongozi wetu walivyo makini,mambo ya kutumia akili wao wanatumia nguvu ila ya nguvu ndo wanatafuta makaratasi.
 
Lawama sitaki mpigieni mwenyewe mjue walimu wapya wataajiriwa lini
hizo ndo namba zake mhe. Wa pemba zimbabwe 0784375922
AND
0754315922
PHILIPO MULUGO.
Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom