Mwalimu ahukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kumbaka mwanafunzi na kumpa ujauzito

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mwalimu wa shule ya msingi Isomya, Manispaa ya Singida, Mjengi Samsoni Munkeny, amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kubaka na kumpa mimba mwanafunzi wa darasa la sita katika shule hiyo.

Katika shauri la jinai namba 81/2020, Mwendesha Mashtaka, Patricia Mkina, alidai tukio la kwanza la ubakaji, lilitokea kati ya Aprili, 04,mwaka 2019 na Julai,19,mwaka 2019.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mfawidhi wa Wilaya, Aristida Tarimo alisema, kwamba katika kosa la kwanza la kumbaka mwanafunzi huyo, anamhukumu adhabu ya miaka 30 jela, na katika kosa la pili la kumpa mimba anamhukumu kifungo cha miaka miwili jela, na kwamba adhabu zote zitaenda pamoja.

Awali katika shauri la jinai namba 81/2020, Mwendesha Mashtaka, Patricia Mkina, alidai kwamba tukio la kwanza la ubakaji lilitendwa na mshtakiwa kati ya Aprili 04,mwaka 2019 na Julai 19, mwaka 2019.

Aidha, Mkina alidai siku ya tukio mshtakiwa akiwa katika maeneo ya Kijiji cha Isomya, Kata ya Mwankoko, alimbaka mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa), mwenye umri wa miaka 16, anayesoma katika Shule ya Msingi Isomya.

Katika shtaka la pili la kumpa mimba mwanafunzi, ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka huyo kuwa katika kipindi cha kati ya Aprili 04,mwaka 2019 na Julai,19, mwaka 2019 mshtakiwa huyo baada ya kumbaka alimpa ujauzito mwanafunzi huyo.

Hata hivyo, baada ya mshtakiwa kusomewa mashtaka hayo alikana, na ndipo upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi watano wakati mshtakiwa hakuwa na mashahidi.

Akitoa ushahidi wake, mwanafunzi huyo alidai katika kipindi hicho mara kadhaa wakati akitoka shuleni, mshitakiwa alikuwa akimwelekeza waende vichakani, na walipofika huko alikuwa akimwelekeza kuvua nguo na yeye (mshtakiwa) akivua nguo za kwake.

Mwanafunzi huyo aliieleza mahakama kwamba matukio ya vitendo hivyo yaliendelea hadi Mei, 2019 na ndipo baada ya wazazi wake kuhofia hali aliyokuwanayo waliamua kwenda kumpima, na kugundulika ana ujauzito.

“Baada ya matokeo ya vipimo vya madaktari ndipo wazazi wake walimuuliza kuwa ujauzito huo ni wa nani,ambapo naye alimtaja mwalimu Mjengi Samsoni Munkenyi na ndipo mzazi alipotoa taarifa kwa ofisa mtendaji wa kata, mkuu wa shule na hatimaye kituo cha polisi, ambapo walipatiwa fomu namba tatu (PF3),” alidai Mkina.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka huyo, baada ya kukabidhiwa fomu namba tatu walikwenda Hospitali ya Mkoa wa Singida ndipo pia mwanafunzi huyo aligundulika kuwa na ujauzito wa wiki 16 na ndipo mshtakiwa alipokamatwa na kushtakiwa.

Akitoa utetezi wake, mshtakiwa aliiomba mahakama impe adhabu ndogo kutokana na kuwa na familia inayomtegemea.
 
Huko Singida si ndiko kwa Mr Mzungu? And he is just eating bata kuleeee Belgium
 
Binti aliebakwa ana miaka mingapi?

Hizi sheria ziangaliwe upya jaman, mtawamaliza walimu sasa
 
Walimu nao wamezidi kuwa wajinga, yani unatembea na mwanafunzi mpaka unampa mimba.
 
Hapa bado najiuliza,ina maana wazazi wasingegundua ujauzito kwa yule mtoto wao,yule jamaa angeendelea na mchezo wake na isingegundulika na pia mtoto asingesema.Mi nadhani hapa ubakaji unakuja kwa kuwa ni mwanafuzi,lakini hizo mara zote unaambiwa twende huku unakwenda halafu unabakwa husemi,halafu ukigundulika una ujauzito ndio inakuwa kabakwa!
 
Akitoa ushahidi wake, mwanafunzi huyo alidai katika kipindi hicho mara kadhaa wakati akitoka shuleni, mshitakiwa alikuwa akimwelekeza waende vichakani, na walipofika huko alikuwa akimwelekeza kuvua nguo na yeye (mshtakiwa) akivua nguo za kwake.
Daaaah!
 
Sheria ya mwanafunzi ni mpaka form six. Miaka ni ile ile 30, whether alihiari au la!
 
Polee yake huyo mwalimu, ila walimu nao wamezidi tamaa aaah.
 
Mwalimu wa shule ya msingi Isomya, Manispaa ya Singida, Mjengi Samsoni Munkeny, amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kubaka na kumpa mimba mwanafunzi wa darasa la sita katika shule hiyo.

Katika shauri la jinai namba 81/2020, Mwendesha Mashtaka, Patricia Mkina, alidai tukio la kwanza la ubakaji, lilitokea kati ya Aprili, 04,mwaka 2019 na Julai,19,mwaka 2019.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mfawidhi wa Wilaya, Aristida Tarimo alisema, kwamba katika kosa la kwanza la kumbaka mwanafunzi huyo, anamhukumu adhabu ya miaka 30 jela, na katika kosa la pili la kumpa mimba anamhukumu kifungo cha miaka miwili jela, na kwamba adhabu zote zitaenda pamoja.

Awali katika shauri la jinai namba 81/2020, Mwendesha Mashtaka, Patricia Mkina, alidai kwamba tukio la kwanza la ubakaji lilitendwa na mshtakiwa kati ya Aprili 04,mwaka 2019 na Julai 19, mwaka 2019.

Aidha, Mkina alidai siku ya tukio mshtakiwa akiwa katika maeneo ya Kijiji cha Isomya, Kata ya Mwankoko, alimbaka mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa), mwenye umri wa miaka 16, anayesoma katika Shule ya Msingi Isomya.

Katika shtaka la pili la kumpa mimba mwanafunzi, ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka huyo kuwa katika kipindi cha kati ya Aprili 04,mwaka 2019 na Julai,19, mwaka 2019 mshtakiwa huyo baada ya kumbaka alimpa ujauzito mwanafunzi huyo.

Hata hivyo, baada ya mshtakiwa kusomewa mashtaka hayo alikana, na ndipo upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi watano wakati mshtakiwa hakuwa na mashahidi.

Akitoa ushahidi wake, mwanafunzi huyo alidai katika kipindi hicho mara kadhaa wakati akitoka shuleni, mshitakiwa alikuwa akimwelekeza waende vichakani, na walipofika huko alikuwa akimwelekeza kuvua nguo na yeye (mshtakiwa) akivua nguo za kwake.

Mwanafunzi huyo aliieleza mahakama kwamba matukio ya vitendo hivyo yaliendelea hadi Mei, 2019 na ndipo baada ya wazazi wake kuhofia hali aliyokuwanayo waliamua kwenda kumpima, na kugundulika ana ujauzito.

“Baada ya matokeo ya vipimo vya madaktari ndipo wazazi wake walimuuliza kuwa ujauzito huo ni wa nani,ambapo naye alimtaja mwalimu Mjengi Samsoni Munkenyi na ndipo mzazi alipotoa taarifa kwa ofisa mtendaji wa kata, mkuu wa shule na hatimaye kituo cha polisi, ambapo walipatiwa fomu namba tatu (PF3),” alidai Mkina.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka huyo, baada ya kukabidhiwa fomu namba tatu walikwenda Hospitali ya Mkoa wa Singida ndipo pia mwanafunzi huyo aligundulika kuwa na ujauzito wa wiki 16 na ndipo mshtakiwa alipokamatwa na kushtakiwa.

Akitoa utetezi wake, mshtakiwa aliiomba mahakama impe adhabu ndogo kutokana na kuwa na familia inayomtegemea.
Kwa mfano ikiwa utabaka unahasiwa, si ishi za ubakaji tungekua tunasimuliwa tu leo hii. Siamini kama kuna mtu hapendi kuwa na watoto, nawasilisha 🙂🙂
 
Back
Top Bottom