Wakati mwingine Wanaume tukumbushwe kwamba anayegawa mafanikio ni Mola pekee huku sisi tukichagiza Kwa kufanya kazi Kwa bidii.
Huenda ulikuwa na ndoto ufanikiwe ukiwa na miaka 30, lakini Mungu akakupa hayo mafanikio ukiwa na miaka 50 ama 60 Kwa sababu maalumu.
Huenda Mungu ameona akikupa mafanikio ukiwa na miaka 35 huenda ukakengeuka na kuishia kufa Kwa maradhi kutokana na Umalaya kupitiliza, maana pesa huwabadirisha wengi tabia wakizipata, unless uwe na nidhamu nazo.
Wakati Mwalimu anahisi amechelewa kuona mafanikio yake licha ya kuajiriwa, Kuna Kijana mwingine ametikiza miaka 8 tangu ahitimu Digrii yake pasipo kuajiriwa.
Boniface Mwaitege aliwahi kuimba "Maisha ni foleni........" 🙌