Mkuu nakubaliana nawe kwa 100% maana siyo Ngorongoro tu kwa wamasai/wasonjo hata maeneo ya Shirati kule Tarime kwa wakurya/wajaluo mambo kama haya yapo. Lakini vyombo vya usalama viko wapi kupambana na mambo haya?
Mkuu vyombo vya usalama pekee haviwezi pambana na mambo haya. Inabidi wananchi wa kawaida nao wachukue hatua kwa sababu ndio wanaoishi na hawa wahalifu na waelewa mahali wanapoenda kujificha mara baada ya kosa kutendeka. Hebu fikiria kwa mfano huyo aliyekata mapanga Mwalimu, sio kweli kwamba baada ya kukata alikimbia na kuijficha porini, lazima atakuwa huko kikjijini au kijiji cha jirani na kuna watu wanafahamu mahali alipo, kitu ambacho ni vigumu kwa Mtendaji wa Kijiji, Kata, Tarafa, Polisi na Ofisi ya DC kwa jumla kufahamu. Tena hayo maeneo mengine uliyotaja (Tarime kwa wakurya/wajaluo) kuna kipindi watu walikuwa wanamiliki bunduki haramu tena zenye uwezo mkubwa kama AK 47 na kutembea nazo hadharani kana kwamba nao ni askari !!!! Labda kwa haya makabila ambayo ni mila zao kutembea na silaha za jadi, mila hizi zingepigwa marufuku, maana hata akiwa mkorofi atapokimbia kwenda kuchukua silaha utakuwa umekimbilia mahala salama !!!! kuliko inapokuwa kiunoni au mkononi, mimi nikiwa TZ nikikutana na Mmasai na sime kiunoni huwa naogopa hata kumwangalia maana nadha anaweza niuliza kwa nini namwangalia na kunishushia kipigo.