Mwalimu aliyekatwa mapanga afariki dunia akiwa njiani kuelekea Arusha

Mkuu nakubaliana nawe kwa 100% maana siyo Ngorongoro tu kwa wamasai/wasonjo hata maeneo ya Shirati kule Tarime kwa wakurya/wajaluo mambo kama haya yapo. Lakini vyombo vya usalama viko wapi kupambana na mambo haya?

Mkuu vyombo vya usalama pekee haviwezi pambana na mambo haya. Inabidi wananchi wa kawaida nao wachukue hatua kwa sababu ndio wanaoishi na hawa wahalifu na waelewa mahali wanapoenda kujificha mara baada ya kosa kutendeka. Hebu fikiria kwa mfano huyo aliyekata mapanga Mwalimu, sio kweli kwamba baada ya kukata alikimbia na kuijficha porini, lazima atakuwa huko kikjijini au kijiji cha jirani na kuna watu wanafahamu mahali alipo, kitu ambacho ni vigumu kwa Mtendaji wa Kijiji, Kata, Tarafa, Polisi na Ofisi ya DC kwa jumla kufahamu. Tena hayo maeneo mengine uliyotaja (Tarime kwa wakurya/wajaluo) kuna kipindi watu walikuwa wanamiliki bunduki haramu tena zenye uwezo mkubwa kama AK 47 na kutembea nazo hadharani kana kwamba nao ni askari !!!! Labda kwa haya makabila ambayo ni mila zao kutembea na silaha za jadi, mila hizi zingepigwa marufuku, maana hata akiwa mkorofi atapokimbia kwenda kuchukua silaha utakuwa umekimbilia mahala salama !!!! kuliko inapokuwa kiunoni au mkononi, mimi nikiwa TZ nikikutana na Mmasai na sime kiunoni huwa naogopa hata kumwangalia maana nadha anaweza niuliza kwa nini namwangalia na kunishushia kipigo.
 

Aisee usemacho ni kweli kabisa maana nilikua naongea na msonjo m1 hapa wasso anasema kua yule jamaa alipomjeruhi mwalimu akaenda kwake kujificha ndani na hakuna aliyethubutu kusema mpaka jana taarifa za msiba zinatufikia jamaa alikua anatesa mitaani bila wasiwasi ila kwa leo sijui kama ataonekana. Yawezekana kabisa akakimbilia Kenya.
 

Saddened really, but why?
 
Ni yule mwalimu wa shule ya msingi digodigo wilaya ya Ngorongoro.

Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.

Na yule muuaji hajakamatwa mpaka sasa.

RIP mwalimu.
 
Duh, mambo mengine ni hatari sana!! R.I.P Mwalimu
Hawa watu wa aina hiyo ni kukamata funga hakuna kupoteza pesa za kuendesha kesi za ajabu ajabu kama hii. Sasa kijiji hicho kitapata shida ya walimu, jamaa limekimbia na halitawasaidia chochote!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…