Habarini za majukumu wanajamvi? Nina ndugu yangu ana cheti cha ualimu wa shule ya msingi ila angependa kujiendeleza kwa malengo ya kutaka kubadiri taaluma. Naomba ushauri wenu ili tuweze kujua asome kozi gani haswa kwa ngazi ya diploma na hapo baadae ataendelea. Naomba mchanganuo jamani, nimepewa jukum hili!
Mwambie asome tax management atapata ajira TRA
Sababu za kubadili taaluma ni zipi? Anabadili kwa sababu hataki ualimu? Yeye mwenyewe ana malengo gani? Sasa hivi kuna vijana wanaohitimu shahada wanakaribia kufika/wanafika 40,000 na ajira hazipatikani. Taaluma ambazo zina uhakika wa ajira ni udaktari na ualimu. Katika ushauri wako usisahau suala la ajira.
Mimi nnachukizwa tu na msiojali matumizi sahihi ya maneno kwenye uandishi. Kubadiri ndiyo mdudu gani? Hata kama ulimi ni mzito kupronounce na kuandika nayo shida?
Huyu ndugu yako sio kwamba tu anataka kubadili taaluma bali ni ugumu wa kusoma unamsumbua maana ni kwenye ualimu tu huwezi kusoma diploma bila kumaliza form six.kubadili taaluma kutamcost kupata kazi tena. Mshauri asome masomo ya five na six kwa mwaka mmoja kisha asome diploma ya ualimu.
Yeye anapenda masomo gani? Anaweza kusoma uhasibu au sheria au procurement au human resource. Vyou vipo vingi ada yake tu kama vile T.I.A, C.b.e, st John, St Augustine n. K.
Akimaliza chuo aombe kubadilisha kada ndani ya halmashauri yake. Je anafanyakazi halmashauri gani?