Mwalimu anataka kubadiri Profession (Taaluma) NAOMBA USHAURI

Damson88

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2011
Posts
259
Reaction score
24
Habarini za majukumu wanajamvi? Nina ndugu yangu ana cheti cha ualimu wa shule ya msingi ila angependa kujiendeleza kwa malengo ya kutaka kubadiri taaluma. Naomba ushauri wenu ili tuweze kujua asome kozi gani haswa kwa ngazi ya diploma na hapo baadae ataendelea. Naomba mchanganuo jamani, nimepewa jukum hili!
 
Sababu za kubadili taaluma ni zipi? Anabadili kwa sababu hataki ualimu? Yeye mwenyewe ana malengo gani? Sasa hivi kuna vijana wanaohitimu shahada wanakaribia kufika/wanafika 40,000 na ajira hazipatikani. Taaluma ambazo zina uhakika wa ajira ni udaktari na ualimu. Katika ushauri wako usisahau suala la ajira.
 
Mwambie asome tax management atapata ajira TRA
 
aisee mwambie ajiunge na masomo ya uchungaji au usista, yanalipa sana siku hizi kama ni mroma akasomee na upadri kabisa , akifuzu tu anaendelea na ajira.
Huko akuna lonolongo kabisa sijui ya usaili wala nini.
Hata uustaadhi na ustaadhati unalipa sana,
Yaani unakuwa unakula sadaka kwa kwenda mbele full kuhudumiwa
 
Mimi nnachukizwa tu na msiojali matumizi sahihi ya maneno kwenye uandishi. Kubadiri ndiyo mdudu gani? Hata kama ulimi ni mzito kupronounce na kuandika nayo shida?
 
Huyu ndugu yako sio kwamba tu anataka kubadili taaluma bali ni ugumu wa kusoma unamsumbua maana ni kwenye ualimu tu huwezi kusoma diploma bila kumaliza form six.kubadili taaluma kutamcost kupata kazi tena. Mshauri asome masomo ya five na six kwa mwaka mmoja kisha asome diploma ya ualimu.
 
Yeye anapenda masomo gani? Anaweza kusoma uhasibu au sheria au procurement au human resource. Vyou vipo vingi ada yake tu kama vile T.I.A, C.b.e, st John, St Augustine n. K.
Akimaliza chuo aombe kubadilisha kada ndani ya halmashauri yake. Je anafanyakazi halmashauri gani?
 
Muulize ana malengo gani kwenye maisha yake na anapenda nini? Hapo sasa ndo uzingatie mapendekezo yake umtafutie kozi anayoipenda.
 
Sababu za kubadili taaluma ni zipi? Anabadili kwa sababu hataki ualimu? Yeye mwenyewe ana malengo gani? Sasa hivi kuna vijana wanaohitimu shahada wanakaribia kufika/wanafika 40,000 na ajira hazipatikani. Taaluma ambazo zina uhakika wa ajira ni udaktari na ualimu. Katika ushauri wako usisahau suala la ajira.

Asante sana Bw. Morinyo, nitalizingatia hili pamoja na mlengwa.
 
hahaha wenye wito wachache, mi nimeishapita huko...:smile-big::A S 39:
 
niwie radhi mkuu, nimeishahisi KIFIMBO CHEZA NA WACHAFUZI WA LUGHA. Nje ha yapo bado una ushauri wowote labda?
Mimi nnachukizwa tu na msiojali matumizi sahihi ya maneno kwenye uandishi. Kubadiri ndiyo mdudu gani? Hata kama ulimi ni mzito kupronounce na kuandika nayo shida?
 
Excellent! asante kwa ushauri mkuu.
Huyu ndugu yako sio kwamba tu anataka kubadili taaluma bali ni ugumu wa kusoma unamsumbua maana ni kwenye ualimu tu huwezi kusoma diploma bila kumaliza form six.kubadili taaluma kutamcost kupata kazi tena. Mshauri asome masomo ya five na six kwa mwaka mmoja kisha asome diploma ya ualimu.
 
Yeye anapenda masomo ya accounts pamoja na ugavi..ni mtazamo mzuri kabisa akiombe kwenye halmashauri yake na kama hatokataliwa itakuwa bora. Asante sana Mitihani
Yeye anapenda masomo gani? Anaweza kusoma uhasibu au sheria au procurement au human resource. Vyou vipo vingi ada yake tu kama vile T.I.A, C.b.e, st John, St Augustine n. K.
Akimaliza chuo aombe kubadilisha kada ndani ya halmashauri yake. Je anafanyakazi halmashauri gani?
 
Anadai malengo ni kubadili taaruma na kuongeza kipato, karibu kwa maoni zaidi. Asante
Muulize ana malengo gani kwenye maisha yake na anapenda nini? Hapo sasa ndo uzingatie mapendekezo yake umtafutie kozi anayoipenda.
 
Majukumu mengi Mitihani ya maisha, nipo ila ni kwa kuwa sijapata notification kuhusu hizi threads. Asante kwa angalizo
Nadhani haupo serious umeomba ushauri alafu umekimbia.
 
Back
Top Bottom