GwaB
JF-Expert Member
- Mar 19, 2014
- 4,291
- 5,786
Wadau huu ndio usanii: Ni miezi karibu minne sasa inakaribia kwisha tangu wazo la kuanzisha benki ya Mwalimu Commercial Bank PLC lilipowekwa hadharani na kutangaza uuzwaji wa hisa zake za awali IPO kwa jamii.Tangu zoezi hilo lilipoanza tarehe 23 march 2015 na kufungwa tarehe 4 may 2015,Hakuna taarifa zinazotolewa na wadhamini na benki yenyewe haijajiorodhesha kwenye soko la mitaji kama ratiba yao ilivyoonyeshwa kwenye nakala ya toleo.Tarehe 8 june 2015 ndiyo siku iliyotajwa kuorodheshwa kwenye soko la mitaji.Pamoja na tarehe hiyo iliyotajwa kwenye ratiba kupita,hakuna taarifa zinazotolewa kuhusu bidhaa hii mpya hata kutoka kwa madalali wa soko la hisa.Nafikiri ni uungwana kuwaambia wawekezaji kile kilichojiri katika uwekezaji wao,kukaa kimya haitasaidia.Kama kuna mahali wamekwama katika mchakato mzima wa kuanzisha benki na hatimae kuorodheshwa kwenye soko la hisa hakuna cha aibu kukiri kuwa wamekurupuka. Naomba kuwasilisha.