Mwalimu Commercial Bank IPO

Mwalimu Commercial Bank IPO

GwaB

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2014
Posts
4,291
Reaction score
5,786
Wadau huu ndio usanii: Ni miezi karibu minne sasa inakaribia kwisha tangu wazo la kuanzisha benki ya Mwalimu Commercial Bank PLC lilipowekwa hadharani na kutangaza uuzwaji wa hisa zake za awali IPO kwa jamii.Tangu zoezi hilo lilipoanza tarehe 23 march 2015 na kufungwa tarehe 4 may 2015,Hakuna taarifa zinazotolewa na wadhamini na benki yenyewe haijajiorodhesha kwenye soko la mitaji kama ratiba yao ilivyoonyeshwa kwenye nakala ya toleo.Tarehe 8 june 2015 ndiyo siku iliyotajwa kuorodheshwa kwenye soko la mitaji.Pamoja na tarehe hiyo iliyotajwa kwenye ratiba kupita,hakuna taarifa zinazotolewa kuhusu bidhaa hii mpya hata kutoka kwa madalali wa soko la hisa.Nafikiri ni uungwana kuwaambia wawekezaji kile kilichojiri katika uwekezaji wao,kukaa kimya haitasaidia.Kama kuna mahali wamekwama katika mchakato mzima wa kuanzisha benki na hatimae kuorodheshwa kwenye soko la hisa hakuna cha aibu kukiri kuwa wamekurupuka. Naomba kuwasilisha.
 
Kuna uchelewaji wa kukusanya pesa kutoka kwa wanunuaji hisa. Hasa walionunua kwa njia ya simu.

Soma kwenye link hii chini:

http://www.dailynews.co.tz/index.php/biz/45855-mwalimu-bank-listing-now-june-22
 
Mkuu umezungumzia jambo muhimu sana.

Watu tuliwekeza lakini hadi sasa tuko gizani kuhusu kinachoendelea.

Ni vizuri wahusika wakafahamisha wanahisa kilichochelewesha ratiba ya kusajili hii benki katika soko la hisa la Dar es Salaam.
 
Nikiona NMB walivyotoka 4000+ hadi 3500. Naziogopa hisa kama ukoma
 
Kuna uchelewaji wa kukusanya pesa kutoka kwa wanunuaji hisa. Hasa walionunua kwa njia ya simu.

Soma kwenye link hii chini:

http://www.dailynews.co.tz/index.php/biz/45855-mwalimu-bank-listing-now-june-22

Pamoja na sababu unazozitoa,pamoja na link ulioichapisha,bado hoja inazidi kusimama kwa ukweli kuwa huu ni mwezi wa saba sasa na hakuna taarifa rasmi kuhusu uwekezaji huu.Kama kweli hiyo ndiyo sababu,wahusika wanapaswa kuweka wazi ni nini kinachoendelea na hasa ukizingatia kuwa DSE iko transparent katika uendeshaji wa biashara hii ya mitaji.Nagundua tu kuwa kuna ukosefu wa uzoefu katika shughuri hii na ni bora kukiri tu kuliko kukaa kimya na kutoa taarifa zisizo sahihi. Hiyo link uliyoiweka ina mapungufu mengi tu k.m. Mwandishi anaandika kwamba: ''MWALIMU Commercial Bank (MCB) listing date has been pushed back to two weeks.....!!!". Wakati huo huo mwandishi wa makala hiyo ambaye ni reporter wa Daily news anamnukuu CEO wa DSE Mr Moremi Marwa kwamba ''Collectors wanted time extention as they encountered a challenge of gethering all funds". Hii inaonyesha kuna kutokujua au kuna ubabaishaji wa hali ya juu katika uwekezaji huu katika ngazi zote.
 
Nikiona NMB walivyotoka 4000+ hadi 3500. Naziogopa hisa kama ukoma

Sasahivi zinauzwa 2900, japo hiyo haina maana ya kuwa haziwezi kupanda tena. Hivyo ndivyo biashara ya hisa ilivyo, we ulitaka iwe inapanda tu? kwa wanaoijua hii biashara muda ambao bei imeshuka wao hununua zaidi
 
Kwani wadau hovi hii benk itakuwa na faida gani ya.kipekee kwa walimu?
 
Nilikandamizwa TOL, nikagalagazwa NICOL, na wenzangu wakalia mdomo juu na DECI/DESI, nikakoswa koswa na PA, nikaachwa hewani na SACCOS Fulani, kwa sasa ngoja nipumzike na haya madudu mnayoyaita hisa.
 
Yani kidogo ningenunua hisa za hii bank!!! Duuuh ningeshika kichwa walahi!!!
 
wote mnapiga kelele na hakuna hata mwenye hisa za 500,000 wote 50,000 tu unaikodolea tulioweka mamilioni yetu tumetulia.
 
Back
Top Bottom