Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MWALIMU KIHERE APEWA MTAA SAHARE TANGA
Tanga imemtunuku Mwalimu Kihere Mtaa kwa kutambua mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Siku moja katika miaka ya mwanzo sana baada ya uhuru ikatokea Mwalimu Kihere, Dossa Aziz, Abdul Sykes na Julius Nyerere walikuwa wako pamoja wakawa wanazungumza.
Mwalimu Kihere akawaambia wenzake hawa kuwa itapendeza kama historia ya TANU itaandikwa wao wakiwa hai.
Julius Nyerere akadakia akasema hiyo ni fikra nzuri sana.
Basi wakakubaliana historia ya TANU iandikwe na Nyerere akasema kuwa mtu ambae angefaa sana kuifanya kazi hiyo ni Abdul Sykes.
Nyerere alisema vile kwa kuwa Abdul hakuwa mbali na African Association na TANU na akiijua historia yote.
Bahati mbaya historia hii ilianza kuandikwa pale ofisi ya TANU, Lumumba lakini kazi hii haikufika mbali ikakumbwa na matatizo.
Abdul Sykes akajitoa katika uandishi wa historia ile.
Kisa hiki nimeshakieleza mara nyingi wengi wanakifahamu.
Mwaka wa 1984 Chuo Cha CCM Kivukoni kilipokuja kuchapa kitabu chake, ''Historia ya TANU 1954 - 1977,'' si Mwalimu Kihere wala Abdul Sykes walitajwa ndani ya kitabu hicho.
Hii ndiyo ikawa sababu ya Mwalimu Kiherere na wazalendo wengi kutofahamika katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mwalimu Kihere ana mengi katika historia ya uhuru lakini mimi napenda kisa cha jinsi alivyokusanya fedha za safari ya Nyerere UNO mwaka wa 1955.
Mweka Hazina wa TANU na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika, Iddi Faiz Mafungo akafunga safari kwenda Tanga kwenda kuzichukua fedha hizo.
Wakati Iddi Faiz anarudi Dar es Salaam na fedha hizo basi lake kufika Turiani Iikasimamishwa na Special Branch Iddi Faiz akakamatwa.
Kisa cha kusisimua.
Lakini zaidi napenda sana kumkumbuka Mwalimu Kihere kwa mchango wake katika kuinusuru TANU na mgogoro mkubwa uliotishia kukigawa chama katika makundi mawili hasimu katika mjadala wa Kura Tatu, Parish Hall, Tabora mwaka wa 1958.
Mwalimu Nyerere alitambua kuwa TANU ilikuwa hatarini kwa sababu ya masharti ya kibaguzi ya kupiga kura na kupigiwa kura.
Kwa ajili hii basi siku chache kabla ya mkutano wa Kura Tatu Tabora, Nyerere na Amos Kisenge wakaenda Tanga kukutana na Mwalimu Kihere, Hamisi Heri na Sheikh Abdallah Rashid Sembe kufanya mashauriano ya siri.
Kikao hiki cha mashauriano na kupanga mkakati vipi watakailiana na wapinzani wa Kura Tatu ndani ya chama na dua iliyofanyika Mnyanjani kijiji kidogo nje ya Tanga ndicho kilichompatia Mwalimu Nyerere ushindi na kuwashinda wapinzani wote Kura Tatu wakiongozwa na Sheikh Suleiman Takadir, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU, Makao Makuu, New Street.
Kwa ujanja mkubwa sana Mwenyekiti wa mkutano wa Kura Tatu Mwalimu Nyerere alimpasia Mwalimu Kihere kwa muda kiti chake cha uenyekiti akidai kuwa yeye anataka achangie mjadala kama mjumbe.
Ndoana ikanasa kwenye koo la samaki.
Mwalimu hakujadili bali alitoa hotuba ambayo ilibadili mle ukumbini fikra za wapinzani wengi wa Kura Tatu.
Kwa nusu karne mkakati huu wa Tanga na kisomo cha Mnyanjani kupambana na "wabishi'' ndani ya TANU ilibakia siri kubwa sana na siri hii kubwa ikazidi kuwa siri kubwa kadri miaka ilivyokuwa ikiyoyoma na wazalendo hawa; mmoja baada ya mwingine wakiaga dunia hadi wakabaki wawili, Sheikh Abdallah Rashid Sembe na Nyerere.
Nyerere akiamini kabisa kuwa siri ya Tanga na Mnyanjani itabaki siri hadi karibu mwaka mmoja anafariki 1999 ndipo alipomdhihirikia kuwa siri imefichuka.
Siri ilifichuka mwaka wa 1998 kitabu cha Abdul Sykes kilipochapwa Uingereza.
Bila shaka Mwalimu Nyerere labda alijiuma kidole aliposoma katika kitabu ule mkutano wao wa siri waliofanya Tanga mjini kisha wakahamisha kikao kwenda Mnjanjani walipofanya, ''tawasul,'' usiku kumuomba Allah asahilishe mpango wao waliopanga kuutekeleza Tabora katika Mkutano Mkuu wa TANU kujadili Kura Tatu.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akishiriki katika dua hii.
Wazalendo hawa wanastahili na wana haki ya kukumbukwa kwani wamefanya mengi.
Kwa kweli ni muhimu sana historia zao zikakumbukwa na kuhifadhiwa.
Mwalimu Kihere