Pantomath
JF-Expert Member
- Jan 4, 2019
- 842
- 3,449
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabelya amemtaka Mwalimu Japhet Maganga kurejea kazini kufuatia Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi, Juma Mkomi kutoidhinisha maombi ya mwalimu huyo kupata kibali cha kuazimwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mabelya, Maganga ni muajiriwa wa Manispaa ya Temeke katika nafasi ya ualimu na aliomba kibali cha kuazimwa kwa vipindi tofauti vya miaka mitatu, kuanzia mwaka 2017- 2020, kisha 2020 hadi Septemba 30, 2023.
“Mwalimu Maganga aliomba tena kibali cha kuazimwa kwa mara ya tatu ambapo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi hajaridhia maombi hayo,
“hivyo, Mwalimu Maganga M. Japhet anapaswa kurejea kwenye kituo chake cha kazi mara moja, mnamo tarehe 01, Oktoba 2023,” kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Manispaa ya Temeke.
Itakumbukwa mnamo Januari 25, 2023, Maganga aliteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, ingali ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) lakini hakuafikiana na uteuzi huo.
====
TANGAZO KWA UMMA KUREJESHWA KWENYE KITUO CHA KAZI CHA AWALI MKURUGENZI WA MANISPAA YA TEMEKE ANAPENDA KUTOA TAARIFA KUWA MWALIMU MAGANGA M. JAPHET MWENYE CHECK NO.9607099 MWAJIRIWA WA MANISPAA YA TEMEKE MWENYE CHEO CHA MWALIMU MWANDAMIZI DARAJA A, ALIOMBA KIBALI CHA KUAZIMWA CHA TAREHE 21 AGOSTI, 2017 NA KUPEWA KIBALI CHA KUAZIMWA NA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA (CWT) KWA BARUA KUMB NA. CA.87/164/01/'Β'/160 YA KATIBU MKUU OFISI YA RAIS -UTUMISHI.
KIBALI HIKI KILIKUWA CHA MIAKA MITATU KUANZIA DESEMBA 2017 HADI SEPТЕМВА 30, 2020. AIDHA MWALIMU MAGANGA ALIOMBA NYONGEZA YA KIBALI KWA BARUA YA TAREHE 01 JUNI, 2020 NA KATIBU MKUU OFISI YA RAIS -UTUMISHI ALIMPA KIBALI CHA NYONGEZA KUMB NA CA.164/228/01/'V'/68 CHA TAREHE 10 AGOSTI, 2020 KINACHOISHIA TAREHE 30 SEPTEMBA, 2023.
MWALIMU MAGANGA ALIOMBA TENA KIBALI CHA KUAZIMWA KWA MARA YA TATU AMBAPO KATIBU MKUU OFISI YA RAIS - UTUMISHI HAJARIDHIA MAOMBI HAYO HIVYO BASI MWALIMU MAGANGA M. JAPHET ANAPASWA KUREJEA KWENYE KITUO CHAKE CHA KAZI MARA MOJA MNAMO TAREHE 01 ОКТОВА, 2023.
IMETOLEWA NA:
Pia soma: Katibu mkuu CWT agoma kurudi Temeke kufundisha

MKURUGENZI MANISPAA YA TEMEKE
23.09.2023