Mwalimu Maganga, Katibu Mkuu CWT aliyekataa uteuzi wa Ukuu wa Wilaya arudishwa kwenye Ualimu

Mwalimu Maganga, Katibu Mkuu CWT aliyekataa uteuzi wa Ukuu wa Wilaya arudishwa kwenye Ualimu

Sasa unajua pesa aliyokuwa anapata kama Katibu Mkuu CWT ni kubwa na Ingeweza kulingana na Pesa ya Mkuu wa wilaya.

Ila kwa sasa anapelekwa kurudi kama Mwalimu mwandamizi Daraja A unajua anapata kiasi gani na atafundisha Shule ya msingi unajua udhalilishaji na majuto atakayopata maana hata diwani atakuwa boss wake sasa....KIPI NI BORA?
Bora maskini huru kuliko tajiri mtumwa
 
Bwana Maganga ana akili sana tena kuzidi wewe mtoa mada alijua fika kuwa cheo cha ukuu wa wilaya ni cheo cha kwenda kudhalilishwa na alikuwa ametegwa ali atenguliwe na kupigwa bench kwa mgongo wa kupangiwa kazi nyingine …kwa hiyo alikuwa mbele ya muda na alifikiri zaidi yako….

Hivi kwa akili yako kabisa alikataa tuu bila kujua kitakachotokea? Alijua fika…
Bora afundishe kwa uhuru kabisa kuliko kwenda kudhalilishwa kwenye ukuu wa wilaya…
Yuko wapi jerry muro? Leo tuu mkuu wa wilaya ya Mtwara katenguliwa…

Alifanya jambo sahihi kabisa
Wewe hujielewi unajua mshahara wa mkuu wa wilaya ni sawa na huo wa mwalimu hata angetenguliwa angebaki na mshahara wake wa mkuu wa wilaya na usingeshuka..

Kifupi ni kwamba alijisahau tena sana..
Hii nchi ishi kimachale sana.
 
Kwa hiyo maganga anachezea chaki sahvi

Ova
 
TANGAZO KWA UMMA. Daaah, Would it help nini kwa UMMA? Nimekereka sana na huu us***nge. Walimu wanaonewa sana
 
Walimu wanaonewa sana

Tatizo wanakikumbatia sana chama kongwe dola, kiasi CCM inahisi CWT - Chama cha Waalimu Tanzania ni Jumuiya mojawapo chini ya mwamvuli wao kama ilivyo UVCCM, UWT, WAWAZI pia BAKWATA inavyodaiwa na baadhi ya waTanzania kuwa ni Jumuiya ya CCM.
 
Back
Top Bottom