Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ili wawowane vizuri!Kuna mambo yanasikitisha sana...
Kuna shule huko ifakara sijui ni Mahenge anonimas alitoa uzi kuiomba serikali iingilie kati Kwani viongozi wakule wameshindwa kulifanyia kazi nahuyo mwalimu anazidi kuharibu wanafunzi just imagine mwl ndie anawafosi wamuinamishe! Anajifanya kuwaagiza nyumbani kwake kisha kawaambia wamfanyieAaahaaa
Shule Gani hiyo?
Hizi akili ngumu sana alipwe kulingana kile alichokitendaJeshi la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Masaunga wilayani Bunda, Vicent Nkunguu (39) kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti mwanafunzi wa darasa la sita shuleni hapo kisha kumnywesha sumu.
Akizungumza na Mwananchi kwa simu leo Machi 13, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Salum Morcase amesema vitendo vya ubakaji na ulawiti vilifanyika siku moja kabla ya kunyweshwa sumu siku iliyofuata lengo likiwa ni kupoteza ushahidi.
Kamanda Morcase amesema mwanafunzi huyo (16) alibakwa Machi 8, 2024 usiku akiwa amelala nyumbani kwa mtuhumiwa huyo Kijiji cha Kisorya alipokuwa amekwenda kwa ajili ya kuwapikia watoto wa mtuhumiwa baada ya kuombwa na mke wa mwalimu huyo aliyesafiri kwenda kwenye maombi katika Kijiji cha Igundu.
"Akiwa amelala na watoto chumbani, mwalimu huyo alikwenda kwenye chumba cha watoto na kumwambia mwanafunzi huyo kuwa, amekosa usingizi na kwenda naye kwenye chumba chake ambako alimbaka na kumlawiti," amesema.
Kamanda Morcase amesema baada ya kumaliza haja zake alimruhusu kurudi chumbani kwa watoto na siku iliyofuata mtoto huyo aliitwa na mama yake kwenda kufukuza ndege kwenye shamba lao la mpunga.