Mwalimu mkuu Kiluvya sec amezidisha adhabu

Mamndenyi

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
43,242
Reaction score
60,939
naamba tuongee hii hali ya ticha mkuu kumchapa mwanafunzi fimbo zaidi ya kumi eti hajalipa ada. mbaya zaidi anafanya hivyo wakati mitihani ya moku inaendelea.
 
Zingatia masomo, kuwa mwadilifu, fuata sheria na kanuni za shule. A teacher is there to assist u achieve your goalz.
 
Walimu wengine wanakuwa kama hawana utu jamani, sasa mwanafunzi hajalipa ada anachapwa kwani hilo ni kosa lake?! Ukizingatia mwanafunzi ana mitihani! Ni wakushtakiwa tu huyo mwalimu!
 
Nilikuwa sijajua kama mwanafunzi kuchapwa fimbo zaidi ya kumi ni assistance. Ahsante mkuu!
 
naamba tuongee hii hali ya ticha mkuu kumchapa mwanafunzi fimbo zaidi ya kumi eti hajalipa ada. mbaya zaidi anafanya hivyo wakati mitihani ya moku inaendelea.
<br />
<br />
mkuu! Kuna hatua gan umemchukulia? Au umemuachia mungu!
 
Wakuu, kuna watoto nao wanaudhi sana kama huwezi kujicontrol bora huyo mtoto umwache kwanza ukishatuliza mkali unaongea naye vizuri vinginevyo unaweza kuumiza bure.

Huenda teacher siku hiyo kaingia kazini amefuraaaaaaaa, hasira kibao kwa huyo mtoto na hii inatokea mara nyingi , huenda mtoto naye anamatatizo ya kiafya au aliogopa kutake action yeyote kuhofia kukosa mtihani wa Mock.

Mwalimu alikosea kumchapa mwanafunzi kwani alitakiwa ajue hali halisi ya mtoto na kama inawezekana kuongea na wazazi/mlezi wa huyo mtoto.
 
Katika shule walimu wanawajua sana wanafunzi wakorofi,huyo mwanafunzi inawezekana alikuwa anamjibu mwalimu ovyo na sio kosa lake la kwanza,kwa hiyo tungesikiliza pande zote mbili kwanza na ndipo tujue tumlaumu nani ndio ingekua fear game.Halafu unauhakika gani kama ni kweli huyo mwalimu alitoa hiyo adhabu,inawezekana pia mwanafunzi amemzushia teacher,ili teacher aletewe noma na mzazi wake au na jamii kwa ujumla,kwa hiyo hawa wanafunzi tusiwaamini sana.
Kuna kitu kingine ambacho nisingependa kukiongelea sana kwa sababu sisi tumetokea hukohuko,mimi navyoelewa kumtandika mwanafunzi viboko ni kinyume cha sheria ya nchi na unaweza kumshtaki mwalimu,lakini tusifike huko manake bila viboko hakuna displine.
 
Walimu wengine wanakuwa kama hawana utu jamani, sasa mwanafunzi hajalipa ada anachapwa kwani hilo ni kosa lake?! Ukizingatia mwanafunzi ana mitihani! Ni wakushtakiwa tu huyo mwalimu!

Mtoto wa kike anachapa fimbo zaidi ya kumi mkononi, anashindwa kuandika anaondoka kwenda nyumbani anaacha kufanya mtihani wa moku.
 
Katika shule walimu wanawajua sana wanafunzi wakorofi,huyo mwanafunzi inawezekana alikuwa anamjibu mwalimu ovyo na sio kosa lake la kwanza,kwa hiyo tungesikiliza pande zote mbili kwanza na ndipo tujue tumlaumu nani ndio ingekua fear game.Halafu unauhakika gani kama ni kweli huyo mwalimu alitoa hiyo adhabu,inawezekana pia mwanafunzi amemzushia teacher,ili teacher aletewe noma na mzazi wake au na jamii kwa ujumla,kwa hiyo hawa wanafunzi tusiwaamini sana.
Kuna kitu kingine ambacho nisingependa kukiongelea sana kwa sababu sisi tumetokea hukohuko,mimi navyoelewa kumtandika mwanafunzi viboko ni kinyume cha sheria ya nchi na unaweza kumshtaki mwalimu,lakini tusifike huko manake bila viboko hakuna displine.

Ili kupata uhakika kama kuna mdau humu jamvini mwenye mtoto pale angafanya uchunguzi zaidi, but chanzo changu cha habari ni cha ukweli.
 
<br />
<br />
mkuu! Kuna hatua gan umemchukulia? Au umemuachia mungu!

nimeweka hapa jamvini ili tulijadili, zaidi natafuta namba ya simu ya huyo ticha ili niiweke hapa tupate kuongea naye.
 
Zingatia masomo, kuwa mwadilifu, fuata sheria na kanuni za shule. A teacher is there to assist u achieve your goalz.

ni zaidi ya hayo, na anaposhindwa kufanya mtihani wa moku, unategemea nini matokeo ya huyo mtoto wakati matokeo haya yanaingizwa kwenye final results, more enough watoto wa kike ndo anawatandika kweli kweli.
 
Waelezeni wazazi wenu walifikishe jambo hili ktk kikao cha bodi ya shule lijadiliwe na kupatiwa ufumbuzi. Ikishindikana wazazi wamwone afisa elimu wa wilaya. Meanwhile acheni ukorofi na muendelee na masomo make wanafunzi siku hizi nanyi.............
 
mwacheni awanyoooshe kama mmekula ada mlizopewa na wazazi wenu
naamba tuongee hii hali ya ticha mkuu kumchapa mwanafunzi fimbo zaidi ya kumi eti hajalipa ada. mbaya zaidi anafanya hivyo wakati mitihani ya moku inaendelea.
 
Zingatia masomo, kuwa mwadilifu, fuata sheria na kanuni za shule. A teacher is there to assist u achieve your goalz.

Haya ndo maoni/ushauri/mawazo toka kwako? Unadhani hii ni adhabu stahili?
 
NI wanafunzi wote wanachapwa hizo fimbo kumi au ilitokea kwa bahati mbaya!?

Ni vizuri adhabu itolewe mwalimu akiwa hana hasira......

....hata mzazi nyumbani kwako kumchapa mwanao ukiwa na hasira ni mbaya na hatari sana!

Kingine sio lazima adhabu iwe fimbo!! unaweza kumpa adhabu ambayo ni productive zaidi kuendana na kosa alilofanya ili iweze kumsaida yeye na mwalim pia.

*****Kulea ni kazi sana jamani uchunguzi ufanyike pande zote mbili ili kubainisha tatizo ni nini!!*****
 
Mtoto wa kike anachapa fimbo zaidi ya kumi mkononi, anashindwa kuandika anaondoka kwenda nyumbani anaacha kufanya mtihani wa moku.
We mtoto mtihani wa moku ni nini? Ndivyo ulivyofundishwa shuleni. Huenda ndiyo sababu unachapwa viboko.
 
Back
Top Bottom