The secretary
JF-Expert Member
- Jan 14, 2012
- 4,148
- 2,537
We siku ya kwenda ni bipu tu!
Mi ntajidai kuwa huyo ni mtoto wa sister!
Halafu ntampiga kibao huyo teacher!
Akisimama lbd mie sio kahtaan!
acha kabisa... kuna kibinti kingine bana kilipandisha majini kwa lazima, namaanisha kwa kujilazimisha! aisee, halafu baada ya hapo akaingia staff room na kufanya fujo ya haja!!!
waacheni tu wafeli.. tushaongea mno mpaka sasa ishakuwa kero..
duh.. aisee Fidel80, huu mfumo ni majanga..! kuangalia tu matokeo inahitaji akili nyingine..
sasa kwa mfano hawa waliopata 49, tuwasaidije aisee?
ha ha ha ha, Kiongozi nimecheka kwenye kupandisha majini kwa lazima.
kumi naona kidogo sana! Kuna shule inaitwa TAQWA sec ya mwanza angalia matokeo yao centre no ni 578, kwa walio soma hapo wanafahamu viboko kumi ni vichache sana watu wanatembelea 15 hadi juu!
Mzazi ukubisha beba mwanao tafutashule ingine! but impact yake inaonekana! nncho pinga ni kutoa adhabu bila sababu, Lakini pia isiwe ya kumuumiza bali kumfunza mtoto, lakini kama mtoto anasumbua mvua imnyeshee tu! hawa watoto wetu wa shule za kata jamani hem fanyeni uchunguzi mtajua tu! Alafu kuiendesha shule ya kata inahitaji moyo mgumu sana! lasiivyo mtamlaumu huyo mkuu wa shule bure tu! namleta mada nahisi wewe ni mwalimu wa iyo shule na unamalengo yako hapa!
Wazazi wa .com mnawalemaza sana watoto ndo maana serikali inahangaika kubadili alama za ufaulu, we endelea kumwona huruma akipata Div. IV ya point 45 usije kulalamika hapa
Kuna jambo moja huwa linanikera sana, haswa pale napoona siasa au propaganda katika elimu au malezi kwa ujumla. Na kama wewe ni mzazi naomba nikushauri kuwa kamwe usije ingize swala la propaganda katika kumlea mwanao eti ukajidanganya unatimiza haki za watoto. Mlele kama wewe ulivyolelewa na mzazi wako hadi leo umekua mtu wakuheshimika na jamii.
Hakuna mtu alielelewa kizembe alafu leo umkute anamaisha mazuri, hata nyie humu ni mashahidi
Kwani. Waliochapwa zamani sio mabosi ofisini
Hapo hakuna .com
ni full p.o.box ila wakati mwingine
mzazi ni lazima uangalie adhabu na kosa
kama vina ulinganisho.
Hiyo div natumaini uwe care kwa wanao isitokee tu
ila kwa upande wangu walishapita huko kote.
we ndo mwalimu sasa unaingia darasani unakuta kuna hewa nzito unauliza 'mbona kuna harufu humu ndani' afu ka mwanafunzi bakibencha huko kanajibu 'hata si tumesikia baada ya we kuingia' unafanyaje hapo.
well, thats good!kusema ukweli mimi nikiingia siulizi ili asijeropoka. Shida yangu nitacheka ila kipindi kikiisha natoka naye taratibu halafu atakuja wasimulia wenzake huyu teacher nuksi kweli. Simchapi hata kidogo. Halafu tuone nani atafaidika. Unajua kazi kubwa ya mwalimu ni kulea. Utajisikiaje ukienda ofisini unamkuta kijana anataka umsalimie ndo akusikilize? Wazazi acheni malezi duni. Sisi tunafahamu tunachokifanya. Ila uangalifu mkubwa sana. Ukipayuka namwonea mwanao its ok. Nakuachia umlee. Kuna mchungaji alisema mtoto wake anadhulumiwa na waalimu na wanafunzi wenzake. Aliachiwa amlee mwanaye. Haikuchukuwa miezi 7. Alipatikana na mimba akarudishwa nyumbani. Baadaye akajaribu kuitoa akafariki. UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO. Tena SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI.