Mwalimu mkuu na mhasibu wake watupwa jela kwa MAKOSA ya rushwa

Kisesetusese

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
547
Reaction score
892
Mwalimu mkuu na mhasibu wake watupwa jela kwa MAKOSA ya rushwa.

Mahakama ya Wilaya ya Mbulu imewahukumu aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyamusta, Daniel Gidambisye Murayda, pamoja na Mhasibu wa shule hiyo, James Cosmas Bazil, baada ya kuwatia hatiani kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka yanayohusisha ukiukaji wa taratibu za manunuzi ya umma.

Hukumu hiyo imetolewa Septemba 10, 2026, na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Mbulu, Vitus Kapugi, katika shauri la uhujumu uchumi namba 14623/2026.

Kwa mujibu wa taarifa ya TAKUKURU, washtakiwa walikiuka kanuni za manunuzi ya umma wakati wa utekelezaji wa Water Sanitization Project katika Shule ya Msingi Nyamusta, Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.

Inadaiwa kuwa washtakiwa walishindwa kushindanisha wazabuni na kutoa zabuni ya kusambaza vifaa vya mradi vyenye thamani ya Shilingi 26,447,217.10, kwa upendeleo na kinyume na Sheria, Kanuni za Manunuzi ya Umma pamoja na miongozo ya utekelezaji wa miradi kwa mfumo wa Force Account.

Baada ya kusikilizwa kwa shauri hilo, Mahakama imewatia hatiani washtakiwa wote wawili na kuwahukumu kila mmoja kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani au kulipa faini ya Shilingi milioni moja.

Shauri hilo liliendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Amiri Addy.

My take.
Mwl Wang wa shule ananifanyia mambo ambayo nikiyafikisha kwa boss wake anaweza ama akamtetea au nikamtia aibu.

Iko hivi.
Alinituma Kiki mimi napaswa kulipwa 150k kwa cheo change per diem nikirejea nikaandikia, wnazitumia eye kwanza. Mara ya kwanza nilisafiri dodoma, mara ingine nikasafiri Arusha. Akita nauli yangu. Ananipa wakati anaotaka yeye.

Edge Tanzania hawa watu ni wengi sana
 
Kaka, zima Autocorrect haipendi Kiswahili.
 
Hao Walimu wangekata rufaa hiyo kesi waanze kujitetea upya

Kwenye utetezi wao waseme wao hawana taaluma ya ununuzi na ugavi, badala yake walipewa kufanya kazi ya ugavi na ununuzi wakati sio taaluma yao

Na wao wameajiriwa kufanya kazi ya kufundisha na sio kununua vifaa vya Ujenzi

Huu mtindo wa Walimu kufanywa wanunuzi, Mainjinia kusimamia Ujenzi wa miradi ya shule inabidi waipige marufuku

Kama maDED wanataka kufanya miradi at lower level, basi ifanywe na Idara zake mama za Ujenzi(Miundominu), Ugavi, Fedha na Mipango
 
My take.
Mwl Wang wa shule ananifanyia mambo ambayo nikiyafikisha kwa boss wake anaweza ama akamtetea au nikamtia aibu.

Iko hivi.
Alinituma Kiki mimi napaswa kulipwa 150k kwa cheo change per diem nikirejea nikaandikia, wnazitumia eye kwanza. Mara ya kwanza nilisafiri dodoma, mara ingine nikasafiri Arusha. Akita nauli yangu. Ananipa wakati anaotaka yeye.

Edge Tanzania hawa watu ni wengi sana
Mwalimu hata kuandika tu tatizo, acha wakuonee🤣
 
Inamaana walishindwa hata kutafuta mwanasheria wa kuwasaidia? Au ndio pesa tatizo
 
Walimu wengi huwa na tatizo la kipato kutotosheleza

Hivyo ni vigumu kumudu gharama za kusimamisha Wakili

Ila kwenye hii kesi, wakikata rufaa na kuwa na Wakili wao, ni lazima washinde

Maana kuna lose hole kupitia kufanya kazi isiyo ya taaluma yao
 
Waganga Wafawidhi wa vituo, Walimu, huko Halmashauri wanatumika kufanya kazi za ununuzi na usimamizi wa shughuli za Ujenzi wakati sio taaluma zao

Wahandisi wapo, lakini badala yake wanatumika wao kufanya kazi hizo hasa kwenye hiyo miradi yao ya Force Account

Ushauri wangu kwao, kataeni hizo kazi

Mtakuja kufungwa mpoteze ajira zenu

Hao maDED hawawezi kuwasaidia mkihukumiwa kufungwa kama hivyo

Ndiyo kwanza watatangaza ajira mpya kuziba nafasi zenu
 
Hao Walimu wangekata rufaa hiyo kesi waanze kujitetea upya

Kwenye utetezi wao waseme wao hawana taaluma ya ununuzi na ugavi, badala yake walipewa kufanya kazi ya ugavi na ununuzi wakati sio taaluma yao
Acheni ujuaji wa kijiweni,ingekuwa hivyo Kila mtu angejitetea hakuwa na taaluma Fulani ndo maana ametenda kosa hilo.

Au hujui kuwa ignorance of the law excuses not?
 
Wafungwe Tu maana wamezidi kuwa na tamaa ya vijisenti vya miradi vinavyopelekwa huko mashuleni
 
Watu hawaelewi tu lakini Katika taasisi za uchunguzi zinazo onea sana watu hasa wa hali ya chini ni hao TAKUKURU

Inashangaza kuona kila kiongozi wa kisiasa akikuta kuna changamoto katika miradi ya serikali/umma utasikia anatoa amri kwa TAKUKURU kuchunguza na kuchukua hatua

Hawa jamaa namna wanavyofanya kazi wanajiona wapo juu ya sheria na hukanyaga haki za watu kuliko hata polisi na kwenye kesi hutumia hila na uongo ili tu watu waliowakamata wapatikane na hatia

Ni kwavile tu Watanzania wana mentality kua mtu akishtikiwa kwa kinachoitwa rushwa au matumizi mabaya ya madaraka wanaona lolote la kumkuta na limkute

Sasa linapokuja suala la kushughulikia mafisadi halisi kama wale wanaotajwa katika ripoti za CAG kila mwaka huoni makucha yao
 
Acheni ujuaji wa kijiweni,ingekuwa hivyo Kila mtu angejitetea hakuwa na taaluma Fulani ndo maana ametenda kosa hilo.

Au hujui kuwa ignorance of the law excuses not?
Nimetoa maoni yangu Mkuu, nawe kuwa huru kutoa yako

By the way, nimetoa angalizo pia umuhimu wa kufanya kazi kutokana na taaluma

Kama umesoma makosa waliyohukumiwa nayo yametokana na manunuzi.

Sasa Mwalimu ameajiriwa kifundisha, wewe unampa kazi ya manunuzi, wakati hata sheria na taratibu za manunuzi yenyewe hajui

Kisha unamfunga

Angebaki kwenye kufundisha, angekutwa na hiyo hatia??

Akili ni nywele 🙌
 
Hao Walimu wangekata rufaa hiyo kesi waanze kujitetea upya

Kwenye utetezi wao waseme wao hawana taaluma ya ununuzi na ugavi, badala yake walipewa kufanya kazi ya ugavi na ununuzi wakati sio taaluma yao

Na wao wameajiriwa kufanya kazi ya kufundisha na sio kununua vifaa vya Ujenzi

Huu mtindo wa Walimu kufanywa wanunuzi, Mainjinia kusimamia Ujenzi wa miradi ya shule inabidi waipige marufuku

Kama maDED wanataka kufanya miradi at lower level, basi ifanywe na Idara zake mama za Ujenzi(Miundominu), Ugavi, Fedha na Mipango
Hakika, wao sio wataalamu wa manunuzi wala ugavi.
 
Kama faini ni million Moja Moja walipe kisha waendelee na mengine
 
Mwalimu mkuu na mhasibu wake watupwa jela kwa MAKOSA ya rushwa.

Mahakama ya Wilaya ya Mbulu imewahukumu aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyamusta, Daniel Gidambisye Murayda, pamoja na Mhasibu wa shule hiyo, James Cosmas Bazil, baada ya kuwatia hatiani kwa makosa ya matumizi mabaya ya madaraka yanayohusisha ukiukaji wa taratibu za manunuzi ya umma.

Hukumu hiyo imetolewa Septemba 10, 2026, na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Mbulu, Vitus Kapugi, katika shauri la uhujumu uchumi namba 14623/2026.

Kwa mujibu wa taarifa ya TAKUKURU, washtakiwa walikiuka kanuni za manunuzi ya umma wakati wa utekelezaji wa Water Sanitization Project katika Shule ya Msingi Nyamusta, Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.

Inadaiwa kuwa washtakiwa walishindwa kushindanisha wazabuni na kutoa zabuni ya kusambaza vifaa vya mradi vyenye thamani ya Shilingi 26,447,217.10, kwa upendeleo na kinyume na Sheria, Kanuni za Manunuzi ya Umma pamoja na miongozo ya utekelezaji wa miradi kwa mfumo wa Force Account.

Baada ya kusikilizwa kwa shauri hilo, Mahakama imewatia hatiani washtakiwa wote wawili na kuwahukumu kila mmoja kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani au kulipa faini ya Shilingi milioni moja.

Shauri hilo liliendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Amiri Addy.

My take.
Mwl Wang wa shule ananifanyia mambo ambayo nikiyafikisha kwa boss wake anaweza ama akamtetea au nikamtia aibu.

Iko hivi.
Alinituma Kiki mimi napaswa kulipwa 150k kwa cheo change per diem nikirejea nikaandikia, wnazitumia eye kwanza. Mara ya kwanza nilisafiri dodoma, mara ingine nikasafiri Arusha. Akita nauli yangu. Ananipa wakati anaotaka yeye.

Edge Tanzania hawa watu ni wengi sana
Hao wakikata rufaa wanashinda mapema sana!
 
Back
Top Bottom