Mwalimu mzoefu natafuta kazi ya kufundisha

Mwalimu mzoefu natafuta kazi ya kufundisha

Posho City

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2012
Posts
648
Reaction score
418
Wadau mimi ni mwalimu mwenye diploma na degree ya elimu pia katika elimu ya watu wazima na maendeleo ya jamii.Nimehitimu 2012 lakini kitendo cha kwenda kusoma kilinifanya nifungiwe mshahara serikalini na hatimaye kufutwa payroll.
Tangu 2012 july nikaamua kujikita shule za binafsi na nimefundisha shule maarufu iliyopo Dar hadi mwaka huu mwezi June.

Ninaweza fundisha masomo ya sst yote kwa English medium primary schools,lakini kwa sekondari nafundisha History na Civics.Lakini pia naweza fundisha vyuo vya ualimu na vituo vya elimu ya watu wazima.(refer to my degree program).
Nipo Dar kwa sasa lakini nipo tayari kufanya kazi shule yoyote au chuo cha ualimu nje ya Dar iwapo tutaelewana na utawala husika.

Nimeamua kuweka hili hapa maana shule nyingi nilizopeleka cv hawana nafasi hadi January mwakani.
Pia mtu mwenye kuhitaji mwalimu wa tuition kwa wanafunzi wa English medium primary schools na masomo ya arts kwa sekondary nipo tayari kwa hilo.

Naomba sana nisiweke namba za simu kwao sababu maalum na badala yake kama umeguswa ni pm au weka namba kwenye comment mimi nikupigie.
 
Back
Top Bottom