mayenga
JF-Expert Member
- Sep 6, 2009
- 4,118
- 1,970
Vituo vingi vya televisheni katika wiki hii ya maadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu,vingi vimejikita katika kuonesha hotuba mbali mbali za Mwalimu Nyerere.Licha ya hotuba hizo kuwa na maudhui mazuri,lakini Mwalimu alizidi sana kuchanganya lugha ya kiswahili na lugha ya kiingereza,hata pale alipokuwa akihutubia watu wa kawaida.
Tatizo hli limeendelea kuwa kubwa hata baada ya kifo chake kwa viongozi walio wengi katika taifa hili.Tofauti na Kawawa na Karume katika hotuba zao,Nyerere alipenda usomi wake na umahiri wa lugha uonekane katika hotuba zake.
Kwa namna ya pekee Mkapa alikuwa rais bora katika makuzi ya Kiswahili.Allikuwa akiamua kuongea Kiswahili au kiingereza anakiongea kwa ufasaha mkubwa sana.Tunahitaji kubadilika waungwana.