Mwalimu Nyerere alikuwa mharibifu namba moja wa lugha ya Kiswahili

Mwalimu Nyerere alikuwa mharibifu namba moja wa lugha ya Kiswahili

Lugha ni chombo cha mawasiliano. Inaweza kuwa rasmi(formal) au isiyo rasmi (informal). lugha ya mazungumzo (spoken language) mara nyingi huwa na sifa ya kuwa informal maana yake haizingatii mpangilio sahihi wa kisarufi pia hweza kuchanganya lugha (code switching/mixing) hasa kama unayewasiliana naye anakuelewa. Mwalimu alikuwa akifanya hivo kulingana na watu aliokuwa akizungumza nao. akiwa kijijini kwa wazee alitumia kiswahili fasaha. kama lengo ni kuwasiliana na unayewasiliana naye anakuelewa haliwi tatizo. Tatizo ni kuwa kuna watu wanatetea dhana fulani mfano uzalendo, sijui lugha fulani ni ya wakoloni nk. Tuwaache watu wawe huru wanapowasiliana katika mfumo usio rasmi na si kuwaponda eti wanaonyesha majigambo la! katika hotuba za kuandika utaona ni lugha moja tu inatumika hii ni sahihi.
 
Watu hujenga lugha kwa kufanya utafiti na kuandika si kwa mazungumzo ya kawaida. lengo la mazungumzo ya kawaida ni mawasiliano. mawasiliano ni mchanganyiko wa vitu vingi inaweza kuwa kwa ishara, alama, lugha nk. mtu anapowasiliana na mtu mwingine katika mfumo usio rasmi anahitaji uhuru. kama mtu akichanganya lugha ni kosa basi hata kutumia ishara na alama kama kutikisa kichwa, kupandisha mabega, kutumia mikono kwa namna yoyote, matumizi ya uso na macho nk. basi itakuwa pia ni kuharibu lugha jambo ambalo si kweli. ukimwangalia mwalimu wakati wa hotuba zake utagundua alikuwa anatumia njia nyingi hatulii kama askari aliyeko paredi. alitumia sanaa ya mawasiliano ikiwa ni pamoja na kuchanganya lugha. Pia mwalimu alikuwa na mchango mkubwa kukijenga kiswahili. aliandika mashairi, vitabu na zaidi sera ya matumizi ya kiswahili...
 
Kwani hiyo unayoita wewe kiswahili unaijua au unasema tu? Kwa taarifa yako sisi tunaongea kiarabu feki eti ndio tunaita kiswahili, labda tuondoe maneno ya sasa na kuweka ya Kikabila
 
Tuambie.unataka kumchukulia hatua gani hayati mwl. Nyerere?Ni kweli mleta mada una nia nzuri ya kuijenga nchi yako,au unataka kulinganisha yupi bora kati ya huyu na yule ?Nasema hutufai kabisa wewe.Usitupotezee muda.
 
Umewahi kutathmini hotuba za Mzee Rukhsa? Kama ni Kiswahili huyu alikuwa namba moja kuliko hata Ben Nkapa!!

Nakufananisha Na Muhadhihi Mmoja Pale UDSM , Anamsifia Mama Salma Kwa Kutumia Kiswahili Nje, Sasa Aongee Nn Kama Kiingeleza Hawezi? Nawewe Mzee Mwinyi Achanganye Rugha Ipi Wakati CV Yake Ni Juzuu Kadhaa!
 
Nakufananisha Na Muhadhihi Mmoja Pale UDSM , Anamsifia Mama Salma Kwa Kutumia Kiswahili Nje, Sasa Aongee Nn Kama Kiingeleza Hawezi? Nawewe Mzee Mwinyi Achanganye Rugha Ipi Wakati CV Yake Ni Juzuu Kadhaa!

Una uhakika gani kama hawajui Kiingereza,ambacho hata watoto wa chekechea wanaongea
 
Nakufananisha Na Muhadhihi Mmoja Pale UDSM , Anamsifia Mama Salma Kwa Kutumia Kiswahili Nje, Sasa Aongee Nn Kama Kiingeleza Hawezi? Nawewe Mzee Mwinyi Achanganye Rugha Ipi Wakati CV Yake Ni Juzuu Kadhaa!

Dhana ya kwamba usomi ni kuongea kiengereza ni ulimbukeni ndo nyinyi maofikiria kwamba wazungu wanajua kila kitu hata kama hawajenda shule eti tu wanaongea kiengereza. Wacha mawazo mgando p.a.m.b.a.f.u wahed
 
Back
Top Bottom