Watu hujenga lugha kwa kufanya utafiti na kuandika si kwa mazungumzo ya kawaida. lengo la mazungumzo ya kawaida ni mawasiliano. mawasiliano ni mchanganyiko wa vitu vingi inaweza kuwa kwa ishara, alama, lugha nk. mtu anapowasiliana na mtu mwingine katika mfumo usio rasmi anahitaji uhuru. kama mtu akichanganya lugha ni kosa basi hata kutumia ishara na alama kama kutikisa kichwa, kupandisha mabega, kutumia mikono kwa namna yoyote, matumizi ya uso na macho nk. basi itakuwa pia ni kuharibu lugha jambo ambalo si kweli. ukimwangalia mwalimu wakati wa hotuba zake utagundua alikuwa anatumia njia nyingi hatulii kama askari aliyeko paredi. alitumia sanaa ya mawasiliano ikiwa ni pamoja na kuchanganya lugha. Pia mwalimu alikuwa na mchango mkubwa kukijenga kiswahili. aliandika mashairi, vitabu na zaidi sera ya matumizi ya kiswahili...