Mwalimu Nyerere alinyimwa VISA na taifa kubwa akaiasa Afrika kufanya mabadiliko

Nyerere alikuwa kiongozi mwenye maono tofauti na awamu ya sita iliyojikita kukopakopa hovyo
 
..Mwalimu Nyerere hakuwahi kunyimwa visa, acheni kumsingizia.
Huyu Jingalao hatofautishi kati ya Kunyimwa visa au visa yenye Masharti. Kila nchi Hata Tanzania zinatoa visa zenye masharti... sasa sijui ni kwa nini anaanzisha mada zenye mfanano na jina lake...
 
Walimpa ya kutembea three blocks only...tafuta hotuba yake
 
Walimpa ya kutembea three blocks only...tafuta hotuba yake
Hata ingekuwa one block au zero block bado ilikuwa ni visa...alikuwa na uhuru wa kuchagua kwenda au kutokwenda... Baada ya kuwa Raisi, alikuwa pia na nafasi ya ku-implement hizo aina za visa kwa hao wazungu walio mfanyia hivyo, lakini hakufanya hivyo kwa sababu zake mwenyewe na hata sasa hakuna mwenye nia ya kuwafanyia, ni malalamiko tu kama yako. Sasa huu uonenvu utaisha lini? Auwae kwa upanga, huuwawa kwa upanga.
 
Ndio maana aliasa mabadiliko
 
Siyo kweli, mwalimu alitembelea mataifa yote ya ulaya na yote mpaka Marekani, Kanada na ya ulaya yalikuwa yanampa misaada ya kila aina mfano shule ya sekondari Kibaha iliyoanzishwa na nchi za Skandanavia kwa mfumo wa Taasisi ya Elimu ikijitegemea kwa kila kitu, ikamshinda kuiendeleza imebakia nyangarakasha. Marekani ilizilisha chakula shule zote nchini, Kanada ilitoa misaada mingi sana kwa Tanzania, Israeli ilianzisha JKT na maada wa elimu ya kilimo, Ujerumani nayo ilitoa misaada mingi sana, Uingereza kulikuwa nyumbani kwake kwani haikututawala kama baadhi ya wasiojua historia wanavyojipamba, Urusi ilitoa msaada wa elimu huku china ilijenga reli, tuwe na shukurani tuache visingizio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…