MWALIMU NYERERE ALITAKA CCM IKOSOLEWE,KWA NINI MZEE BULEMBO ANAPINGA CCM KUKOSOLEWA!?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
MWALIMU NYERERE ALITAKA CCM IKOSOLEWE,KWA NINI MZEE BULEMBO ANAPINGA CCM KUKOSOLEWA!?

Nimemtaja makusudi mwanzilishi wa CCM,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili kuvunjilia mbali hizi propoganda zinazotaka kuenezwa kwamba hutakiwi kukosoa chama iwe CCM,CHADEMA,CUF au ACT WAZALENDO.

Na ukumbuke Julius Nyerere haishii kuwa mwanzilishi wa CCM bali ni baba wa taifa hili hivyo alikuwa anafundisha taifa lake kuwa taifa la wakosoaji na siyo waoga wa machawa kila waamkapo kujikomba .

Nimetaja makusudi kwamba Julius Nyerere alitamka waziwazi kuwa alikuwa radhi kuhama CCM kama chama hakikutaka kukosolewa,katika kile kitabu chake alitamka waziwazi tena kwa kurudiarudia kwamba yeye kama Julius Nyerere anaona ni bora kitokee chama kingine kichukue madaraka kuliko CCM isiyotaka kukosolewa..

Kama mkosoaji ni mwongo basi hiyo ni fursa ya kumuumbua ikibidi kumshitaki mahakamani,Je CCM haiwezi kuumbua wakosoaji waongo? Kama mkosoaji anasema ukweli, kama alivyofundisha Mwalimu Julius Nyerere, je CCM haiwezi kujirudi na kufuata ukweli huo kama ilivyojirudi kwa kuitupilia mbali hoja ya serikali tatu ?

Yote haya CCM au chama chochote kinayaweza, basi kifanye hayo,iweje uko madarakani, una tools zote, una wataalam wote na hata kama huna wataalam bado unaweza ku hire wataalamu duniani kuhusu suala lolote, sasa iweje uhangaishwe na mkosoaji mmoja tu au hata umzuie.

Uhai wa kiumbe hai chochote ni kukubali kukosolewa kikaendana na ukweli wa mkosoaji,kwa hiyo waliposhindwa kuzuia kukosolewa akina Julius Caesar, Constatine, Napoleon, Hitler na hata vidikteta vidogovidogo kama Idi Amin vya huku Africa, maana yake hajazaliwa aliyewahi kuzuia watu duniani kukosoa na hatakuja kuzaliwa tuache watu watukosoe ili tujue panapovuja na tupazibe.
 
Bulembo ni chawa mzee ambae ana tumia mbinu ya kujipendekeza kama silaha ya Kujilinda ili asiadhibiwe kwa madhambi aliyoyafanyia chama akiwa kama Mwenyekiti wa wazazi kabla ya kulazimishwa kuachia ngazi!
 
MWALIMU NYERERE ALITAKA CCM IKOSOLEWE,KWA NINI MZEE BULEMBO ANAPINGA CCM KUKOSOLEWA!?

Nimemtaja makusudi mwanzilishi wa CCM,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili kuvunjilia mbali hizi propoganda zinazotaka kuenezwa kwamba hutakiwi kukosoa chama iwe CCM,CHADEMA,CUF au ACT WAZALENDO.

Na ukumbuke Julius Nyerere haishii kuwa mwanzilishi wa CCM bali ni baba wa taifa hili hivyo alikuwa anafundisha taifa lake kuwa taifa la wakosoaji na siyo waoga wa machawa kila waamkapo kujikomba .

Nimetaja makusudi kwamba Julius Nyerere alitamka waziwazi kuwa alikuwa radhi kuhama CCM kama chama hakikutaka kukosolewa,katika kile kitabu chake alitamka waziwazi tena kwa kurudiarudia kwamba yeye kama Julius Nyerere anaona ni bora kitokee chama kingine kichukue madaraka kuliko CCM isiyotaka kukosolewa..

Kama mkosoaji ni mwongo basi hiyo ni fursa ya kumuumbua ikibidi kumshitaki mahakamani,Je CCM haiwezi kuumbua wakosoaji waongo? Kama mkosoaji anasema ukweli, kama alivyofundisha Mwalimu Julius Nyerere, je CCM haiwezi kujirudi na kufuata ukweli huo kama ilivyojirudi kwa kuitupilia mbali hoja ya serikali tatu ?

Yote haya CCM au chama chochote kinayaweza, basi kifanye hayo,iweje uko madarakani, una tools zote, una wataalam wote na hata kama huna wataalam bado unaweza ku hire wataalamu duniani kuhusu suala lolote, sasa iweje uhangaishwe na mkosoaji mmoja tu au hata umzuie.

Uhai wa kiumbe hai chochote ni kukubali kukosolewa kikaendana na ukweli wa mkosoaji,kwa hiyo waliposhindwa kuzuia kukosolewa akina Julius Caesar, Constatine, Napoleon, Hitler na hata vidikteta vidogovidogo kama Idi Amin vya huku Africa, maana yake hajazaliwa aliyewahi kuzuia watu duniani kukosoa na hatakuja kuzaliwa tuache watu watukosoe ili tujue panapovuja na tupazibe.
Samia kama hakuwa makam wa Rais

USSR
 
Anataka uteuzi,nafasi sliyopewa Kinana anatamani angepewa yeye.
 
Back
Top Bottom