Mwalimu Nyerere hadi anafariki alikuwa hafahamu kuendesha gari

Mwalimu Nyerere hadi anafariki alikuwa hafahamu kuendesha gari

issa ramadhani

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2014
Posts
1,319
Reaction score
260
Nadhani kila mwanaJF anaifaham historia ya nguli wa siasa nchini tanzania,baba wa taifa,hayati mwalimu Nyerere.Ndugu ulishawahi kusikia kuwa hayati mwalimu alishawahi kuishi na wake wawili tu katika maisha yake?

Je, ulishawahi kusikia kuwa mwalimu alikuwa hatumii vyakula vyenye gharama kubwa na visivyo na mafuta? Lakini kali zaidi mwalimu hakuwahi kujifunza wala kutaka yaani kuweka nia na yeye aweze kuendesha gari,sasa basi hadi umauti unamkuta alikuwa hajawahi kuendesha gari hata siku moja.

Unamuenzije wewe mwanasiasa au mfuatiliaji siasa kwa hili?
 
Alikuwa anaendeshwa sasa ajifunze kuendesha gari ili iweje?
 
Hao wake wawili ni nani na nani? Naomba uweke bayana. Ni Maria Nyerere na Sophia kawawa, Queen Elizabeth ama nani?

Aendeshe gari la nini wakti siku zote alikuwa akiendeshwa na usalama wa taifa walikuwepo kuhakikisha kila jambo liko sawia?

Hakuwa muhuni kama kina kikwete wa kwenda kwenye madisco usiku na kwa makahaba hivo kutaka kuwa na siri siri za kuendesha magari. Kama vile kikwete pale mbeya akienda block T kwa Maria Mwanjelwa kulala!. Eti raisi!.
 
Hii ya wake wawili ndio naisikia kwako ebu fafanua kiduchu hapo huyu mwanamke mwingine alikuwa na watoto wangapi na ikiwezekana tuwekee na majina yao.
 
Kwani kuendesha gari ni lazima? Ni hitaji la msingi la binadamu ambayo ndio ilikuwa ajenda kuu ya Mwl. kwa Tanzania changa? Wanaotaka kundesha waendeshe, wasiotaka sio lazima.
 
Je, aliwahi kumiliki gari? Vipi kuhusu kuendesha baiskeli? Je, sio zile siasa za wakati ule ndio zilifanya awe hivyo? Kuna mambo mengine ni tabia binafsi na wala hazina mchango katika maendeleo ya nchi!
 
Kwani Mungu Alimuumba Nyerere Ili Ajue kila Kitu? ?

Mbona Husemi hakuwahi kuendesha Ndege?...traikter...pikipiki.... n.k

Hilo ni jambo la kawaida huwezi kujua kila kitu.. na mimi sijawahi ona Raisi wa Tanzania Yeyote akiendesha Gari.. haimaanishi hawajui ila Vyeo vyao haviruhusu
 
Najua watu watamsema mamake na. mbowe..!ila sio yeye..!!
 
Hii ya wake wawili ndio naisikia kwako ebu fafanua kiduchu hapo huyu mwanamke mwingine alikuwa na watoto wangapi na ikiwezekana tuwekee na majina yao.

Huyo wa pili ndiyo mama yake Yeriko Nyerere. Mtu kama hana mpango wa kununua gari kwa nini ajifunze kuendesha?
 
Last edited by a moderator:
Kwani kuendesha gari ni lazima? Ni hitaji la msingi la binadamu ambayo ndio ilikuwa ajenda kuu ya Mwl. kwa Tanzania changa? Wanaotaka kundesha waendeshe, wasiotaka sio lazima.

ni kweli
 
nadhani kila mwanaJF anaifaham historia ya nguli wa siasa nchini tanzania,baba wa taifa,hayati mwalimu nyerere.ndugu ulishawahi kusikia kuwa hayati mwalimu alishawahi kuishi na wake wawili tu katika maisha yake?je ulishawahi kusikia kuwa mwalimu alikuwa hatumii vyakula vyenye gharama kubwa na visivyo na mafuta?lakini kali zaidi mwalimu hakuwahi kujifunza wala kutaka yaani kuweka nia na yeye aweze kuendesha gari,sasa basi hadi umauti unamkuta alikuwa hajawahi kuendesha gari hata siku moja.unamuenzije wewe mwanasiasa au mfuatiliaji siasa kwa hili?

Mada zingine zinachekesha! sasa Nyerere kutoendesha gari ni shida? Isitoshe mtu anawezaje kujua kuendesha trekta but at the same time ashindwe kuendesha gari?! au kwa muanzisha mada trekta siyo gari? [ a tractor is not automobile/vehicle?]
 
nadhani kila mwanaJF anaifaham historia ya nguli wa siasa nchini tanzania,baba wa taifa,hayati mwalimu nyerere.ndugu ulishawahi kusikia kuwa hayati mwalimu alishawahi kuishi na wake wawili tu katika maisha yake?je ulishawahi kusikia kuwa mwalimu alikuwa hatumii vyakula vyenye gharama kubwa na visivyo na mafuta?lakini kali zaidi mwalimu hakuwahi kujifunza wala kutaka yaani kuweka nia na yeye aweze kuendesha gari,sasa basi hadi umauti unamkuta alikuwa hajawahi kuendesha gari hata siku moja.unamuenzije wewe mwanasiasa au mfuatiliaji siasa kwa hili?

Mandela alisema alipokutana na Mwalimu mara ya kwanza, 1962, Mwalimu alikuwa anaendesha gari ndogo aina ya Austin:

"I met with Julius Nyerere, the newly independent country's first president. We talked at his house, which was not at all grand, and I recall that he drove himself in a simple car, a little Austin. This impressed me, for it suggested that he was a man of the people." - (Nelson Mandela, Long Walk to Freedom:The Autobiography of Nelson Mandela, New York: Little, Brown & Co., 1994, p. 538).
 
Back
Top Bottom