Ameonyesha ni jinsi gani mtu mmoja anaweza kulisababishia taifa hasara katika nyanja za kiuchumi, kijamii, kiusalama, kisiasa, na hamna cha kumfanya.
Kinadharia katiba inasema mamlaka yanatoka kwa wananchi lakini kiuhalisia wananchi wamepokwa nguvu, wako powerless, hawawezi kufanya chochote kuiwajibisha serikali, sio kwenye sanduku la kura, sio bungeni ambako ni sawa na mkutano wa halmashauri kuu ya CCM, au hata kutoa maoni tu, na ukinung'unika jiandae kutekwa na kupotezwa.
Magufuli kathibitisha pasipo na shaka kuwa katiba inayotegemea utashi wa mtu mmoja ni moja ya mfumo mbovu kabisa wa kiutawala.
Kaonyesha matundu kwenye katiba yetu ambayo zamani yalikuwa yanasemwa kwa kinadharia, lakini sasahivi tunayashuhudia madhara yake live kutokana na matendo ya mtu mmoja kutodhibitiwa kikatiba na yeye kufanya atakavyo bila kujali wengine.
Magufuli ni kilele cha uthibitisho wa ubovu wa katiba tuliyonayo. Katukwamisha na kuturudisha nyuma. Nchi haina mwelekeo.
Kwa kadhia tuliyopitia hii miaka michache, inaonyesha ni jinsi gani pamoja na kuwa katiba ya warioba ina afadhali kuliko tuliyonayo sasa, bado na yenyewe ina mapungufu.
Tunahitaji katiba mpya, bahati mbaya kwa vile nchi inategemea maamuzi ya mtu mmoja. Hilo tusahau kwa sasa.