Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Hotuba nzuri sana iko hapo chini Mwalimu akionya kuhusu tatizo la udini na ukabila.
Msomaji wangu mmoja kaniletea na kuniomba nimpe fikra zangu kuhusu hii kansa.
Nami nimejitahidi kuliangalia tatizo hili nikipitia historia yake mwenyewe Mwalimu.
Mwalimu Nyerere alipigiwa kura kuwa Rais wa TAA ndani ya ukumbi wa Arnautoglo mwaka wa 1953 na wengi wa waliompigia kura kumchagua walikuwa Waislam.
Kuna video imetengenezwa na TBC1 kuhusu tukio hili la kihistoria nikihojiwa ndani ya ukumbi ule wa Arnautoglo.
Nyerere mwaka wa 1953 hakuwa aliyekuwa anamfahamu.
Alikuwa hajulikani na nafasi hiyo alikuwa anagombea na kijana maarufu wa Dar es Salaam Abdulwahid Sykes aliyekuwa Act. President na Secretary wa TAA.
Halikadhalika alikuwa mmoja wa wafadhili wa TAA pamoja na mdogo wake Ally, Dossa Aziz na John Rupia.
Nyerere alishinda uchaguzi ule.
Uchaguzi huu ndiyo uliobadili historia ya Nyerere.
Nini kimesababisha leo kuwa wananchi wanapiga kura kuchagua viongozi kwa kigezo cha dini na kabila?
Hili swali linahitaji jibu.
Tazama historia ya African Association ilikotoka 1929 hadi kufikia 1954 ilipoundwa TANU.
Tuanze 1954 na turudi nyuma:
Waasisi wa TANU 1954:
1. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
2. Germano Pacha – Jimbo la Magharibi
3. Joseph Kimalando – Jimbo la Kaskazini
4. Japhet Kirilo – Jimbo la Kaskazini
5. C.O. Milinga – Jimbo la Mashariki
6. Abubakari Ilanga – Jimbo la Ziwa
7. L.B. Makaranga – Jimbo la Ziwa
8. Saadani A. Kandoro – Jimbo la Ziwa
9. Suleman M. Kitwana – Jimbo la Ziwa
10. Kisung’uta Gabara – Jimbo la Ziwa
11. Tewa Said Tewa – Jimbo la Mashariki
12. Dossa A. Aziz – Jimbo la Mashariki
13. Abdulwahid Sykes – Jimbo la Mashariki
14. Patrick Kunambi – Jimbo la Mashariki
15. Joseph K. Bantu – Jimbo la Mashariki
16. Ally Sykes – Jimbo la Mashariki
17. John Rupia – Jimbo la Mashariki
Waasisi wa African Association 1929:
1. Cecil Matola (President)
2. Kleist Sykes (Secretary)
3. Mzee bin Sudi
4. Ibrahim Hamisi
5. Zibe Kidasi
6. Suleiman Majisu
7. Ali Said Mpima
8. Rawson Watts
9. Raikes Kusi
TAA Political Subcommittee 1950:
1. Dr. Vedasto Kyaruzi (President)
2. Abdul Sykes (Secretary)
3. Mufti Sheikh Hassan bin Ameir
4. Sheikh Said Chaurembo
5. Hamza Mwapachu
6. Steven Mhando
7. John Rupia
TAA Executive Committee 1953:
1. J.K. Nyerere (President)
2. Abdulwahid Sykes (Vice-President)
3. J.P. Kasella Bantu (General Secretary)
4. Alexander M. Tobias na Waziri Dossa Aziz (Joint Minuting Secretary)
5. John Rupia (Treasurer)
6. Ally K. Sykes (Assistant Treasurer)
7. Committee Members: Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na Patrick Aoko.
(Tanganyika Standard 19 June, 1953)
Denis Phombeah alikuwa Mnyasa kutoka Nyasaland, Dome Budohi Mluya kutoka Kenya, C. Ongalo na Patrick Aoko Wajaluo kutoka Kenya.
Hawa Wakristo na wala hawakuwa Watanganyika.
Hawa wamechaguliwa kuwa viongozi katika TAA na waliowapigia kura ni Waislam.
Kitu gani kilitokea kubadili hali hii na kuingiza uhasama na uadui baina ya wananchi kiasi Mwalimu Nyerere anaonya kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa sababu ya udini na ukabila?
Lakini kwa Tanzania ukabila si tatizo.
Tatizo la Tanzania ni udini.
Hali hii imekujaje?
Nani aliyeleta udini katika siasa Tanzania?
View: https://youtu.be/XgQQoWKh6H0?si=Lw-Jy9ACJHcotbwe