Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MWALIMU NYERERE NA AKINA MAMA WA TANU
Sijui lini CCM itaamka kutoka usingizi mzito na kulitupa pembeni hili blanketi zito walilojigubika kuanzia unyayoni hadi utosini.
Ikajitoa katika huu usingizi wa pono wakakusanya picha alizopiga Mohamed Shebe kuanzia zile alizopiga 1954 katika mikutano ya TANU Viwanja vya Mnazi Mmoja hadi alipopumzika kupiga picha miaka mingi baada ya uhuru.
Hapo chini ni moja ya johari za Mzee Shebe.
Mama zetu wamekuja kupiga kura kumwingiza Julius Nyerere na TANU madarakani uchaguzi wa mwaka wa 1962.
Akina mama hawa wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika walikuwa na nyimbo yao wakimwimbia Nyerere:
Muheshimiwa nakupenda sana,
Wallahi sina mwinginewe,
In Shaa Allah Mungu yupo,
Tanganyika tutajitawala."
Bi. Hawa bint Maftah ndiye akiimbisha nyimbo hii na nyingine nyingi za kuhamasisha umma.
Unaweza kuamini kuwa natafuta picha ya Bi. Hawa Maftah hadi leo sijaipata?
Jana jioni nimepita nje ya Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba Avenue nikachungulia ndani macho yangu yanaangalia kuta za ndani.
Kuta tupu mfano wa jangwa.
Hakuna picha mfano wa hiyo hapo chini kuonyesha historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Nilipokuwa mtoto mdogo kila mimi na baba yangu tukipita nje ya nyumba ya Bi. Hawa Mtaa wa Mkunguni si mbali na ofisi ya TANU wakati ule baba atasimama barazani kwake na kumtolea salamu.
Fanya wema uende zako usingoje shukurani.