lakini Chedieli Mgonja alikuwa waziri wa elimu 1971/1974, na aliyempokea wizara hiyo ni Simon Chiwanga. kwa hiyo inaelekea Mgonja aliondoka wizara ya elimu kwa sababu nyingine na siyo "kuchongewa" na Siwale kama unavyosema.
marehemu Chediel Mgonja "kaghembe" ni mhanga wa siasa za maji taka. wanasiasa wenye chuki toka north pare ndiyo waliokuwa wakimfanyia vituko na kumzushia kila aina ya uongo. mgogoro wa kisiasa dhidi ya Mgonja ulidhoofisha maendeleo ya wilaya ya Pare na kusababisha utengano baina ya jamii moja, kabila moja.
Mgogoro huo ulioanzishwa na wanasiasa wa north pare ambao walikuwa hawawezi kupambana na Mgonja katika medani ya siasa ndiyo umeendelea mpaka ukahamia kwenye Dayosisi ya Pare ya KKKT.
hivi inaingia akilini Mgonja awe anazini na wanafunzi halafu Mwalimu Nyerere aendelee kumteua katika baraza la mawaziri. Tena amwamini kiasi cha kumteua mkuu wa mkoa wa Mtwara wakati vita vya ukombozi wa Msumbiji vimepamba moto?
The Fixer,
Dingswayo,
Queen Esther, Naghenjwa,
tenanzinyo,
MASHANJARA