Mwalimu Nyerere vs Thabita Siwale


sijawahi muona huyu andrew, lakini mara nyingi posts zake zinakuwa na walakini. I think smth is missing upstairs.
 
Wapi Andrew Nyerere atupe version yake?

Wanyakyusa sio watu wakubembeleza bembeleza, Ambangile Mwambungu nae kama Thabitha Mwambenja Siwale alimfukuza shule Andrew Nyerere toka Mkwawa!! Nyerere kama alivyomteua Kamuzora kuwa RDD nae Mwambungu akateuliwa kuwa RDD!! Chezea wanyakyusa wewe hata baba MwanaAsha anajua jeuri yao!!
 

Makongoro Nyerere alisoma Tabora Boys mpaka anaenda jeshini.
 
Ndiyo,huyu Andrew ''something is missing upstairs'' You are not the only one who thinks that.

Funguka Andrew, comments zako mara nyingi zina utata. Tunadhani ipo shidaa fulani kwako!
 

Andrew nyerere amejibu hapo juu ila hakusema kama yeye ndie aliyefukuzwa labda atakuja kueleza hapa kama yeye ndie aliyefuzwa.
 
Last edited by a moderator:

Siyo kweli; mama Tabitha alipandishwa kutokana na ujasiri wa kumshitaki Chediel Mgonja aliyekuwa Waziri wa Elimu wakati huo ila akawa anafanya umalaya na wanafunzi wa kike, mmoja wa wanafunzi waliokuwa wakifanya ufuska na Mgonja alikuwa mwanafunzi wa Korogwe Girls ambako Tabitha alikuwa Headmistress. Hivyo Tabitha akamfuata Mwalimu pale Magogoni akiwa na makbarasha ya ushahidi dhidi ya Mgonja ka kumpa makavu makavu Nyerere kuhusu waziri wake huyo; huku akimtaka akome kuvurugia wanafunzi wake. Ndipo Mwalimu alifurahia ujasiri wa mama yule, akamfuta Mgonja Uwaziri wa Elimu mara moja na kumpa nafasi hiyo mama Tabitha.
 
Roho mbaya ya huyu mama ni ya asili. Aliwahi kuropoka amri mwaka 1982 wakati akiwa waziri. Alisema eti seminary si secondary za kawaida hivyo alizuia wote waliomaliza f 4 seminary wasiendelee f5 kwenye shule za serikari na watu wakaumizwa kirahisi . Wkt huo shule zilikuwa chache ajabu hasa high school. Mama huyu nikimwona nitamani nimwadhibu. Nyambaf
 
Hao wa kutoka seminarini walienda wapi baada ya kumaliza kidato cha nne.
 
Alikuwa headmistress Korogwe Girls na sio Tabora. Her political stardom started with the then infamous Chediel Mgonja flinging with school girls.........I will end here for now!

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/23748-waziri-wa-zamani-chadiel-mgonja-afariki-print.html
 
Mmmghhh Heri yangu mimi ambaye sijasikia chochote.... Better shut up
 
Mkuu hao waliomaliza f4 walilazimika kwenda kubanana kwenye high school chache za seminary hata km hawakutaka, wengine walijiunga na shule za binafsi ila kuna wengi walilazimika kutafuta vyuo mbalimbali.
Ila yote hayo sbb ya wakubwa km huyu mama wameropoka. Too sad.
 

lakini Chedieli Mgonja alikuwa waziri wa elimu 1971/1974, na aliyempokea wizara hiyo ni Simon Chiwanga. kwa hiyo inaelekea Mgonja aliondoka wizara ya elimu kwa sababu nyingine na siyo "kuchongewa" na Siwale kama unavyosema.

marehemu Chediel Mgonja "kaghembe" ni mhanga wa siasa za maji taka. wanasiasa wenye chuki toka north pare ndiyo waliokuwa wakimfanyia vituko na kumzushia kila aina ya uongo. mgogoro wa kisiasa dhidi ya Mgonja ulidhoofisha maendeleo ya wilaya ya Pare na kusababisha utengano baina ya jamii moja, kabila moja.

Mgogoro huo ulioanzishwa na wanasiasa wa north pare ambao walikuwa hawawezi kupambana na Mgonja katika medani ya siasa ndiyo umeendelea mpaka ukahamia kwenye Dayosisi ya Pare ya KKKT.

hivi inaingia akilini Mgonja awe anazini na wanafunzi halafu Mwalimu Nyerere aendelee kumteua katika baraza la mawaziri. Tena amwamini kiasi cha kumteua mkuu wa mkoa wa Mtwara wakati vita vya ukombozi wa Msumbiji vimepamba moto?

The Fixer, Dingswayo, [MENTION=215045]Queen Esther, Naghenjwa, tenanzinyo, MASHANJARA
 
Last edited by a moderator:

Ni kweli, nami niliandika kwa lugha ya mkato tu. Nyerere alikuwa na tabia fulani ambayo labda itasaidia kujua kwa nini Mgonja aliendelea kwenye siasa. Alikuwa mgumu sana wa kufukuza watu wake kwa hiyo alikuwa akiwahamisha kutoka sehemu moja kwenda nyingie; Mgonja alikuwa ni mmoja wa watu wa Nyerere; alikuwa mchapakazi mzuri sana inapokuwa utendaji, ila personal behavior yake tumekuwa tunaiskia kwa watu tu. Mashitaka ya Siwale dhidi ya Mgonja ndiyo yaliyopelekea Mgonja kutolewa Wizara ya Elimu na kufanwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Mtwara ingawa yule mama hakufanywa kuwa Waziri wa Elimu mara moja bali alifanywa waziri wa Nyumba ambayo nadhani pia ilikuwa pia na jukumu la kusimamia mambo ya wanaweke na watoto. Politics za upareni za wakati huo sizifahamu. Friction hiyo baina ya Mgonja na Siwale haikuwa publicized kwenye media bali ilipatikana kutoka kwa watu waliokuwa wakiijua kwa kina, hasa waalimu wa Korogwe Girls; kama unamjua mwalimu mmoja wapo wa Korogwe ghirls wakati huo jaribu kufuatilia.
 
Mkuu suala hapa siyo tu ujasiri was with pia unaangalia na viongozi wenyewe kwan sidhan kamakunakiongozi ambaye ataweza kustahimili aliyostahimili Mwalimu Nyerere.
 
je kwa sasa hivi ni mkuu gani wa shule anaweza kumfukuza mtoto wa rais.?

Jibu ni kwamba hakuna rais au waziri atakae wasomesha watoto wake tanzania..
 
Sawa kabisa ebaeban! Tabitha alipewa uwaziri kwa sababu ya ujasuri wake. Si unajua yule ni Mnyakyusa?

Ila alikija kukosana na Nyerere baada Tabitha kuanza kumdharau mumewe. Kwa vile tu alikuwa waziri!

Safi sana Mwalimu. Siyo hawa kina Pindi Chana ambao ndoa zimewashinda kisa madaraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…