Makundi yalianza 1995 mpaka sasa ndiyo yamekomaa kabisaa, kama si juhudi za Nyerere basi from there tungeanza kupata viongozi wa juu wasio na maadili, wanaotaka kuingia ikulu bila kuwa na strategic plan ya kuleta maendeleo na kutokomeza umasikini unaokula migongo ya watu kila siku.
Kwa sasa ndani ya CCM hakukaliki makundi dhahili yapo mawili sasa ni kundi lipi litashinda jingine hapo ndo mtihani - na ndani ya chama kila mtu ni msemaji na katika wasemaji hao pia kuna wapayukaji, waimba kwaya, ngojera, mashari na makungwi.
Kundi la mafisadi ( wengine wanaliita mwanamtandao) ni wajanja na wezi na wana pesa chafu lukuki na wengi wao wamo ndani ya dola, jingine ni la watu makini sana ila halina pesa chafu.
Cha kusikitisha hakuna ndani ya CCM Mtu kwenye nguvu ya kukemea ndo maana unasikia taarabu na mipasho kila kona hadi masikio yanauma - Mimi Natabiri kumeguka kwa Chama hiki kikubwa vipande viwili na so muda mrefu toka sasa. (Soma Ufunuo wa Nyerere)
Kama CCM haitameguka basi lazima kundi moja likubali yaishe (yaani liwe tumwa la kundi jingine) kitu ambacho hakiningii akilini kabisa.
Kwenye NEC - wanamtandao (mafisadi) wana nguvu ya ajabu wanaweza kabisa kuwaadhibisha hawa wanaojiita wapiganaji - lakini kufanya hivyo basi ni Mwisho wa CCM na hapo ndo tutapata nuru mpya na mapinduzi ya kweli.
Binafsi ningependa CCM imeguke ili tupate kundi safi litusaidie kuongoza kuongeza chachu ya kufikia maendelea kama taifai, kwa sasa CCM imebeba watu na viatu humo humo, yaani kuna watu safi na makini, pia mende hawakosi na ndo wa kwanza kutoa mashairi kwamba mafisadi hakuna ndani ya chama.
Watanzania tunakaribia kupata mapinduzi ya kweli - Alutaa