Mwalimu uliyemtelekeza Mpwayungu Village, tafadhali rudi umchukue mtoto wako

Mwalimu uliyemtelekeza Mpwayungu Village, tafadhali rudi umchukue mtoto wako

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
Tangu ulipomtelekeza kijana huyu hajawa sawa!

- mtoto wako sasa anachukia walimu wote na kukesha akiwazulia kila baya kwa lengo la kujitibu stress ulizomsababishia za kumtelekeza kwa mzazi wake wa kike. Bahati mbaya sasa, anaowashambulia ni mabingwa wa kuhangaika na akili za watu hivyo wanamuelewa na wanajua namna ya kumjibu au kutomjibu katika namna ambayo inamfanya aendelee kuongezekewa na stress.

Dada zangu:
- Si busara kuwahadithia watoto madhira uliyokutana nayo kutoka kwa baba zao.....fanya iwe siri yenu tu na mtoto aambiwe mambo yaliyo positive tu. Kumhadithia mtoto hadi mambo ya kukimbiwa na baba yake matokeo yake ni kuwa na kina mpwayungu wengi hadi kwenye majukwaa ya maana kama jf.

Wadau:
Hivi ni falsafa ya dunia au nini hiki ambacho kinafanya watu wanaobeba uzito zaidi kwenye jamii kudharaulika?!!!!
  • angalia mama zetu wanavyokoga matusi muda wote....viungo vyao vikitajwa hovyo hovyo. Wakati hayo yakiendelea, wao ndiyo nguzo muhimu ya uhai duniani.
  • walimu ndo kama hivyo........kadiri wanavyojitahidi kuwalea watoto wa watu na kuwatoa katika ujinga, ndivyo kina mpwayungu wanavyoongezeka.
  • tunalala kwa amani sababu ya walinzi lakini angalia wanavyodharaulika.
  • tunafurahia viepe huko mijini, lakini angalia maneno ya shombo na kukatisha tamaa wapewayo hao wakulima mara baada ya watu kushiba hivyo viepe.
  • waliotuimbia nyimbo za kizalendo kina bitchuka, tongolanga, atomic jazz n.k wanakufa hata vibanda hawana, wanaokohoa tu wanapata hela ya kununua chochote wanachokitaka.
  • waafrika tumeshiriki mno katika maendeleo ya watu weupe, wakati wa ukoloni na biashara ya utumwa, na hata sasa ambapo tunategemewa nao katika umalighafi lakini hatuishi kudhihakiwa nao.
 
😂😂😂 ila watu wa jf bhn sjawahi jutia kujiunga na huu mtandao kwa kweli kuna burudan ya kipekee kbs
 
Conspiracy theory

Mpwayungu na victim

Are the same person.
 
Back
Top Bottom