Mwalimu wa book keeping kwenda kusahihisha geography NECTA ni sahihi?

The Red Pen

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2014
Posts
517
Reaction score
206
Habari zenu wanajamvi...! Kuna mkasa hapa umenishangaza kidogo.

Kumekuwa na tabia ya wakuu wa shule kuhujumu Baraza la Mitihani kwa kupeleka walimu kufanya marking ya masomo wasiyofundisha wala hawana taaluma ya masomo husika. Kwa mfano mwalimu wa BOOK KEEPING anapewa barua na mkuu wa shule kufanya marking ya Geography ili hali mwalimu husika wa hilo somo yupo.

Hili jambo lilifanywa siri kwa makubaliano ya siri kati ya mkuu wa shule na huyo mwalimu wa Book Keeping huku mwalimu wa Geography akiwa hajui kinachoendelea.

Je wadau hili ni sahihi?
 
Kwa utawala wa ccm hayo yote yamewekwa kuwa sahihi! na sio ilo tu ujazungumzia semina ya walimu wa biology anaenda wa kiswahil, tanzania tunasema mwl anazaraulika lakin mi huwa napnga kwa kusema mwl anajizarau mwenyewe!

kwa kukosa ushirikiano na ugandamizwaj unaosababishwa na maafisa elimu wakurugenz kwa kuwatumia maheadmaster na danganya toto ya tuvisemina..

NDO MANA UTASKIA WATOTO WAMEFAIL KUMBE NDO ILE WAMEPASUA MGUU BADALA YA KICHWA sasa nambien hapo uuyo mwl atasahisha pepa kwa ufasaha -or kwel jaman?????????????????????????????
 
Haya yote ni matokeo ya rushwa katika serikali hii. Walimu wamekuwa vitega uchumi vya maafisa elimu na wakuu wa shule kupitia vifursa uchwara vya semina, kusimamia mitihani na kusahihisha mitihani.

Ili mwalimu aweze kupata nafasi hizo ni lazima atoboke kwa boss wake. Hivyo mkuu wa shule mara zote atapendekeza wale anaojua watamrudishia kitu regardless wana sifa za kufanya kazi hiyo au la.

Walimu wanasikitisha sana ukiwakuta wanavyojikomba komba kwa maafisa elimu na wakuu wa shule ili walau wapate hizo fursa. Ni sheeeeeedaaaa!
 
Mi nasema; Hakuna tatizo kwa mwalim wa Book-keeping kwend sahihisha Geography. Kule kuna tayari mfumo unaofanana wa kusahihishia.

Haendi kufundisha Geography bali kusahihisha. Kwanza maswali yenyewe ni hayo ya kujaza abc?? Kwani anaenda kusahihisha ya kujieleza?

Acheni za kuleta, mwache mwalim mkuu naye ajiinue nyiye mmheshimu. Atapata wapi heshima yake kwenu waalim anao waongoza?? Ukimnyenyekea kama boss wako wengine wanasema anatunyanyasa yaani Tz kila kitu siasa
 
....hata mwalimu Wa siasa anaweza kusahihisha fiziksi, cha msingi kaangalie wanacho fundishwa watoto wetu. mfano somo la sayansi anaulizwa kuku ni...... a. ndege b. kunguru c. binadamu.

chagua jibu sahihi atashindwa kusahihisha hapo akipewa making skimu...
 
mwalimu wa physics anaweza kusahisha geography ila wa geography hawez kusahisha physics.
 

Mkuu hebu fikiria maswali ya "ESSAY"na mengine YA MFUMO HUO yanayohitaji mwanafunzi ajieleze hususani katika Mitihani ya KIDATO CHA PILI;KIDATO CHA NNE;NA KIDATO CHA SITA katika mitihani ya taifa.

Je,ni kweli mwalimu asiyekuwa mtaaluma wa somo husika anaweza kuifanya kazi hii kwa ufanisi?
Hebu tuache ushabiki tuwe wakweli na tujenge hoja za msingi katika hili..
?
 
Sielewi mtindo wa TZ, sana. Ikiwa ni mambo ya ABCD, basi hapo hamna shida. Lakini ikiwa ni mengine, basi hapo kuna shida. Tatizo hilo usilaumu mwalimu, bali laumu NECTA yenyewe. Waje huku Kenya wajifunze jambo kutoka kwa KNEC.

Nilipokuwa mwanafunzi kidato cha nne, yule anayesahihisha Geography Paper 1 (Physical Geography,) hakuwa anasahihisha Geography paper 2 (Human Geography.) Hii ni kwasababu paper 1 na paper 2 yalitofautiana sana. Kiingereza na Kiswahili, Paper 1 (Insha na Lugha) na Paper 2 (Fasihi) zilikuwa na sheria tufauti sana, na yule aliyekuwa amezoa kumark Paper 1, angeona tatizo kumark paper 2.

Ninashangazwa na yule anayesema kuwa eti mwalimu wa fizikia anaweza kusahihisha mtihani wa Jiographia. Labda iwe ni ule mchezo tunaoita "cha baba na mama." Kabla walimu kuanza kusahihisha, ilibidi waufanye mtihani huo huo, na apate zaidi ya 60%. Baada ya hapo, waufanye mtihani huo kama mara mbili hivi, mkijadiliana njia zote zile mwanafunzi anaweza kuwa amelielewa lile swali, an ni wapi mtihani huo unaweza kuwa hujaeleweka vizuri. Baada ya hapo, mnaiunda marking scheme vizuri zaidi na kutunga sheria mpya kwa huo mtihani pekee, kulingana na yale matatizo ambayo hao examiners wameona. Kwa mfano, mtihani wa Paper hisabati mwaka wa 1999, ulikuwa mgumu hadi examiners wakaambiwa wa mark hadi cancelled work. Kama umefanya, kisha ukachora msitari, na ukaandika vibaya, examiners wanakubaliwa kusahihisha ile kazi mbovu. Walimu hawa walikuwa wanasajiliwa na KNEC wenyewe, bali sio mwalimu mkuu wa shule.

Baada ya hapo, wanapelekwa mafunzo, jinsi ya kudetect irregularity na mambo mengine. Mtu huendelea hapo akizidi kupandishwa madaraka. Ukishakuwa examiner kwa mda mrefu, basi unapandishwa cheo na kuwa "team leader." Baada ya hapo unakuwa Senior examiner (Kama ni History paper 1, basi ni senior examiner, History paper 1,) Baada ya hapo ukifanikiwa, basi unazidi kupanda madaraka hadi unakuwa Chief Examiner. Hakuna vile basi unaweza kuja kupewe kazi ambayo hujasomea, na hata hujafundisha. Utaelewaje matatizo yanayowakumba wanafunzi ikiwa hujawahi kuwafundisha na kusahihisha vitabu vyao?
 

Asante kwa ufafanuzi wako mkuu. Hapa kuna tatizo kubwa sana katika mfumo mzima wa Elimu hapa Tanzania.Sekta ya elimu imegeuzwa kichwa cha mwendawazimu. KILA MMOJA ANAJINYOLEA KWA STAILI ANAYOONA ITAMPENDEZA NAFSINI. Siasa imetawala katika mambo ya msingi yanayogusa msitakabali wa maisha ya watu. RUSHWA nayo imekuwa kama muongozo wa kutoa haki.

MASWALI KWA WATENDAJI WA NECTA:-

1:Kwani BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA(NECTA) hawajui kuwa elimu inahujumiwa?

2:Je,hawajui kwamba mitihani ya Taifa inahujumiwa kwa kuibwa au kuvujishwa?

3:Je,Baraza halijui kuwa kuna watu wasiokuwa na sifa za kusahihisha mitihani ya Taifa wanajipenyeza na kwenda kufanya kazi hiyo?

4:Hawajui kuwa hujuma hizo zinafanywa na WAKUU WA SHULE kwa kushirikiana na watendaji wengine WASIOKUWA WAADILIFU?

5: Je,mwalimu akigundua hujuma hizi za wakuu wa shule anaweza kuripoti ngazi ipi?


Wenye DHAMANA hebu tusaidieni hapa.
 
Baraza wanatumia marker walewale miaka nenda rudi, sio utaratibu mzuri sana. Nashauri baraza wawaumie tu wakuu wa shule na data base yao kujua nani anafaa lkn sio kila mwaka mtu huyohuyo, kusimamia huyohuyo, necta form 4 huyohuyo necta form 2 huyohuyo necta form 6 huyo, ni upuuzi mkubwa kabisa. Kibaya zaidi necta haijui utegaji wa mtu katika kazi za kishule, wanawapa viburi marker wa aina hii.

Markers wanaochaguliwa haohao kila mwaka wanasababisha kusimama kazi nyingi sana. Hivi hawo marker hawafundishi masomo yanayohitaji kusahihishwa mwisho wa mwaka?

hivi wanajua huyo mtu wanaemuita anatulia kazini? Tabia za wanaojiita maacordinator kupigia simu ndio wanaharibu kabisa.

kule kule marking unashangaa mtu ameitwa.

Kule kule marking wfundishana stail za ajabu kabisa namna ya ushaihishaji, yaani ni upuuzi mtupu.
 
Hakuna shida kama kukiwa na marking scheme

Na kila mtunga mtihani lazima aandae marking scheme kumrahisishia yeye kufanya marking au mtu yeyote ataye Fanya marking

Walimu mwende shule jamani

Ukisoma teaching methodology huwez lalamikia hili
 
Ni kweli kabisa mkuu.Kuna rafiki yangu mmoja anafundisha shule "X" ya Private jijini Dar alinidokeza kuwa yaani ile shule ni Vituko vya Mkuu wa shule na makamu wake. Barua ilikuja ikiwa inamtaka ateue walimu wasiopungua Watano kwenda kusimamia mtihani wa kidato cha NNE.Lakini cha kushangaza MKUU WA SHULE AKAMTEUA MAKAM WAKE TU akaenda kusimamia. Makamu ametoka huko akaunganisha kusimamia NECTA F2.Makam huyo huyo ametoka kusimamia NECTA F2 akaunganisha kwenda kusahihisha NECTA F2 kwa Ticketi ya Somo la kiingereza huku yeye akiwa siyo mwalimu wa hilo somo na wala hafundishi somo lolote kidato cha Pili.Huku mwalimu wa hilo somo akiachwa solemba.

Lakini maajabu zaidi ni pale mkuu wa shule akishirikiana na huyo makamu wake walipo mpeleka Mwalimu wa Book Keeping akasahihishe Geography na wa Kiswahili ameenda kusahihisha Biology. Taarifa za kuaminika zinadai kuwa haya yote yamefanyika kwa siri kubwa sana huku walimu halisi wa masomo husika wakiwa hawajui kinachoendelea.

Sasa hebu jiulize hapo elimu yetu itakuwa na UFANISI kweli?
 
Wewe mleta mada ni muongo Necta wenyewe ndo wanachagua, anachofanya mkuu wa Shule ni kujaza form kila mwaka ya Walimu walioko kituoni... Mwaka wa kuanza kwzi, TSD no na masomo yanayofundishwa kazi ya Baraza ni kuchagua ingawa pia comment za mkuu zibaanfaliwa
 

Usimwite mtu Muongo ili hali ukiwa hujui mlolongo mzima wa tukio hili.Au ndo wewe unayetenda uozo huu? Kama hutendi basi utakuwa unanufaika kwa namna moja au nyingine...
 
Labda ungesema mitihani inayosimamiwa na TAHOSSA labda ila Necta Mkuu wa shule hahusiki
 
Labda ungesema mitihani inayosimamiwa na TAHOSSA labda ila Necta Mkuu wa shule hahusiki

Wewe unafundisha shule ya serikali au binafsi?

Hao walimu wamepachikwa hapo baada ya walimu husika waliokuwa wanaenda marking kuacha kazi. Hivyo basi barua zilikuja kama kawaida lakini badala ya mkuu wa shule kuwaita wanaostahili barua hizo(walimu wapya walioajiliwa) alifanya dili na kuwaita walim wengine tofauti (wasiohusika) na kuingia makubaliano ya rushwa.

Hivyo wale walimu wakaenda marking kisiri siri. Bila shaka japo kidogo utakuwa umenielewa.
 
Kwa mda mrefu nimekuwa nikitamani kuona vile mitihani ya TZ yanakaa, lakini sikupata uwezo. Siku ya leo, nimefanikiwa kuona mitihani wa kidato cha nne, na nimeshangazwa na kile wanachofanya NECTA.

Kwa kweli, huu sio ubishi, lakini NECTA ni lazima waamke. Nadhani wametilia maanani sana mtihani wa Kidato cha sita hata hawana nafasi ya kushughlikia kidato cha nne. Hii sana sana inahusiana na mitihani ya Kiingereza na Kiswahili. Kweli ukichukua mtihani wa 2013 wa kiingereza na utoe Literature watoto wa darasa la saba ninaowafundisha Sunday School wangepita vizuri sana.

Cha kuudhi kabisa ni kuwa mitihani hii imejaa makosa tele hata nashindwa cha kusema.

Ukiangalia mtihani wa kiswahili, utadhani ni school assignement. Lakini mitihani ya Kidato cha sita naona ni afadhali. Hata yale ya kidato cha nne ya masomo mengine sio mbaya vile, lakini Kiingereza na Kiswahili, kuna shida kubwa sana. Yafaa kuwe na professionalism kiasi.

kidole007 Wajua sio kila kitu ambacho ni lazima utegemee marking scheeme. What if mwanafunzi alifanya Masomo ya ziada, na anapojibu swali, anagusia topic nyingine ambayo inahusiana na hili swali?

Wewe nawe ni examiner, lakini huwezi deviate kutoka kwa marking scheme, utakuwa mwalimu aina gani?
 
Na uyo wa somo la geography akasahahishe Book keeping si ndio? Tatizo lipo hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…