Mwalimu wa book keeping kwenda kusahihisha geography NECTA ni sahihi?


Sasa wewe Mwalimu mpya Huna sifa za kwenda kusahihisha mitihani!! Sifa ni miaka 2, KAZINI ... Acha papara kwa vitu usivyojua!! Hivi! Hamfanyi vikao! Uulize huko!!
 
Sasa wewe Mwalimu mpya Huna sifa za kwenda kusahihisha mitihani!! Sifa ni miaka 2, KAZINI ... Acha papara kwa vitu usivyojua!! Hivi! Hamfanyi vikao! Uulize huko!!

Acha kukurupuka mkuu. Siyo kwamba wale ni walimu wapya kwa maana ya kwamba ndo wameanza kazi ya Ualimu. La hasha! Ni walimu wenye uzoefu wa zaidi ya miaka 4 had hadi 7.Isipokuwa ni walimu wageni katika ile shule. Ni katika kutafuta masilahi.Kwa hiyo walishafundisha shule nyingine wakaamua kusitisha mikataba kutokana na masilahi kuwa kidogo ukilinganisha na WELEDI ULIOTUKUKA walionao.Umeelewa...?
 

MwendaOmo,
Wewe ni mwalimu kitaaluma? au ndio yale yale mambo yetu ya kwakuwa unajua kiingereza basi unaweza kufundisha? Unawezaje kuangalia tu Mtihani na kufikia conclusion uliyoifikia kwamba upo below the standard pasipo kujua kuwa huo mtihani unatokana na muhtasari wa alichofundishwa mwanafunzi kwa kipindi husika? Umetumia instrument gani kujua hayo? Kwa hoja hii nimeku disqualify kwani hujui hata nini maana ya mtihani.
 
Last edited by a moderator:

Taja jina lake na na shule uwasaidie wahusika,
Vinginevyo hasira za kukosa marking/majungu.
 
Taja jina lake na na shule uwasaidie wahusika,
Vinginevyo hasira za kukosa marking/majungu.

Hata Kafulila aliitwa TUMBILI matokeo yake watu wakaambulia aibu.

Hivi unafikiri wote waliotoa michango yao hapa wakiliona hilo ni tatizo wote walikosa marking?

Kwa uelewa wako mfinyu unafikiri wachangiaji wote kwenye jukwaa hili ni walimu?

Jenga hoja. Kama huna uwezo huo basi ni vyema ukatulia ili watu wakuelimishe...
 

I take the second option then.
Halafu huwa sijali wengine wamesemaje kwani The strongest man is he who stands alone.

 
Na uyo wa somo la geography akasahahishe Book keeping si ndio? Tatizo lipo hapo.

Meeting;
Mfuatilie mwenye kuleta hoja asemavyo. Hajasema wa Geography alienda kusahihisha Book keeping. No way. Tatizo hapa ni watu hao wasomi wanapo dharau masomo au mikondo ya wengine bila kuangalia ulinganio. Ulisoma mpaka form v, je katika masomo yako hukuchukua hilo somo?? Ungelinganisha mwalim wa Phyisics kusahihisha Book keeping hapo ndo tofauti. Ndo maana hakuna Head master anayeambiwa awe amechukua combi flani bali Admn.
 

Mkuu, sitakupa qualifications zangu kwa kuwa hayo hayana manufaa katika mjadala huu. Ukweli ni kwamba huwezi ukaseti mtihani aina hiyo kwa watu amabo wamesoma kiingereza kwanzia darasa la tatu hadi kidato cha nne. Iwe silabasi iliyotolewa na wizara ya elimu basi nayo ni hafifu. Lakini sitaguisia methodology ya kuset, bali nitaguzia makosa ambayo yanafanywa na Necta wenyewe. Sasa ikiwa NECTA - ambao ni wataalamu - Kushinda mwalimu wa kawaida, wanafanya makosa ya kitoto, basi mwanafunzi wa Kidato cha nne atafanya nini?

Sentensi ndio hizi; wewe mwenyewe tafuta makosa:

English - CSEE, 2013)
1. These countries cover an area of about 1.8 million square kilometres and, by 2005, the community had a population of about 100 million people.
2. The legislation arm of the East African Community is the East African Legislative Assembly.
3. The Court oversees the interpretation and application of the 1999 treaty that established the EAC.
4. Soil erosion is a problem that causes concern world widely.
5. This is because it has very bad effects on the areas concerned???:confused2:
6. The new development in agriculture and improved methods of farming has helped in prevention of soil erosion .
7. On our way to the air port, we reached a point where there was a heavy traffic jam which stranded us for two hours.
8. When we made a call home, we were told that he was taking bath at home, so we decided to go back.
9 . I was told to go to the airport with my sister around 12:30 noon as he was expected to arrive at 01:00 pm.
10. Imagine that you were invited to your best friend wedding ceremony which was held at Lego hotel.....

Ndugu, hizi ni basic grammar mistakes. Punctuation mbovo, ambiguous sentences, poor spelling. Jamani - na HUU NI MTIHANI ULIOANDIKWA NA NECTA? AU NI MI NIMEPATA KARATASI MBAYA?

Ikiwa NECTA wanaleta mtihani kama huu, basi mwalimu naye atafunza nini? Na mwanafunzi je?

Siwalaumu wananchi wa TZ hata kidogo. Usinichukulie vibaya kamwe. Lakini, huu mtihani, hata ukitoa makosa haya, ulikuwa very SUBSTANDARD kwa mtu amabye anahitajika kusoma Fizikia, Kemia, na masomo mengine kwa lugha ya Kiingereza. Kwa kweli, nimekuwa nikijiuliza inawezekanaje watu wengi wanasoma kiingereza miaka kumi ilhali bado wana tatizo na lugha?

Mzalendo yeyote ni lazima ahuzunishwe na kile wanchofanya hawa. Kwani hata proofreading pekee hakuna? Kwani mtihani unaandikwa na mtu mmoja?

Huu si ungwana. Tafadhali jadili hoja, bali usinijadili mimi. Mimi si hoja.
 

Nimependa jinsi ulivojenga hoja yako. Hata hivyo, hukutufahamisha kuwa swali liliwataka watahiniwa wafanye nini? Yawezekana kuwa walitakiwa kubaini makosa yaliyomo katika sentensi hizo na kuzirekebisha!! Sasa nikijiingiza moja kwa moja kuzidadili sitakuwa nimetenda haki kwa NECTA, pamoja na wadau wa elimu hata kwa hoja yako.
Ni lazima kujiridhisha pasipo kuacha shaka kuwa huo ni mtihani uliotolewa na NECTA, na Pili, What was the question?

Nikishaupata mtihani huo nitarudi kisha tuendelee na mjadala.
 
^ Walimu walio hapa wanaweza kutuhakikishia kama huu ndio mtihani mwenyewe. Au iwe ni mtu anayejaribu kuiga mitihani hiyo.

http://maktaba.tetea.org/wp-content/uploads/2014/05/English-Langauge-2013.pdf

Lile ambalo limenifanya niyalete hapa (ingawa title ya uzi huu ni Geography na Bookkeeping,) ni kwa sababu haya ni makosa yanayoonyesha laxity/ulegevu. Mtihani wa kitaifa unafaa uwe na seriousness kiasi. Na ikiwa mchezo kama huu unaweza ukafanywa, basi naelewa jinsi shule inawezamtuma mwalimu wa bookkeeping kwenda kusahihisha mtihani wa Jiografia.

Kwa maoni na kulingana na vile maswali yalifululizwa, huu ni mtihani ambao hukufanyiwa review wala standardization. kosa lile lile pia liko katika somo la Kiswahili: pahali ambapo Tanzania yaffa itambe kabisa. Hata hivyo, kwa mtihani wa Kidato cha sita, naona ni kama kuna kujitahidi kiwango fulani. Kama watu tunaolipa kodi, lazima tudemand excellence kutoka kwa viongozi wetu. Mara nyingi mi huonekana mbishi napoguzia mambo ya elimu hapa Kenya. Lakini lile ambalo hunikera ni kuwa viongozi wetu hawaelewi kuwa elimu bora ndio msingi wa maendeleo na kujitegemea
 
Hakuna kitu kama hiyo kamwe.....
 
vichekesho zaidi viko katika literature,walimu walio wengi hususani wale wa degree hawaisomi literature vyuoni.sasa wakiajiliwa secondary wanatakiwa wafundishe linguistics na literature kwa kigezo kwamba ktk secondary somo hilo linaitwa English.nilibahatika kumkuta mwalimu ambae hajasomea litr kwa kweli alikua anatia huruma,kwani hana ujuzi wowote tofauti na mwanga alioupata form6.serikari chonde chonde angalieni matatizo kama haya.
 

nimekuelewa,mitihani Mingi ya kwetu Ni bomu tuu, ukicheki mitihani ya English form two unaweza Lia machozi, mwanafunzi anaambiwa aandike opposite of white,women,stupid etc yani maswali ya std 4 anaulizwa mtoto WA form two! Huko kwenye History Ni balaa wanafunzi wanaulizwa wachore ramani saa sijui kwenye geography watafanya nn?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…