MwendaOmo,
Wewe ni mwalimu kitaaluma? au ndio yale yale mambo yetu ya kwakuwa unajua kiingereza basi unaweza kufundisha? Unawezaje kuangalia tu Mtihani na kufikia conclusion uliyoifikia kwamba upo below the standard pasipo kujua kuwa huo mtihani unatokana na muhtasari wa alichofundishwa mwanafunzi kwa kipindi husika? Umetumia instrument gani kujua hayo? Kwa hoja hii nimeku disqualify kwani hujui hata nini maana ya mtihani.
Mkuu, sitakupa qualifications zangu kwa kuwa hayo hayana manufaa katika mjadala huu. Ukweli ni kwamba huwezi ukaseti mtihani aina hiyo kwa watu amabo wamesoma kiingereza kwanzia darasa la tatu hadi kidato cha nne. Iwe silabasi iliyotolewa na wizara ya elimu basi nayo ni hafifu. Lakini sitaguisia methodology ya kuset, bali nitaguzia makosa ambayo yanafanywa na Necta wenyewe. Sasa ikiwa NECTA - ambao ni wataalamu - Kushinda mwalimu wa kawaida, wanafanya makosa ya kitoto, basi mwanafunzi wa Kidato cha nne atafanya nini?
Sentensi ndio hizi; wewe mwenyewe tafuta makosa:
English - CSEE, 2013)
1. These countries cover an area of about 1.8 million square kilometres and, by 2005, the community had a population of about 100 million people.
2. The legislation arm of the East African Community is the East African Legislative Assembly.
3. The Court oversees the interpretation and application of the 1999 treaty that established the EAC.
4. Soil erosion is a problem that causes concern world widely.
5. This is because it has very bad effects on the areas concerned???:confused2:
6. The new development in agriculture and improved methods of farming has helped in prevention of soil erosion .
7. On our way to the air port, we reached a point where there was a heavy traffic jam which stranded us for two hours.
8. When we made a call home, we were told that he was taking bath at home, so we decided to go back.
9 . I was told to go to the airport with my sister around 12:30 noon as he was expected to arrive at 01:00 pm.
10. Imagine that you were invited to your best friend wedding ceremony which was held at Lego hotel.....
Ndugu, hizi ni basic grammar mistakes. Punctuation mbovo, ambiguous sentences, poor spelling. Jamani - na HUU NI MTIHANI ULIOANDIKWA NA NECTA? AU NI MI NIMEPATA KARATASI MBAYA?
Ikiwa NECTA wanaleta mtihani kama huu, basi mwalimu naye atafunza nini? Na mwanafunzi je?
Siwalaumu wananchi wa TZ hata kidogo. Usinichukulie vibaya kamwe. Lakini, huu mtihani, hata ukitoa makosa haya, ulikuwa very SUBSTANDARD kwa mtu amabye anahitajika kusoma Fizikia, Kemia, na masomo mengine kwa lugha ya Kiingereza. Kwa kweli, nimekuwa nikijiuliza inawezekanaje watu wengi wanasoma kiingereza miaka kumi ilhali bado wana tatizo na lugha?
Mzalendo yeyote ni lazima ahuzunishwe na kile wanchofanya hawa. Kwani hata proofreading pekee hakuna? Kwani mtihani unaandikwa na mtu mmoja?
Huu si ungwana. Tafadhali jadili hoja, bali usinijadili mimi. Mimi si hoja.