Mwalimu wa kiingereza wa Diamond Platnumz amefanikiwa

Mwalimu wa kiingereza wa Diamond Platnumz amefanikiwa

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2015
Posts
1,393
Reaction score
3,237
Hatimaye mwalimu wa kiingereza wa diamond na wasanii wengine wa WCB amefanikiwa kumfanya Diamond aongee kiingereza. Nimesikiliza interview aliyoifanya Washington DC Marekani nikashangaa ama kweli hakuna lisilowezekana mtu ukiweka nia.

Interview yenyewe hii hapa chini




Kwa upande wake mwalimu aliyemfundisha Diamond kiingereza ameelezea jinsi alivyokutana na Diamond na akaombwa amfundishe kiingereza. Aidha mwalimu huyo amemsifu Diamond Platnumz kwa kuonesha juhudi ya kutaka kujifunza kiingereza hivyo kujifunza kwa haraka zaidi.
Msikilize mwalimu wake hapa



Hata hivyo lugha ya kiingereza imeendelea kuwa kichomi kwa Harmonize ambaye amejaribu kufanya tour nchini Nigeria na katika interview zake zote anazozifanya hajatuma YouTube na zile alizozituma amemute sauti. Mashabiki wake wamekichukulia kitendo cha harmonize kumute sauti kwenye interview alizozifanya nchini Nigeria kama ishara ya kuwa lugha kwa msanii huyo ni kichomi.



Juhudi za kuzisaka kwa udi na uvumba interview za harmonize alizofanya Nigeria bado zinaendelea.
 
Hatimaye mwalimu wa kiingereza wa diamond na wasanii wengine wa WCB amefanikiwa kumfanya Diamond aongee kiingereza. Nimesikiliza interview aliyoifanya Washington DC Marekani nikashangaa ama kweli hakuna lisilowezekana mtu ukiweka nia.
Interview yenyewe hii hapa chini

.

Zamani tuliaminishwa kuwa Ras Simba peke yake ndiye anayeweza kumfundisha mtu kikristo na akawa fundi hasa...
 
kajua kiingereza na muziki umeisha!!!..siku hizi dogo anavuruga tu kikazi
 
Mshikaji anatema yai kama kazaliwa Manchester kumbe mtoto wa kwa Bibi paka
Kulingana na elimu yake na background yake amejitahidi sana. Au labda niseme ushamba wetu wabongo ndiyo unatufanya kuona kama amefanya kitu cha maana. Angekuwa amejifunza kijaluo tungemsifia? Lakini mimi nimegundua mushkeli fulani fulani kwenye kiingereza chake:
1. Anajaribu kuiga lafudhi na kiingereza cha black americans! Hili ni kosa kubwa katika kijifunza lugha. Au labda niseme siyo kosa kama unapatia na umekuwa nguli kwenye lugha yenyewe. Tatizo lipo pale unapokuja kujisahau na kuchanganya lafudhi. Hili nimeliona kwa mnigeria mmoja alikuwa anajifanya na slang za kimarekani lakini siku aliyokamatwa na polisi mara kikageuka kuwa pigeon english wanayozungumza West Africans.
2. Nimegundua siyo mzuri kama watu wengi wanavyodhani kwani hiyo interview aliandaliwa na alikariri mambo mengi eg historia ya maisha yake (unaweza kugundua kwa jinsi anvyoongea). Nina uhakika ukimkurupusha vuu bin ghafla na kuongea naye subject ambayo utaichagua randomly hayuko vizuri kama inavyoonekana na lafudhi yake itarudi kuwa ya kiswahili.
 
Kujifunza lugha za kigeni darasani huwezi kuongea kwa ufasaha lugha hiyo kama mtu aliyekaa na watu wanaoongea lugha hiyo. Ndo maana bongo unakuta mtu ana phd lakini lete mdahalo wa kiingereza unaweza kucheka.hivyo kaa na wahusika wa lugha hiyo halafu jitahidi usiongee kiswahili kwa muda wewe ni kiingereza mda wote hapo lazima uwe vizuri.
 
ndo mana nashangaa hapa PM kuna sms ya kingereza itakuwa ye nd kantumia
 
F0AF0723-CB7D-4F5A-8798-4913AF80C1BD.jpeg
Focus!
 
Back
Top Bottom