Mfumo wetu wa elimu ni mbovu sana, na unazalisha watu wabovu. Ukiangalia elimu ya TZ kwa ujumla aliyefeli na aliyepasi wote ni zao lile lile, iweje mtu afaulu kwa wizi wa mtihani, au kwa kukariri majibu tu. Zao la elimu yetu siyo critical, analytical wala visionary.
Kufeli ni tatizo moja na kukata taaa ni tatizo lingine, kwenye aisha hakuna kufeli kun -changamoto. Haiingii akilini mtoto kufeli masomo lazima kuwe na sababu za msingi, na hawa watoto tuna wa brabd failure wanakuwa anyo na kuikubali. Tubomoe mfumo wetu wa elimu sioni kama mitihani ya form four na six inatija kwani haipi uwezo halisi wa watoto wetu.
Haiwezekani mtoto alikuwa na maendeleo mazuri kwa miaka minne akafeli mtihani mmoja tu ukawa amepoteza miaka yake yote miine bure. Kama alifaulu form one, two, three lazima kuwe na sababu za msingi sana kufeshindwa mtihani mmoja tu wa mwisho kwenye somo husika.
Badala ya bkupigia kelele haya madara ya kufaulu je hata hao waliofaulu wanatofauti gani na hao walioshindwa?? Je hao wanaomaliza vyuo vikuu wanatofauti gani na hawa wa form six?? Elimu yetu inatayarisha wataalamu na watengeneza ajira au linazalisha mzigo kwa taifa. Kwa nini kila kada awe daktari au injinia yuko tayari kufanya kazi voda kwa kisingizio cha ajira hawawezi kujiajiri. Majibu ni elimu yetu haiandae kizazi kujitegemea.
Division mbovu tutaendelea kuziona sana na zitatuhudmia kwani ndio wengi tunaozalisha kwa ukosefu sio wa waalimu wabovu tu bali shule, mitaala, ukosefu wa vitabu nk vibovu.
Sio waliofeli tu wanatufundisha bali wanatutibu, wanatujengea nyumba zinazoanguka, wanatutawala, wanatuendesha, wanatutengenezea vyakula, ndio tunaowategemea sana halafu tunashangaa nchi haiendelei. Itaendeleaje wakati tumeandaa vihiyo watupu.
Mfumo wa elimu yetu ni mbovu sio alama ndio tatizo.