JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Akisoma mashtaka hayo jana Agosti 15, 2024, Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali, Charles Magonza aliiambia mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, John Mdoe kuwa mtuhumiwa alikuwa akimnajisi mtoto huyo (jina limehifadhiwa) chooni kipindi cha kunywa uji.
Soma Pia: Mwalimu Mkuu adaiwa kumlawiti mwanafunzi Bunda
Alidai Julai 26, 2024 kati ya saa 1 na saa 2 usiku bibi wa mtoto huyo alibaini mtoto huyo kufanyiwa vitendo vya unajisi baada ya kumkagua na kuona alivyoharibiwa.
Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Adhabu Sura ya 16 marejeo ya Mwaka 2022 Kifungu cha 154 Sura Ndogo ya 15 ya Makosa ya Utu, mtu atakayemwingilia mwenzake kinyume cha maumbile kwa lazima ama kwa kutaka mwenyewe adhabu yake/zao wote ni kifungo cha maisha gerezani au kifungo cha miaka 30 jela.
Mshtakiwa Elias baada ya kusomewa mashitaka yake alikana kutenda kosa hilo kwa mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka saba.
Chanzo: Habari Leo